Falsafa za Adolf Hitler na siasa za Tanzania


M

Meddah Sotta

Member
Joined
Oct 31, 2013
Messages
5
Likes
0
Points
0
M

Meddah Sotta

Member
Joined Oct 31, 2013
5 0 0
Siku zote madaraka ujenga tamaa kubwa, hasa yale madaraka yenye kupitia wakati wa mapambano yenye hisia ya kufikia 'Nchi ya Ahadi'. Waingereza husema,"Power corrupts, but absolute power corrupts absolutely". Kishawishi kikubwa anachopata kiongozi katika kipindi hicho ni kuona kwamba kaishapambana vyakutosha na labda anaweza kupata ushindi.
Viongozi wengi wamekuwa wagumu sana kuachia ngazi katika kipindi hiki, kwa kuhisi kama watakuwa walipigana bure ili kuwapa ushindi watu wengine au kwa kuhisi hawatofutwa jasho kama ushindi utapatikana mikononi mwa watu wengi au labda wakiwaachia wengine watasaliti na kuacha harakati zao au kwa ulafi na uroho wa madaraka.
Tamaa na kishawishi hiko cha madaraka, kama vilivyo vishawishi vya mali n.k. humpelekea kiongozi kutamani kufikia 'Nchi ya Ahadi' akiwa na watu wachache hasa wale ambao hawawezi kumletea 'kauzibe' na watakao sema ndio kwa kila atakachoagiza bila kuhoji, na kwa jinsi hiyo uanza kupambana na kuhakikisha anawaondoa wale wote walio maarufu kumshinda, wanaompinga au kuonyesha ushindani, na hata kudharau na kupuuza mchango wa baadhi ya watu ambao kwa hoja, ushawishi na majitoleo yao wamemfanya ndoto ya kufika nchi ya Ahadi ianze kuaminika.
Hii inafanana na ile hadithi ya kufikirika, ambapo watu wa jamii moja walipigana kwa pamoja kwa muda mrefu wakiilinda dhahabu iliyo katika sehemu moja ya nchi yao, kutokana na umoja wao waliweza kupata ushindi mkubwa sana! Baada ya muda, kwa kuamini adui hana nguvu tena watu wa sehemu ile yenye dhahabu walishawishiana na kuamua kuidai ile sehemu na kujitenga na jamii yao, wakiamini kwamba watafaidi na kunufaika zaidi wakiwa peke yao hata kudharau umoja wao ambao ndio hasa ulipelekea ushindi wao. Iliwachukua mwezi mmoja tu kumiliki sehemu ile, na baada ya hapo walikuja kuporwa sehemu ile na watu wenye nguvu waliowashinda mwanzo kwasababu ya umoja wao.
Hadithi hiyo ya kufikirika ni funzo na mfano tosha wa sura ya siasa ya Tanzania. Viongozi wa vyama vya siasa, wamekuwa wakigeuka walevi wa madaraka na 'madikteta' hasa pale wanapoona kwamba chama kimesha ushawishi umma vyakutosha na wameshamshinda adui yao, hata kudharau nguvu ya umoja wao ambao ndio hasa uliwafikisha hapo walipo, huhakikisha wanawaondoa na kuwachafua wale wote wanaonekana kuwapinga, kukubalika zaidi yao na kuonyesha ushindani, ili kubaki tu na wale watu watakaokubaliana nao bila kuhoji kwa kila wanachokisema.
Katika kipindi hiko ili kujilinda, kujiimalisha, kuhakikisha wanaogopwa na azaliwi mwingine atakayehoji wala kuuliza matendo na mawazo yao, wanaanzisha utawala wenye falsafa za mabavu, wenye 'slogan' nyingi, na kukihamisha chama na wafuasi wake kutoka kuwaza kwa mantiki kwenda kwenye kuwaza kwa kutumia hisia. Hoja zao uhama kutoka kwenye misingi ya umoja kwa utetezi na kupigana na matatizo wanayopata watu hasa wa tabaka la chini, na adui mkubwa ugeuka Chama Tawala, na matatizo yoyote yanayokikumba chama, shutma na hoja zozote nzito dhidi yao, hata kama zimesababishwa na wao wenyewe na hata kama zikiwa nzito kiasi gani uwa na jibu moja tu, nalo ni yanaletwa, yanatengenezwa au wanaohoji wametumwa au wanatumiwa na Chama Tawala, kana kwamba bila Chama Tawala basi chama chao kisingikuwa na shida yoyote ile.
Viongozi wa vyama vyetu wanakosa sana uwezo wa kujipima, kujitathimini na kupima ukweli wa mawazo na sifa wanazomwagiwa kutoka kwa wafuasi, washauri na viongozi wenzao. Kiongozi mahili ni yule mwenye mbinu za kupima kama anaambiwa ukweli kama mfano wa Mfalme Mmoja Mwanafalsafa, aliyeongoza Empire moja huko Ulaya na kushangaa katika miaka Ishirini na Mitano aliyoongoza Empire ile hajawahi kupingwa wala kuhojiwa kwa maamuzi yake au jambo lolote lile. Kwa kutambua hilo aliamua kupima uaminifu na ukweli wa washauri, wafuasi na wananchi wake. Aliitangazia Empire yake kwamba, siku itakayofuata atavaa vazi zuri na la thamani kubwa na kutembea nalo kila eneo la Empire yake, na alimtaka kila Mwananchi wa Empire yake aandike tenzi na mashairi ya kusifia vazi lake, na atakaye andika kiasi cha kumfurahisha basi angempa nusu ya mali zake.
