Falsafa Yetu

George Kahangwa

JF-Expert Member
Oct 18, 2007
547
147
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,
Mahali fulani katika jukwaa hili suala la falsafa limehojiwa. hojaji hiyo imeambatana na madai ya kwamba taasisi zetu za kisiasa(vyama) havina misingi ya kifalsafa. Lakini msingi huo wa kifalsafa hauwezi kujengwa hewani bali katika jamii lengwa ya vyama husika. Kwa mantiki hiyo falsafa bora ya chama haina budi kutokana na falsafa inayoheshimika na kutumika katika jamii. Siasa zipo ili kuifanya jamii ibaki katika msitari sahihi wa kuifuata na kuiheshimu falsafa hiyo na kuifanya iwe na manufaa zaidi.
Naomba nibainishe kwamba,falsafa ya jamii yetu (watanzania) iliyo na mizizi katika mila na tamaduni zetu za enzi na enzi ni;

UTU
(Nafarijika kulisema hili katika siku/tarehe yangu muhimu sana ya 39)
 
Naomba tunapoendelea kulitafakari hilo nililodokeza tujiulize maswali haya;
1.Falsafa ni nini?
2.Mtu ni nini?
3.Utu ni nini?

Kuweni huru kuweka majibu yenu, wakati huo huo najiandaa kuleta uchanganuzi yakinifu wa falsafa ya UTU.
 
katika kutafakari maana ya falsafa, fikiria juu ya maneno haya;
1.hekima
2.mantiki
3.maadili
4.uzuri
5.maarifa
6.kanuni
 
Na katika kutafakari mtu nini,tujiulize hivi;
1.Je,mtu ni mnyama tu au anacho kinachomtofautisha na wanyama?
2.Mtu ni kuwa na umiliki wa vitu/mali basi?
3.Au mtu ni utu?
 
mimi masikio yote nimetega,naamini kwa vidokezo hivi kuna kitu kikali unataka kupakua, fanya hima tafadhali
 
Na katika kutafakari mtu nini,tujiulize hivi;
1.Je,mtu ni mnyama tu au anacho kinachomtofautisha na wanyama?
2.Mtu ni kuwa na umiliki wa vitu/mali basi?
3.Au mtu ni utu?
kibaolojia mtu ni mnyama, wenywewe wanasema yuko katika kingdom ya animalia. Tofauti yake na wanayama wenzake ni upeo wa kiakili unaomuwezesha kuunda zana (man is a tool maker) lakini anacho kingine...LUGHA.
Nadhani sijakosea mkuu.
 
Zamani uliweza kusema "Watanzania" ukamaanisha kitu kimoja.Tulikuwa wamoja, watu wa chama kimoja kinachoamini itikadi moja na tena hakukuwa na matabaka ya kuonekana, tofauti ya mijini na vijijini haikuwa ya kutisha, tyulielewana.

Siku hizi ukisema "Watanzania" unakuwa unaongelea fumbo kama alilolisema Mfalme Selassie na kutoholewa na mwanamuziki Bob Marley katika wimbo wake wa "War", kwamba neno hili, jina hili "Watanzania" linakuwa ni mauzauza ya kutafutwa lakini yasiyopatikanika.Utanzania, na zaidi ya hapo, utanzania wa sare hii unaousema wewe, kwamba tukawa na falsafa moja wote ni dhana ya kizamani, kijamaa na iliyopitwa na wakati.

leo hii "Watanzania" hawawezi kuwa na falsafa moja, kwa sababu wakati wengine wanakufa kwa njaa na kwa kukosa vidonge ya shilingi elfu hamsini, wengine wana mamilioni ya pesa, siyo katika hela za kitanzania au shilingi ya madafu kama wanavyoiita watoto wa mjini, bali katika dala za kimarekani.

Kweli unaweza kusema hawa watu wamoja hawa? Unaweza kusema wana falsafa moja hawa? Au ndiyo tunakuwa na Utanzania wa kidini, kwamba mimi mkristo au muislam kwa sababu familia yangu ni wakristo ama waislam na labda kwa sababu siku moja moja kama za Krismas au Pasaka -Idi kwa waislam- nakwenda kanisani/msikitini.

