Falsafa na mbinu ya Uongozi anayoitumia Rais William Ruto itamuwezesha kushinda muhula wa pili Uongozini kirahisi sana 2027

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
16,761
18,764
Kukubali kuondoa muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2024/2025, uliolalamikiwa na kuibua maandamano ya Gen Z, kuvunjwa kwa baraza la Mawaziri na kuwafuta kazi Mawaziri wote waandamizi Serikalini, kusitisha nyongeza ya mishahara kwa Watumishi wa Umma na kupunguza safari za nje, posho, marupurupu ya mishahara hususani kwa wastaafu, kupunguza mshahara wake.

Naibu wake na maafisa waandamizi wengine serikali, pamoja na kusitisha ununuzi wa magari mapya ya idara mbalimbali za serikali.

Mbali na muhimu zaidi ya hayo kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa, yenye uwakilishi wa pande zote za Jamuhuri ya Kenya, kumemfanya kua ni miongoni mwa Viongozi jasiri sana, wasikivu na makini, shupavu wenye maono ya mbali, wastahimilivu na wenye subra sana.

Kwa hakika, Dr.William Samoe Ruto ameonyesha moyo wa Uongozi thabiti na Mzalendo wa kweli Kenya, mwenye nia na dhamira njema kwa wakenya, asie na tamaa, uchu wala ung'ang'anizi wa madaraka.

Amekubali kujishusha na kusikiliza kwa makini sana, tena kwa hekima na busara kuu kila sauti, maoni na mtazamo wa Mkenya juu ya mambo ambavyo wangefurahi yaendeshwe na Serikali yake sikivu ya Kenya Kwanza.

Ama kwa hakika, uongozi wa Rais Ruto una mkono wa Mungu, ni sauti halisi ya wananchi walio wengi, ambayo kwa hakika ni sauti ya Mungu.

Ni dhahiri ana uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda uchaguzi ujao kwa kishindo, kukamilisha muhula wake wa pili mamlakani, na kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa, ataukwaa kirahisi sana muhula wa pili ukilinganisha na upinzani dhaifu sana anaoupata kutoka kwa washindani wake kisiasa.

Gen z wanaendelea kupoa, wanaendelea kugawanyika na hasa kwa kuengemea na kufungamana na upande wa serikali ya Dr Ruto, hali hii ikiashiria vijana wa gen z wanakubaliana na hatua muhimu anazochukua Rais wao katika kuimarisha utendaji wa serikali na kuboresha maisha ya wakenya 🐒

God bless Republic of Kenya
God bless Dr William Ruto, the President of Kenya
 
Ruto ni akili kubwa, sio kama huyu! Eti kafikiria weee kaja na wazo anataka akachimbe dhahabu Serengeti🤣
Anadhani watangulizi wake hawakuwa wanajua kule kuna dhahabu ila yeye katoka Kizimkazi kaja kuigundua leo!
Yaani uharibu mbuga zinazotupa mapato ya uhakika uje kubet kwenye mgodi...by the way migodi imekuwepo miaka mingi imetusaidia nn cha ajabu.
Utalii ndio unaongoza kwa kuongeza mapato hapa nchini.
 
Amekubali kujishusha na kusikiliza kwa makini sana, tena kwa hekima na busara kuu kila sauti, maoni na mtazamo wa Mkenya juu ya mambo ambavyo wangefurahi yaendeshwe na Serikali yake sikivu ya Kenya Kwanza.
Hangaya yeye badala ya kusikiliza maoni ya wananchi, akaamua kuwa Chura Kiziwi
 
Licha ya hayo yote aliyofanya Ruto eti kuna jamaa wanamwandalia maandamano tarehe nane mwezi wa nane wanalenga kumng'oa😎
 
Back
Top Bottom