Falsafa za Adoph Hilter zinapendwa kutumiwa na viongozi wa Afrika kubaki madarakani

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,595
8,729
Kuna wimbi kubwa wengi tunapenda kuokota bila kufatilia kiundani sana.

Kama utakuwa umebahatika kujua na kusoma vizuri utawala adolph hilter basi utaona kuna chechembe nyingi aina ya viongozi wengi wakitumia ili kubaki, kukubalika na hata kutenganisha watu.

Sio mgeni ndani ya nchi yetu na nchi nyengine tumeona kabisa viongozi wengi wakiweka kinga hizo ili watu wafumbwe macho kujua ndio mtawala mzuri.

Viongozi hawa wanaweza kutenganisha nchi, ukabira,dini, matukio na mbinu zozote ili mradi tu waendelea kuungwa mkono kwa mbinu zozote.

Leo nikamkumbuka bwana Yahya Jammeh. Huyu jamaa ukiangalia mambo aliyofanya mpaka kudai kutibu ukimwi kwa kisingizio cha imani.

Nika mkumbuka Marehemu Mugabe. Baada ya kuona kunaelekea kubaya kwenye madaraka akaanza kufukuza wazungu ili kuungwa mkono.

Nika mkumbuka awamu ya tano. Alivotutenganisha maskini na matajiri akijua maskini tupo wengi tokea ccm kuingia madarakani.

Hawa ni wachache ambao nikijaza itakuwa nawachosha.

Falsafa za viongozi wengi wanaposhindwa
 
Adolph alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa la Ujerumani. Extra- nationalist. Leo Ni mfanowe Vladmir Putin. Kwa Adolph mikataba ya kinyang'au ya Verssaile ilikuwa Ni kidonda kikuu moyoni. Kwa maono yake, Ujerumani ya taswirani isingetimia.

Adolph alitaka Ujerumani yenye nguvu kijeshi, kijamii , kiutamaduni na kiuchumi . IIi kutimiza Hili lengo la moyoni akaanza kuua, kuteka na kuharibu kila kilichokuwa dhidi ya Ujenzi wa Great German.

Kwa namna hii ya kutisha Ujerumani ikaanza kuwa tishio si tu kwa Paris na London, Bali ikawa Hitler Ni kitisho Hadi Moscow, Warsaw na Newyork.

Wabishi wakamshughulikia na akapoa i'la Ni kwa gharama kubwa ya dam.
 
Back
Top Bottom