mwekundu
JF-Expert Member
- Mar 4, 2013
- 21,859
- 19,738
Naona na kuna kila dalili na ishara kuwa mh el kapania kuutwaa urais 2015,mchakato ambao anatakiwa kujiandaa kwenye chama chake(kama anavyofanya sasa) na baadae akipewa turufu hiyo asimame kama mgombea urais kwa tiketi ya ccm.
Kinachonishangaza na kuniogopesha katika mchakato huu ni staili yake ya kumwaga fedha nyingi sana katika harakati zake hizi,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa,sote tumeshuhudia nguvu yake katika kupandikiza makada wake katika kila level ya uongozi katika chama chake hiko ccm tena kwa nguvu nyingi sana(fedha) ili mradi tu ajisafishie njia ya kuchaguliwa ndani ya NEC kuwakilisha chama,hadi hapa karibuni iliripotiwa kuwa anawakusanya makatibu wakuu na wakuu wa wilaya Tanzania nzima kwa gharama zake mwenyewe na hatimae kufanya ajenda zake ili atimize malengo yake.nina uhakika katika historia ya Tanzania hamna mtu au Raisi ambaye ametumia nguvu na gharama nyingi za kutaka kuukwaa uraisi kama anavyofanya muheshimiwa huyu,hivo basi kwa watafsiri makini lazima watilie mashaka ambition ya uraisi ya muheshimiwa huyu na anaweza akawa ni mmoja ya watu katika taifa hili ambao wameingia kwenye record mbaya ya kukosa weledi(degree of intergrity)-kama rekodi zinavoonyesha ni mtu ambaye ana tuhuma kadhaa za ubadhilifu wa fedha-tuhuma kama Richmond haiwezi kutufanya watu tumsahau,na ni matarajio yetu kuwa Mh EL kwa tuhuma kama zile zingemfanya astaafu kabisa mambo ya siasa na asiwe na hata hamu ya kugombea nafasi yoyote ile...cha ajabu ndo kwanza anazidisha mashambulizi ya kutaka ngazi ya juu kabisa ya uongozi,huu ni ukosefu wa aibu na uzalendo
Sasa swali linakuja "Je hivi fedha kazipata wapi?fedha nyingi kama hizi sio ushahidi tosha wa tuhuma zinazomkabili?-hayo ni maswali ambayo ni baadhi tu naweza jiuliza mimi mkulima
Mwanafalsafa Mwl.Nyerere alishawahi kusema kuwa "Mtu anayetumia Fedha nyingi kuingia ikulu ni wakuogopwa zaidi ya ukoma,yafaa watu wajiulize hizi fedha kazitoa wapi?kazipata Vipi? na atazirudishaje?alikozitoa?kwani ikulu sio sehemu ya biashara,kuna biashara gani kule?ikulu ni mzigo-akaongeza na kutoa experience kuwa yeye ndo Rais aliyewahi na hamna kwa mujibu wa democrasia atakaa miaka mingi ikulu!!
Swali lingine la kimapana zaidi ni kweli ccm wameshasahau falsafa za mwanzilishi wetu huyu?hadi baadhi ya viongozi ndani ya chama wabariki harakati hizi ambazo kwa hata falsafa tu za Mwl. J K Nyerere zinamwangamiza na kukosa sifa hata moja ya kuwa Raisi?
Karibuni wanajamvi mtiririke.......
ent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums