FaizaFoxy, Mwita25, MalariaSugu, Freedom Is coming... I am out of CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FaizaFoxy, Mwita25, MalariaSugu, Freedom Is coming... I am out of CCM

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Muke Ya Muzungu, Nov 8, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  FaizaFoxy, : Dadangu, hata mie nimezaliwa na kulelewa ndani ya CCM. Nadhani tunahitaji mabadiliko. Sijui unafanya kazi serikalini, au wapi, Mie nafanya Private Sector, lakini baba yangu mzazi ni Waziri kwenye serikali ya Kikwete. Mama ni mtumishi wa serikali pia, lakini nakiri kwamba mabadiliko ni muhimu. Nimeondoka asubuhi na mapema kuja Arusha kujiunga na Wanaharakati na hali ambayo nimeikuta inasikitisha tamaa. Sitaki siasa za majungu za Ngeleja za kuchafua watoto wa makamba

  Hebu fikiria tuliowapa madaraka wanavyojilimbikizia mali kwa wizi. Hebu tazama raia wa kawaida wanavyoonewa. Hali inatisha kwenye mahospitali, vyuo vikuu. Nchimbi katoa wapi utajiri wake, Loawassa, Chenge, Kikwete, Msekwa, Wakina Kinje Mwiru, Wakina Abdala kigoda listi ni ndefu. Watu wa EPA wanadunda mitaani, Richomnd hawajulikani. Dowans ni mapepo, TCRA, UDA listi ni ndefu aliyewajibishwa? Hakuna. liumba kaenda jela kwa sababu ya Demu siyo Ufisadi. Nchi gani hii Dada yangu? unachotetea ni nini? Ardhi inauzwa, rasilimali zetu zinachotwa, Rais ni kuzurura tu cha maana anachokifanyia taifa HAKUNA.

  Mahakama zetu hazina haki, polisi ni majambazi. Sasa tukimbilie wapi? siwezi kuiunga CCM mkono kwa maslahi ya familia yangu au Baba yangu. Ni heri tuishi maisha ya zamani ya umasikini badala ya kuishi kama watumwa. Sitaki nife leo na kuwaacha wanangu watumwa kwenye nchi yao. siwezi kamwe. Sijui unao watoto, ila kama unao, hebu niambie nchi watakayoishi bada ya miaka 10 CCM ikizidi kukaa madarakani ni nchi ya aina gani. Ukiwa na uwezo na nia, sidhani hata CCM ikiondoka utakosa kazi, lakini ukiwa mchafu, lazima utayaona mabadiliko kuwa machungu. Sijui hupo upande gani, nijuzi dadangu.

  Sijui wewe dada yangu au mdogo wangu ila hiyo haijalishi mimi ni (33) watoto wawili wakiume 7 na wakike 9 ambao naomba Mungu wakue na kusoma katika nchi yenye matumaini. Kwa sasa hata kama familia yangu ina uwezo wa kifedha, uwezo tulionao ni wa muda mfupi, kwani tumezungukwa na wengi masikini, kwa maana hiyo hakuna amani. Siwezi kuishi na kuitakasa CCM ni kuishi kitumwa. Na inaniuma sana kukuona kila mara ukishabikia CCM wakati unajua fika kwamba CCM inayumbisha nchi yetu. nilijifungua Aghakan, wewe sijui ulijifungua India lakini pia kumbuka mwanamke mwezio amejifungua kwenye sakafu Temeke.

  Siyo mshabiki wa CHADEMA ila hata kama mabadiliko yataletwa na chama kingine, mara 100 afadhali kuliko kubaki kwenye utawala wa CCM. Sitazami maslahi yangu, natazama Maslahi ya watoto wangu na vitukuu vyao. Samahani sana lakini huo ndio ukweli wa mambo, nadhani kwenye utetezi wako wa CCM fikiria ukweli wa mambo. Ukiniita muhasi, basi waasi watakuwa wengi sana ndani ya CCM. Kama vipi mjadala uendelee....

  Msisahau 15/12/2011 Hakuna kutumia Simu za TIGO..... Ni Wezi wanawanyonya walalahoi. Tupo SIM card yao


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Mh una ujumbe mzito.I think you are right.Bora wewe umejipambanua mapema ili baadaye usije kujutia kama ridhiwan atakavyojutia kwa kutumia madaraka ya baba yake
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  safi...

  sasa napiga nyanga kidogo, halafu baadaye kwenye saa saba hivi naenda kulala.

  Jumapili nina test jamani niombeeni.

  niwatajie venue?
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio CCM tunaojivunia Tanzania, unakwenda unakopenda, ndio demokrasia, hata Mbowe babake na Mkwewe si walikuwa Serikalini?

  Ngoja tumtafute waziri mchaga ni yupi kwa sasa tutamjuwa baba'ko.
   
 5. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,482
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  hao unaowaambia ni vichaa(sanasana huyo FaizaFoxy na Maralia Sugu),czan kama watakuelewa zaid ya kukujbu ovyo,WANA KINYES.I KWENYE UBONGO...
   
 6. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kumjua babangu siyo shida. Babangu hausiki na maamuzi yangu, lakini wewe pia kama mzalendo na mama, ungeangalia hali halisi na kuchukua maamuzi magumu badala ya kufanya ushabiki. Maisha wanayoishi watanzania ni sawa na ya wanyama wa porini. Tungeshirkiana kuleta mapinduzi kuliko kumtafuta baba yangu hayatatusaidia. Jiulize ni nini utakachowaachia wanao....
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Haki ina gharama kubwa kuliko uhai
   
 8. Bebrn

  Bebrn Senior Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kweli mkuu, ila nataka na hapahapa dar lianzishwe ili tuungemkono maana arusha mbali sana kwa sisi wafanyakazi wa serikali
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  topic zingine ni watu wanajifunza kuandika au nini? hazina mantiki..

