Familia Dar yagombea kuzika maiti ya baba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Familia Dar yagombea kuzika maiti ya baba

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,770
  Likes Received: 4,911
  Trophy Points: 280
  Sakata la kugombea mwili wa marehemu Gerald Ngindo uliokuwa unatarajiwa kuzikwa wiki iliyopita huko Tabata Chang'ombe, limezua mzozo baina ya pande mbili za familia kila mmoja akitaka ichukue maiti hiyo na kuizika.

  Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Afumwisye Kibona.

  Upande wa wakili wa utetezi, Mussa Roma ambaye anatetea mke wa mwisho marehemu aliyefungua kesi hiyo alidai kuwa marehemu awali alikuwa ni Mkristo na alishawahi kuwa na wanawake wengi ukiachiliambali yeye aliyekuwa akiishi naye.

  Alisema kuwa pande hizo mbili zinagombea maiti upande wa mwanamke wa kwanza na wa pili wanataka azikwe Kikristo wakati mke wa tatu, Kundra Salum, akitaka izikwe Kiislamu.

  Roma alidai kuwa marehemu alikuwa anaishi na Kundra na ndipo walipokubaliana kufunga ndoa ya Kiisilamu hivyo kubadilisha dini na kuitwa Salimu Ngindo.

  Roma alidai kuwa marehemu alibadilisha dini yake ya Kikiristo na kuwa Muisilamu katika msikiti wa Tabata Chang'ombe unaojulikana kwa jina la Masjid Adil.

  Wakili alidai kuwa ndoa hiyo ilifungwa Aprili 10, mwaka 1994 marehemu akiwa ameshabadilisha dini na alifanikiwa kuzaa mtoto mmoja na Kundra anaitwa Adamu Salimu.
  Roma alidia kuwa suala la marehemu huyo kubadili dini lilifahamika kwa ndugu zake.

  Hata hivyo wakili huyo alidai kuwa marehemu amekuwa akiugua kwa zaidi ya miaka sita iliyopita na alikuwa akiuguzwa na Kundra.

  Roma alidai kuwa marehemu alifariki dunia Februari 24, 2010 katika Hospitali ya Hindu Mandal.

  Alidai kuwa Kundra alitoa taarifa kwa ndugu wa marehemu kuhusu msiba huo kwa ajili ya kushiriki mazishi.

  Aliieleza kuwa kwa dini ya Kiislamu haitakiwi mwili wa marehemu kukaa muda mrefu ila kuzikwa hivyo walifanya busara kusubiri ndugu ili kufanya mazishi kwa pamoja.

  Roma alidai kuwa ndugu hao walipofika waliungana na kupanga taratibu za mazishi.

  Alidai kuwa maiti hiyo ilitakiwa kuzikwa Feebruari 26 na kwamba walitoka nyumbani pamoja lakini walipofika hospitalini, walikataliwa kuchukua mwili kwa madai kuwa ndugu wa marehemu walishachukua kibali cha kuuchukua mwili.

  Roma alidai kuwa walalamikaji walitaka kuisafirisha maiti hiyo kuelekea Ifakara na kuizika Kikristo.

  Aliiomba mahakama kumpatia Kundra kibali cha kuichukua maiti hiyo na kuizika Kiislamu.
  Kwa upande wa wakili wa wototo wake wengine, Steven Tonya, alidai alikiri kuwa Kundra alikuwa anaishi na marehemu na ndugu walimtambua.

  Hata hivyo alidia kuwa jina la Salumu Ngindo halitambuliki hata kwa watoto wake.

  Alidai kuwa cheti cha ndoa walichopatiwa kina utata kwani kinadai kuwa marehemu alifunga ndoa hiyo akiwa na umri wa miaka 38, jambo ambalo limewapa mashaka.

  Alidai kuwa ndoa hiyo inaonyesha kuwa ilifungiwa Mkoa wa Mara katika Wilaya ya Bunda lakini aliyeifungiasha hayupo kwenye orodha ya watu wanaotakiwa kutoa huduma hiyo.

  Tonya alidai kuwa mlalamikaji anatakiwa kutoa ushahidi wa kina kuhusiana na cheti hicho kwani bado familia haitambui kama marehemu alikuwa amebadilisha dini.

  Tonya aliieleza mahakama kuwa watoto wanawajibu wa kuzika wazazi wao kwa mujibu wa utamaduni bila kuangalia dini.

  Aliiomba mahakama kutoa kibali cha kuwaruhusu wanandugu hao kuisafirisha maiti hiyo kwa ajili ya mazishi na sio vinginevyo.

  Hakimu Kibona aliamua kuiahirisha kesi hiyo ya mpaka leo ambapo atatoa hukumu.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Amezikwa kiislam
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 11,007
  Likes Received: 3,271
  Trophy Points: 280
  Yesu alimwambia mtu mwingine, ``Nifuate.'' Mtu huyo akamjibu, ``Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.'' Yesu akamwambia, ``Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautangaze Ufalme wa Mungu.''
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Kuna cha kujifunza hapa. Jamani kuepuka adha hii, ni vizuri tukajenga utamaduni wa kuandika wosia na kutoa maelekezo kuhusu mali ulizoacha na kuweka bayana uzikwe sehemu gani!!!

  Hawa ndugu na mke wake ni kama wanamuua mara mbili marehemu sasa!!!

  Tiba
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...