Falsafa nongwa za Heraclitus: Part Two

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,131
2,008
Wanajamii habari gani

Baada ya kutoa toleo la kwanza juu ya falsafa za gwiji huyu wa kale, sasa naendeleza maana naona dawa haikuingia ipasavyo, chukulieni hili toleo kama mwendelezo wa dozi.

Baada ya kusikiliza yaliyojiri Zanzibari na siasa zake kwa haraka nimeona nitoe dawa, hii dawa ni mahususi kwa wapinzani wa kweli itatuliza mioyo na kuonyesha njia ya kweli

Kaeni mkao wa kula

Katika moja ya sentensi zinazojumuisha falsa za gwiji wetu ni sentensi inayosema "everything change" can't step on same river twice"
Katika hizi sentensi inachomaanisha hapa ulimwenguni kila kitu kina badilika kitu pekee ambacho hakibadiliki ni mabadiliko yenywewe ambayo usiku na mchana yanaendelea kubadilisha taswira ya maisha yetu.

Mabadiliko yataletwa na vijana waliozaliwa miaka ya 2000 na kuendelea hawa wanajulikana kama kizazi Zed hiki kizazi kina uthubutu na mawazo yao yamefunguka haswa itakapofika kipindi cha wao au watoto wao kushika hatamu tutashuhudia mabadiliko makubwa sana katika siasa zetu hapa nchini Tanzania, kwani hawa vijana hawataacha jiwe lolote linalokandamiza au kufunika baadhi ya mambo muhimu yanayokabili taifa.

Hawa vijana wana umoja madhubuti na maono yao yanaenea ghafla sana kwa njia ya mitandao ya kijamii, hakika ambaye atakuwa anazuia mabadiliko ya hawa vijana atakuwa amekaa upande mbaya wa kihistoria, kwani atakachofanywa muumba ndio ajuaye.

Hawa vijana watakuwa na maamuzi binafsi katika nyadhifa zao hata kwa wale watakao kuwa na mamlaka ya polisi hawatasukumwa kimawazo kama makondoo. Nina ndoto angavu kweli kweli juu ya mambo yatakavyomwulikwa kwa mwanga mweupe mwanga wa xenon mwanga wa LED na hichi kizazi.

Ni matumaini yangu hichi kizazi Zed hakitaniangusha. Lakini alas mambo yanabadilika kama falsafa zinavyosema hichi kizazi kitabadilika na mwelekeo wa ubadiliko wake utatokana na maarifa, elimu chanya ambayo wanayo vichwani.
 
Mkuu unauhakika na unacho andika.kwani kizazi cha 80 na 90' kineahindwa nini mpaka hao 2000 waweze nini .Kizazi cha 2000 hata kupiga kura hawaendi ndio walete mabadiriko? Kizazi 2000 kinapenda shortcut. Hakuna misingi yoyote ilioandaliwa ili Kizazi hicho kilete mabadiriko.Kama Kizazi cha 80 and 90 kimeshindwa kuleta mabadiriko basi itachukua miaka 100 Kizazi kingine kuleta mabadiriko.
Binafsi sio dalili ya mabadiriko hivi karibuni katika sekta zote kuanzia siasa uchumi,kilimo na teknolojia.
 
Back
Top Bottom