Familia ambazo Baba na Mtoto wameshika Nafasi ya Urais

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,960
4,209
Ifuatayo ni orodha ya familia ambazo Baba na mtoto walifanikiwa/wamefanikiwa kushika nafasi ya Urais.

Lengo la uzi huu ni kuelimisha tu juu ya familia ambazo wanafamilia walishika nafasi za juu katika nchi.

1. Baba John Adams (1797 - 1781) Mtoto John Quincy Adam (1825 - 1829). Nchini Marekani

2. Baba Laurent Desire Kabila (1997 - 2001), Mtoto Joseph Kabila (2001- 2019). Nchini DRC

3. Baba Jomo Kenyatta - Mtoto Uhuru Kenyatta. Nchini Kenya

4. Baba George Bush (1989 - 1992) Mtoto George W Bush ( 2001 - 2009). Nchini Marekani

5. Baba Gnassingbé Eyadema (1967 - 2005) Mtoto Faure Gnassingbé (2005 - mpaka leo) . Nchini Togo

6. Baba Abeid Aman Karume - Mtoto Aman Abeid Karume. Nchini Zanzibar

7. Baba Sir Seretse Goitsebeng Maphiri Khama rais wa kwanza - Mtoto Ian Khama rais wa nne. Nchini Botswana

8. Baba Pierre Trudeau - Mtoto Justin Trudeau - Waziri mkuu wa Canada( cheo cha juu nchini Canada)

9. Baba Rais Park Chung-hee - Mtoto (mwanamke) Pak Geu-hye. Nchini Korea Kusini.

10. Baba Omar Bongo (1967 - 2009) - Mtoto Ali Bongo Ondimba ( 2009 - ). Nchini Gabon.

11. Baba Edward Akufo-Addo (Rais wa pili) - Mtoto Nana Addo Dankwah Akufo-Addo. Nchini Ghana.

Tutaendelea na orodha maana kuna kina Mahatma Ghandhi na Indira Ghandhi hapo.

Malawi wao ni tofauti maana ni kaka amemuachia kaka Rais Peter Mutharika alichukua nafasi ya kaka yake Bingu Mutharika.
 
Vipi kuhusu Kamuzu Banda na mwanawe Joyce Banda?
Joyce Hilda Ntila Banda aliyezaliwa mwaka 1950 katika kijiji cha Malemia, wilaya ya Zomba the Zomba nchini Malawi.
Baba yake alikuwa afisa Polisi hana mahusiano yoyote na Kamuzu Banda.

Joyce Banda(Kama alivyozoeleka) aliyepata kuwa makamu wa Rais chini ya Bingu -wa- Mutharika.
Alikuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Malawi kutoka April 2012 - May 2014 na Rais wa pili mwanamke barani Afrika.
 
Back
Top Bottom