Mimi siamini kama kuna falsafa ya kitanzania, kwa sababu falsafa ya kitanzania ni muungano wa falsafa za makabila ya watanzania, na katika effort za kuujenga utanzania tumebomoa/ tunabomoa ukabila kabisa kwa kasi kubwa sana, kitu ambacho ni kizuri kwa upande mmoja kwa sababu hatupati sana matatizo ya vita vya kikabila kama jirani zetu, lakini kwa upande mwingine kuvunja ukabila huku katika jitihada za kuukumbatia utanzania ndiko kunakotusababishia tusahau core values za utanzania, tunataka kujenga nyumba lakini tunatupa matofali yatakayojengea nyumba kwa sababu matofali yatagawanya nyumba na kuleta nyufa, mwishowe nyumba inakuwa haina unit blocks na inaanza kupata nyufa kubwa sana.

Kwa hiyo kupata national values back in the sense described here, inabidi tupate tribal values back na tuwe makini kufanya hivyo bila kuleta tribalism.Only the positives, with the right goals.

Other than that ndiyo tutaendelea kuikumbatia hii classic society na ufisadi itakuwa ni kitu kila mtu atakuwa ana aspire.Na hii habari ya falsafa ya kitaifa itakuwa ni ndoto na propaganda.

Personally I believe this is already a genie outside the bottle.
 
Pundit,
Ahsante sana kwa mchango wako.Ninaanini katika nilichokisema kwamba tuna falsafa yetu watanzania, na wala hilo si wazo la kizamani bali ni la tafakuri yakinifu.
Aidha, naomba ufanye kutofautisha maneno haya mawili falsafa na itikadi. Kudhania kwamba yana maana moja ndio mwanzo wa hoja ya kudai kuwa hatuna falsafa moja/isitahiliyo kuitwa ya kitanzania.
Katika mchango wako 'nimepigia mstari' neno moja zuri sana;VALUES. values are related to ethics(which is one of the branches of philosophy) huwezi kuwa na ethics bila UTU
 
Utangulizi
Mojawapo ya mambo yanayomtofautisha mwanadamu/mtu na wanyama wengine au viumbe wengine ni uwezo wake wa kufikiri, kutenda kwa hekima na busara na kufanya ayafanyayo kwa kanuni za kipekee. Hekima hiyo na kanuni hizo humwongoza mtu katika maisha yake binafsi ya kila siku na katika uhusiano wake na wanadamu/watu wenzake, kadhalika hata katika mahusiano yake na viumbe vyote vilivyoko katika mazingira yake.
Ni hekima na kanuni hizo ambazo huitwa falsafa ya mtu. Lakini mtu hawezi kuwa na falsafa na akaitumia bila kujitambua yeye ni nani na yupo kwa sababu gani. Katika mantiki hiyo viwango vya kujitambua miongoni mwa watu ni tofauti. Tofauti hizo zinaweza kuwa kwa sababu ya umri, kwa sababu ya uamuzi na mtazamo au kwa sababu ya uelewa. Hata hivyo inatarajika kwamba watu wote waufikie upeo wa juu wa utambuzi ili falsafa ya mtu mmoja mmoja na watu wote kwa pamoja iwe ya kiwango cha juu kabisa tena yenye kukubalika.
Makala hii inajikita katika kubainisha na kueleza falsafa inayojidhihiri katika maisha ya kila siku ya mtu na watu itokanayo na kujitambua kwake/kwao. Makala inarejea kidogo katika maana ya falsafa, inaonesha kile ambacho jamii za watu hususan watanzania na hata Afrika kwa ujumla wanakiamini kama ndiyo hekima na kanuni sahihi ya maisha ya mtu mmoja mmoja na ya jamiii kwa ujumla. Makala inarejea pia mifano kadhaaa katika tamaduni za wanajamii zainazoashiria falsafa inayowaongoza. Pia makala inaangalia jinsi falsafa hii ya watu inavyotafsiriwa na kufuatwa au kutofuatwa katika masuala ya uongozi wa jamii, na utawala wa kisheria. Aidha inatazama mahusiano ya falsafa na itikadi za kisiasa, na mwisho wa makala ni majumuisho.

