Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,156
Okay, CCM ina Wabunge karibu 300, ina maRaisi wawili, ina Makamu wa Raisi, ina Waziri Mkuu, ina waziri Kiongozi , ina Spika wa Bunge, ina Mawaziri wote, ina Wakuu wote wa Mikoa, ina Wakuu wote wa Wilaya, inawateua Wakuu wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, inawateua Wakuu wote wa Mashirika ya Umma, inamteua Jaji Mkuu, inateua majaji wote, ina
Mahakama zote, ina magereza yote, inamiliki karibu Viwanja vyote vya Umma vya Michezo, inatoza na kukusanya kodi, inamiliki hata katiba ya sasa, ina.........................
Cha ajabu Chadema ina Wabunge 23 tu, haina Raisi hata moja, haina makamu wa Raisi, haina Waizri Kiongozi, haina Spika, haina Waizri hata moja, haina Mkuu wa Mkoa, haina Mkuu wa Wilaya, haina Mkuu kwenye chombo chochote cha Usalama, haiteui Wakuu wa Mashirika, haimteui Jaji Mkuu, haimteui Jaji hata moja, haiendeshi Mahakama,
haiendeshi Magereza, haimiliki hata kiwanja kimoja cha Umma cha Michezo, haitozi wala kukusanya kodi, inakandamizwa na katiba, haina..........................................
Sasa Mkuu ritz, kwa nini unawaomba wananchi Wananchi kutobabaishwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Chadema kutokana na chama hicho kutokuwa na nguvu ya UMMA ? Hofu yako kwa Chadema inatokana na nini ? Kwa nini Wananchi wakishabikie Chadema,
chama kisichokuwa na chochote cha kuwapa, chama ambacho hakiko madarakani na hivyo kukosa meno ? Woga na hofu yako ritz inatokana na nini huku wewe ndiye umekamata mpini, je unaogopa kuumbuliwa kuwa uko uchi ? (na uko uchi kikwelikweli !)
Asante mkuu nisaidie kumuelimisha huyu anaefikiria kwa kurudi nyuma badala ya kwenda mbele,sasa sijui keshachukua pesa ya kuchafua hali ya hewa himu JF!!?