Miss JF 2023 FaizaFoxy: Wanaonitongoza waje hapa

Faiza....! Si rahisi sana japo inawezekana kwa mtu kua na hisia na mapenzi ya dhati kwa mtu pasi na kumuona.

Si kwa uzuri wa sura wala maumbile yako, si kwa ukubwa wa jina wala umaarufu wako.........
Ila Hekima, Busara na uwezo wako mzuri wa kufikiri na kuchanganua mambo ndivyo vilivyo nivutia kwako.

Bubu mwenye kinywa kizuri hakika maneno yako yameijenga taswira yako katika fikra zangu,
Nifanye niwe wako tafadhali..........!

Naahidi....... Nitakupa utulivu na nitakuongoza vyema.
 
Mwanamke bila kutongozwa haiji, hata posa ni kutongoza amma ukubaliwe amma ukataliwe.

Sema mijitu haina adabu, mtu mzima mke wa mtu zaidi ya miaka 40 anaweza kukuzaa huku anasuka, wewe kinyangarakata unajidai kumtongoza, Wengi hata senti za voucher mpaka wapige mzinga.

Sasa waje hapa, waoneshe utongozaji wao.
Kutongoza kunahitaji faragha mama, halafu umri siyo ishu sana kwenye hayo mambo!!
 
Kutongoza kunahitaji faragha mama, halafu umri siyo ishu sana kwenye hayo mambo!!
Faragha ya nini? Kufanya haramu ndiyo kunahitaji faragha.

Kama unaona ukitongoza hufanyi haramu basi wewe tongoza tu, wazi wazi. Sijaona mnyama akijificha anapotongoza na hata wanapoingiliana. Vipi kitendo cha kinyama kiwe faragha?
 
Kwani kutongoza ni haramu bibie?!!
 
Hicho kiingilio, ukitongozwa na watu 30 tayari una mtaji... alafu mbona umetaja ndogo sana best, weka 50k, mara watu kama 20 hivi una 1m.
Kiingilio hicho nakupa namba unatuma, ni sadaka. Ukiweza zaidi weka.
 
Back
Top Bottom