maana ya Falsafa
Ili tuweze kuchanganua vizuri hekima na kanuni hizo, hapana budi kwanza tukiangalia ainisho la neno falsafa. Hili neno, tafsiri yake ni pana sana kiasi kwamba ni vigumu kuifungamanisha katika maana moja. Hata hivyo linaweza kutafakariwa kwa kuangalia katiaka chimbuko na matumizi yake ya awali (etymologically) linamaanisha nini. Vile vile linaweza kuangaliwa kwa tafsiri ya kile kinachoitwa matawi yake yanayoyatajwa na waichukuliao falsafa kuwa somo (discipline). Kadhalika mtazamo wa falsafa kuwa ni mwongozo wa maisha unastahili kuzingatiwa.
Falsafa ni msamiati uliotoholewa kutoka neno la Kigiriki - philosophos ambalo ni muunganiko wa maneno mawili; philein (kupenda) na Sophia (busara), kwa maana hiyo falsafa ni kupenda busara au kuwa na busara. Katika mantiki hiyo hiyo, kuwa na busara ni sawa na kuwa na uwezo wa kutambua kwa usahihi jambo au kitu kilicho cha thamani na kisha kuwa na uwezo wa kutenda matendo yathibitishayo utambuzi huo. Kwa maneno mengine falsafa/ busara ni uwezo wa kupambanua jema na lisilo, lifaalo na lisilofaa au kilicho kizuri na kilicho kibaya.
Katika tafsiri ya falsafa kama somo lenye matawi, kuna matawi ya aksiolojia (amali na maadili), epistemolojia (maarifa), mantiki(logic) na metafizikia (zaidi ya vitu halisi). Hivyo falsafa ni maadili, maarifa, mantiki na mtazamo ulio zaidi ya kuviangalia vitu halisi vinavyoonekana.
Ni kwa sababu hiyo, falsafa hujishughulisha na mambo yanayothaminiwa katika jamii na yanayochukuliwa kuwa ni tabia adilifu au matendo ya kimaadili. Aidha kwa kuwa falsafa ni maarifa hujishughulisha na utambuzi wa ukweli, uwepo wa vitu na watu, uhalisia, sababu za matukio na uhuru wa kweli
Falsafa kama mantiki inahusika na utambuzi na utendaji wa mambo kwa mantiki sahihi. Vile vile falsafa ni uelewa wa kibusara kwamba maisha ni zaidi ya ulimwengu wa vitu na mali.

Busara, maadili, maarifa na mantiki na mitazamo humuundia mtu seti ya kanuni, malengo na imani zinazomongoza katika ayafanyayo/ ayatendayo. Na hii ndio tafsiri ya falsafa kama mwongozo wa maisha ya mtu. Falsafa ya mtu vile vile, ni busara ya kitabia na fikira kuntu.
makala itaendelea...
 
mimi nadhani kati ya mambo tunayoyathamini(values) watanzania ni HEKIMA, UMOJA,UHURU na AMANI, rejea wimbo wa Taifa.
 