Siku ile ilipofika, Mfalme alivua mawazi yake yote na kuzunguka nchi ile hakiwa kama alivyozaliwa, lakini chakushangaza kila alikopita katika Empire yake alishangiliwa na kusifiwa kwamba amependeza sana na hata baadhi ya washauri wake wakadiriki kusema hakuna siku aliyopendeza kama ile. Na hata baada ya kurudi kwenye makao yake na kuanza kusoma Tenzi na Mashairi toka kwa wananchi wake, akiwemo mke wake, wote waliandika kusifia na kulitukuza lile vazi kadri ya uwezo wao na ni Mwananchi mmoja tu maskini aliyeandika ukweli juu ya vazi la mfalme kwa kuandika, "Mfalme yuko Uchi". Na mfalme huyo Mwanafalsafa kwa kugundua unafiki, uoga na uongo wa watu anaowaongoza aliamua kumrithisha Mwananchi yule Maskini ufalme wake.
Tofauti na Mfalme huyo Mwanafalsafa viongozi wetu wa siasa uwachukia sana na kuwafanyia kila aina ya mizengwe watu wanaotofautiana nao mawazo na kuwaambia ukweli chamani, na uwapenda sana wale watu waoga, wenye kuwasifia na kuunga mkono bila kuhoji kila wanalosema na kutenda. Na kwa jinsi hiyo ugeuka 'MADIKTETA' na hutumia mbinu za "kinazi" zile zile alizotumia ADOLF HITLER miaka ya 1900s.
Adolf Hitler aliamini na kusema, "I use emotion for the many and reserve reason for the few" akimaanisha, "Natumia hisia kwa wengi na kuhifadhi mantiki kwa wachache". Wanasiasa wetu leo wanatulazimisha tuwaze kihisia na kuamini kwamba kila anaye tofautiana nao mawazo au kudai mabadiliko au kuhoji basi ni msaliti, na anatumiwa kana kwamba viongozi ndio chama chenyewe na ukiwapinga wao basi unakipinga chama.
Pia Adolf Hitler huyo huyo alipata kusema,"Kama ukisema uongo mkubwa na ukiendelea kuusema mara nyingi vyakutosha, Utaaminika" na kwamba, "Umati mkubwa wa watu ni rahisi zaidi kuudanganya kuliko umati mdogo" zaidi "Kwa kutumia propaganda kwa ufundi, mtu anaweza kufanya watu wakaona hata mbinguni ni motoni na motoni ni mbinguni" na kwahiyo mwisho wa siku "Sio ukweli ulio na maana, bali ushindi".
Wanasiasa wetu wameonyesha kila mara kutumia mbinu na kila aina ya uongo na mihemko ya hisia za wingi kuficha ukweli na kuwachafua wanao waambia ukweli ili mradi tu waaminike na kupata ushindi. Uwapa majina ya WAHAINI wale wanaodai MABADILIKO, nasema, hakuna Uhaini wowote duniani unaozaliwa kwa mtu au kikundi cha watu kudai au kuhitaji MABADILIKO, tena kwa njia ya ushawishi wa kura, Uhaini wa aina yoyote ile ni zao la mpango wa MAPINDUZI, mpango wa MAPINDUZI, na sio mpango wa MABADILIKO.
Hitler aliamini, "The great strength of the totalitarian state is that it forces those who fear it to imitate it", akimaanisha, "Nguvu kubwa ya utawala wa mabavu ni kwamba, unawalazimisha wale wanaouogopa kuufata".
Vyama vyetu vya siasa vimegeuzwa na viongozi kuwa sehemu ya kuogopwa na sehemu marufuku kutoa wala kuhoji mawazo ya viongozi. Na kwa jinsi hiyo kama ilivyokuwa katika enzi za Hitler, mfumo wa siasa zetu uwa lazimisha waoga, mashabiki na wafata mkumbo, ambao ndio wengi kwenye vyama vyetu, KUUFUATA!
Kwa Mtazamo wangu SIASA hizi mpya za KIDEKTETA zinazoanza kuibuka na kushamiri nchini ni Tabaka Jipya Kandamizi kwa watu wetu, na ni lazima tuzipinge kwa nguvu zetu zote! Na kama zikiachiwa ziendelee na zikue, siku za usoni ndio zitakuwa hasa siasa za nchi yetu, na kama vyama vya jinsi hii VIKIENDELEA kuiongoza Tanzania au KUCHUKUA dola ya Tanzania, mana VYAMA uzaa serikali, kama ilivyo, kwa MTOTO wa NYOKA nae ni NYOKA, basi ni wazi chama chenye mitazamo ya KIDIKTETA, kitazaa serikali ya KIDIKTETA pia.
Ni kujidanganya kupita kiasi, kuamiani kwamba chama ambacho viongozi wake wanaweza kudiriki kufuta Ukomo wa Uongozi kwenye Katiba ya Chama, na kuwageukia wanaohoji hilo wakidai kuwa ni Wasaliti na Wahaini eti kesho wanaweza wakaiongoza Tanzania na kuwaacha SALAMA watu watakaokuwa na mitazamo tofauti na wao.
 

Forum statistics

Threads 1,250,757
Members 481,468
Posts 29,743,911