  Hivi dada chadamu wana uwezo wa kuleta chochote tanzania zaidi ya ubaguzi na vurugu?
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Majibu mepesi kwa maswali magumu...... Ukishamjua Baba yake utafanya nini? Mbona Rachel Masishanga unamjua Baba yake, umemfanya nini?
   
 11. BABU CHONDO

  BABU CHONDO JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Unahangaaikaa na watu wanao lipwa na magamba kwa kutafuta habari hasa huku jamvini ndo kiini cha kuwafinya,wana tetea ugali wao,makachero wa magamba ndani jf,mi haijalishi chama gani tunahitaji maisha ya hali halisi ya watanzania kutokana na rasilimali tulizo anazo inauma kuona srkl inhangaika na wanasiasa badala badala ya kutu boreshea maisha.kama wangekuwa na mwendendo mzuri hata hawa wapinzani wasingepata cha kuongea.
   
 12. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Uhuru 1;

  Maelezo yako yamenigusa sana na hata machozi yananilenga. Hapa nilipo, nipo nje ya nchi kwa shughuli zangu lakini huwezi kuamini ninavyoumia ninavyoona hali ya nchi kwa ujumla inavyokwenda.

  Nimewahi kupost 2 threads; moja iliuliza, ni Kwanini Kikwete asiondoke madarakani, kwani hana jipya na hana Vision kwa ajili ya nchi na wananchi wake na kile alichohitaji ni URAIS na tayari ameshaupata tena kwa miaka 6 sasa; na thread nyingine ilihoji kihusu GHARAMA (BAJETI) za ziara za SALMA KIKWETE Mikoani kama mtendaji wa serikali, je hizo gharama zinakuwa kwenye bajeti ipi ya serikali? niliuliza nafasi ya Familia ya Rais wa nchi kwenye KATIBA yetu lkn cha ajabu hizo thread zote zilitolewa mapema sana kwenye jukwaa na sijajua ni kwanini? ungepata hizo thread, naamini ungeelewa ni kwanini nasema hata machozi yananitoka kila ninapofikiria hali ya nchi yetu na watanzania waliowengi mara baada ya uongozi wa Kikwete; ndiyo maana nazidi KUMWOMBA KIKWETE AACHIE MADARAKA KWA HIARI KWANI UWEZO WA KUSAIDIA NCHI HANA.

  Ndugu yangu, hata mimi ni mwana-CCM, kwani nina kadi ya UVCCM, Wazazi ni CCM; tena mwanachama hai lkn HALI YA NCHI NA CHAMA INANITISHA SANA. Hakika imefika kipindi Tanzania inahitaji Rais mwenye sura mbaya na hata ikiwezekana awe DIKTETA LKN mwenye VISION; mwenye kujua nini thamani ya rasilimali zetu, mwenye kujua nini cha kufanya leo, nini mwakani, nini baada ya miaka 5, n.k. Ni dhahiri kabisa Tanzania inahitaji mtu na si bora mtu yuko IKULU.

  Kuhusu CCM, bado sijaelewa ni wapi nielekee, kwani hata mamabo ya CCM yenyewe nayo hayaeleweki.

  Pole sana Uhuru 1, naamini ipo siku na wala haiko mbali sana tutapata uhuru wetu kwa gharama yoyote ile.
  Nawasilisha.
   
 13. A

  Abu-Musab Senior Member

  #13
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ukihama kimyakimya kuna tatizo? matangazo yako hayana tija wala mashiko.....ukweli ni wa kwako moyoni
   
 14. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona umeamua kujaribu kumpigia mbuzi gitaa, hawa wabadilike? sijui.
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Nani anaetaka Mapinduzi zaidi ya mapinduzi tunayoendelea nayo sasa? Unanchekesha!

  Baba'ko kweli hausiki hilo sina shaka nalo, ila nnahisi ni mchaga. Au sio?
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Bila kumtaja selebriti namba moja unafikiri atauza habari yake?
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna ugumu upi hapo, huyo hata CCM yenyewe hana kadi ya uanachama, usifanye maskhara wewe, "eti" mtoto wa waziri, ndio nini? watu wameona mtoto wa Rais hayupo CCM na wala hawakustuka itakuwa waziri? Unanchekesha!
   
 18. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Dada yangu Uhuru1 hongera kwa kuwa huru na kukubali kuongozwa na utashi na maamuzi yako, ni hatua nzuri.

  Neno moja tu la kukupa courage toka kwa MLK Jr "[FONT=&quot]Our lives begin to end the day we become silent about things that matter" [/FONT]....keep talking on things that matter, without fear
   
 19. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sidhani kama ni uamuzi mzuri kuondoka CCM.kwa mtazamo wangu nadhani mapambano mazuri ya kuwaondoa viongozi wasiofaa yataanzia ndani ya chama chenyewe hasa ktk mchakato wa kura za maoni.Ilipofikia CCM sasa hivi si rahisi kuachia madaraka kwa upinzani kwani wanajua kuwa viongozi wengi wataishia jela.

  Nashauri vijana wengi wajiunge CCM mapema ili kuleta mabadiliko ndani ya chama sivyo utawala wa kurithishana ndani ya ccm utaendelea milele.
   
 20. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  TUMIA MASABURI KUWAZA WE,SIJUI WA KIUME au WA KIKE! Lakini kinacholengwa ni HALI YA USALAMA MKUBWA!
   
Loading...