UTU: Hekima na Kanuni Sahihi ya Maisha
Kwa kuwa mtu si mnyama tu kama walivyo wanyama wengine, kila siku ya uhai wake anafaya shughuli mbali mbali katika namna ambayo ni ya kiutu. Mtu hatarajiwi kufanya kazi kwa ajili ya kujidhuru yeye mwenyewe. Ni pale tu utu wa kawaida unapomtoka anapoweza kuamua kuidhuru nafsi yake, au pale maarifa aliyonayo yanapokuwa ni finyu kiasi kwamba hatambui kuwa anachokifanya kitamletea madhara. Kadhalika mtu hatarajiwi kwamba katika shughuli zake kwa maksudi atafanya mambo yaliyo na madhara kwa watu wenzake. Kwa sababu ni mtu mwenye utu atafanya shughuli katika namna ya kiutu na kuwatendea wenzake mambo ya kiutu. Kinyume chake ni vitendo vya kinyama, kikatili, kibinafsi, kidhuluma na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Vile vile shughuli za kiutu za mtu ziko katika namna ambayo si ya madhara kwa viumbe wengine na chochote kilichomo katika mazingira. Mtu mwenye utu, hachukulii udhuru wa mahitaji yake yatokanayo na mazingira kumfanya awe mharibifu wa kila kilichomo katika mazingira yake, bali mahitaji ya kiutu hutoshelezwa kwa namna ya kistaaarabu. Hayawani wasio na utu, hawashangazi wanapokuwa wakatili katika harakati zao za kujitafutia mahitaji na wala hawatambui kama wanafanya ukatili. Chukulia mfano wa chui katika mbuga za Serengeti na kwingine, jinsi maisha yake yanavyoongozwa na sirika ya kuua takribani kila mnyama mnyonge anayekatiza mbele yake hata kama tayari amekwisha kupata kimtoshacho kwa ajili ya siku. Ataendelea kuua tu hata asivyovihitaji, na huo ndio uhayawani halisi.
Mtu mmoja mmoja mwenye utu ndiye hatimaye huunda jamii yenye utu. Utu katika jamii inayoundwa na watu wenye utu hujidhihiri katika mahusiano baina yao, katika shughuli zao za uzalishaji mali/ shughuli za kiuchumi, imani zao, mipangilio yao ya kisiasa na hata katika utamaduni wao wa siku hadi siku kwa ujumla wake.
Katika jamii yenye utu zipo amali za jamii za kiutu na yapo maadili ya kiutu ambayo yanaheshimika, yanazingatiwa na kuenziwa miongoni mwa watu na taasisi zao. Hii ni jamii ambayo heshima ya kila mmoja ni ya kipekee,wema unashamiri miongoni mwa watu, kujali na kutunza ni sifa ya kila mmoja, ukarimu na upendo haviwapigi chenga, kutakiana heri hakuko katika maneno tu bali hata katika vitendo. Ni jamii ambayo matendo ya udanganyifu, rushwa dhuluma, utapeli, uonevu, udhalilishaji na maovu mengine ya aina hii inayawekea alama ya ukengeufu wa utu na kuyatungia sheria na kanuni za kuyadhibiti.
Katika siasa za jamii hii, uongozi unachululiwa kuwa ni alama ya mfano wa uadilifu na utu uliotukuka. Uongozi unakuwepo ili kuzidi kuiekeza jamii katika kiwango kikubwa zaidi cha utu na kuwezesha kuurithishwa utu huo toka kizazi hata kizazi. Wanasiasa na wote wanaopewa dhamana ya kuongoza, jamii inawatarajia katika kauli zao mbele ya watu, katika utekelezaji wa majukumu yao, na katika maisha yao binafsi wawe vinara wa utu. Hawatarajiwi viongozi hawa kuwa upande wa dhuluma za kiwango na aina yoyote ile, bali wazingativu wa sheria na kanuni za utu.
