Fairchild Republic: A-10 Thunderbolt II a.k.a Warthog!

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
The A-10 Thunderbolt II au kwa jina jingine The Warthog ni moja kati ya ndege bora zaidi kwa upande wangu.
Ndege hii ina speed ya 450mph/720kmh na inaweza fikia altitude ya futi 45,000/13kms juu angani, huku ikiwa na uwezo wa kusafiri ardhini kwa maili 2,580/4152kms. A-10 iliundwa mahususi kuikabili ndege ya warusi Su-25.
Su25_Shootdown-top.jpg

Sifa yake kubwa ikiwa ni uwezo wa kushambulia ardhini toka angani (Air-to-Surface attack) wakati huo ikiweza himili mashambulizi ya maadui kutokana na ubora wa body lake.
Usiyoyajua kuhusu ndege hii:
  • Hii ni moja ya ndege bora zaidi kwenye jeshi la marekani na wanaitambua kama "Guardian Angel" kutokana na msaada iliyotoa kwenye vita mbalimbali za marekani huko Kosovo, Iraq, Afghan na Syria.
  • Vifaa vyake vingi kama Engine na Landing gear vinaweza badilishwa pande toka kulia-kushoto hii ikipelekea umiliki wake na kuihudumia kuwa nafuu zaidi.
  • Hata kama vifaa vyake vingi kama hydraulic systems, brake system na mfumo wa dharula utakuwa umeharibiwa lakini rubani wake anaweza iendesha mpaka kwenye kambi yake bila kuathirika sana.
    Kim_campbell_damage_a10.jpg
  • Inachukua upana mfupi sana kuruka, kiasi haihitaji eneo kubwa na hata jangwani inaweza tua na kupaa bila shida.
    5abbfbd45c0d6364798b4739-1334-1000.jpg
  • Mbele ya ndege hii pamewekwa bunduki aina ya GAU-8/A cannon ikiwa na matundu saba yanayoweza toa risasi mpaka 4,200 kwa dakika!. Hii ni ndege pekee iliyofungwa aina hii ya bunduki.
    A10gun3.jpg
    noseviewofana10thunderboltiiaircraft.jpg
  • Baada ya Gulf War jeshi la Marekani lilipanga kuzibadili kwenye system yake kwa kuleta F-16, lakini kutokana na ubora iliyoonyesha kwenye vita ile Bunge la marekani likaamua zibaki na toka hapo zimekuwa ndege bora zaidi kwenye mashambulizi uwanja wa vita.
    188th_FW_A-10_Warthog_fires_Maverick_in_training.jpg
  • Inatambulika kama Tank Aircraft (kifaru kinachopaa) kutokana na ugumu wa material yaliyotumika kuitengeneza body lake.
    A10FactSheet.jpg
  • Kutokana na ukasi wake na mashambulizi inayoweza fanya, Imekuwa ni kivutio kwenye filamu mbalimbali kama Transformers, Terminator, Man of Steel, Jarhead etc.



5a54f121c32ae644008b5412-750-375.jpg
5ab3c899410e841d018b488c-750-375.jpg
70-80_TechInnovation_36x24_72dpi_NEW.jpg
 
Kwanini hata sisi hapa tusiwe nayo hata moja, badala yake tunazidi kichukua 'bombadia'!
 
Back
Top Bottom