Ni bahati mbaya kwamba kwa sababu ya baadhi ya wanajamii na baadhi ya viongozi kutokuwa na utashi wa kutambua na kutenda utu, dunia imekuwa pahala pa unyama, kudhuriana na kudhulumiana. Utu kamwe hauwezi kukubaliana na utaratibu wa maisha unaoongozwa na dhana ya mwenye nguvu mpishe/mwenye nguvu ndiye anaishi (survival of the fittest). Utu hauwezi kuendana na ubepari ambao umesheheni ushindani umnufaishao anayenyakua fursa ilihali jirani yake akidhulumika stahili yake. Utu hauwezi kukumbatia kumgeuza mtu aliyezaliwa na mwanamke (heshima mbele), kuwa mtumwa. Utu hauwezi kuendana na kanuni za kiuchumi zinazokuza uchumi wa watu wachache na kuwaacha wengi wakiwa hohehahe. Utu hauwezi kuvumilia kuona mchanganyiko wa wakwasi na mafukara katika jamii moja. Palipo na utu hapana migogoro na migongano.
Leo hii katika ulimwengu, tunapoendelea kushuhudia machafuko, vita na mauaji ya mtu mmoja mmoja na ya kimbali, ugaidi, uvamizi, ukaliaji wa kimabavu wa nchi moja dhidi ya nyingine, utengenezaji wa silaha za maangamizi, nyukilia, za kibaiolojia na nyinginezo, tatizo linadhihirka kuwa moja tu, mtu kakengeuka kutoka kwenye utu wake.
Leo hii mataifa yanapoendelea kushuhudia ongezeko la ufisadi, rushwa nene, ubadhilifu na uchafu mwingine miongoni mwa viongozi, watumishi wa umma na wetendaji katika sekta mbalimbali, kinachogomba hapo ni tatizo moja kuu; wamepoteza utu. Fisadi (weka jina la fisadi yoyote hapa) hana utu, vinginevyo asingeyafungamanisha maisha yake na kuiridhisha nafsi yake kwa gharama ya kuwadhulumu wengine; asingeweza kujilimbikizia fedha na mali asizozihitaji kana kwamba yeye ni hayawani wa porini.
Leo hii jamii inapoendelea kushuhudia matendo ya kishirikina, udhalilishaji wa akina mama na watoto, ni dhihirisho jingine la kuondokewa na utu kunakowapata wahusika wa matendo hayo machafu. Ni ajabu kwamba hata wanyama na uayawani wao hawafanyi haya watu wasio na utu wanayoyafanya.
Leo hii tunapoendelea kulia na ongezeko la joto duniani, uharibifu wa mazingira na kadhalika, tatizo ni kwamba mtu kaacha au kapunguza uhusiano wake wa kiutu na mazingira yake. Mtu mwenye utu si mtumiaji wa rasilimali kana kwamba hakuna kesho, ufujaji wa aina yoyote ile si utu. Mtu mwenye utu hawezi kuthubutu kuanzisha moto wa pori ili uteketeze mbuga, misitu, viumbe anuai, na vyazo vya maji. Mtu mwenye utu hawezi kudiriki kuachia tak zenye sumu ziiharibu ardhi, ziyachafue maji na hewa chafu iendelee kuzalishwa kwa wingi toka viwandani. Kukosekana kwa utu kunamfanya mtu asione mbele na wala asitambue uhusianao wa uhai wake na uhai wa viumbe wengine. (balance of the eco system, and biodiversity)
Mtu mwenye utu hawezi kufanya vitendo vya kimaendeleo bila kuzingatia manufaa yake kiutu. Maendeleo ya viwanda na technolojia, kama ni ya madhara kwa watu, basi hayo si maendeleo ya kiutu bali matumizi ya kiayawani ya karama ya maarifa. Ugunduzi wa technolojia sio ukamilifu wa mambo bali ukamilifu wake ni uboreshaji wa utu wa mtu.
Kwa ujumla katika jamii ya watu wenye utu kuna utambuzi kwamba maisha sio tu kuwa na chakula, mavazi, nyumba magari na mali nyinginezo (material wealth) bali utu ni zaidi ya kuwa na mali maana maisha si ya mwilini tu, maisha yako katika nafsi na katika roho pia. Mtu hukamilika kwa roho, nafsi na mwili. Roho siku zote hutaka kutenda mema, lakini mwili una shida ya tamaa; hapo ndipo palipo na fursa ya nafsi kuingilia kati na kufanya utashi wa kutenda utu.
Utashi ndio mwamuzi wa falsafa ya maisha ya mtu mmoja mmoja. Jamii zetu tayari zina utashi huu, zikitarajia kila mmoja wetu aongozwe na falsafa ya UTU, ndio maana si nadra kusikia wanajamii wakimkosoa mtu akosaye utu, wakilalamikia viashiria vya kupungua kwa utu wanavyoviona na kuvisikia katika matukio mbalimbali.

itaendelea...
 
Back
Top Bottom