‘Fair comments’ kuhusu CCM, Vyama mbadala na Uchaguzi wa Oktoba

Unaposema bora CCM kuliko upinzani sijui kama unakumbuka 2015 walivyomfuata Lowassa Chadema? na hao hao tena wakaja kumfuata alivyorudi CCM? umetumia maneno "relatively better" kuhalalisha CCM iendelee kubaki madarakani, binafsi sioni huo unafuu unaouzungumzia kwa hiyo CCM.

Kwa upande wa upinzani; unaweza vipi kukilaumu chama kwa baadhi ya wanachama wake kununuliwa? hawa watu wananunuliwa kwasababu hawana misimamo wako selfish, hilo sio tatizo la chama, ni tatizo la watu binafsi, na hata wale waliokimbia CCM kumfuata Lowassa Chadema walienda kwa sababu zao binafsi, sio kosa la chama chao, ni ubinafsi wao.

Simply put; siasa za nchi yetu zimetawaliwa na wanasiasa wenye tamaa ya madaraka, na wako tayari kupata chochote wanachotaka bila kujali upande, wako wanaoondoka chama kimoja kwenda kingine kwa mapenzi yao binafsi, na wapo wanaoondoka chama kimoja kwenda kingine kwa kurubuniwa, tuliona hilo 2015, na tuona tena sasa 2020, na Mungu akipenda tutayaona tena mengine 2025 kutegemeana na upepo wa kisiasa utakavyovuma.

Mpaka pale wanasiasa wetu watakapostaarabika, wakaacha kuweka matumbo yao mbele kwa maslahi yao binafsi, wajue jukumu lao ni kuwatumikia wanatanzania, mtu akatae kuhama chama chake hata kama akirubuniwa kwa pesa, siasa zetu zitaendelea kuwa za maigizo tu, japo wako wachache wenye misimamo, wanatumika kama mfano.
 
Tukianza kuingia ndani sasa kwenye mizania yetu, tunaanza kuangalia dhana ya kwanza ambayo ni "kiwango cha kujitambua miongoni mwa viongozi na wanachama wa CCM na wale wa vyama mbadala".

Ijapokuwa ni vigumu kutoa hitimisho ambalo linaakisi uwezo wa kujitambua wa kundi kubwa la watu kwa kuwa kila mtu ana tabia tofauti na kwa kiwango tofauti, bado kuna vigezo mbalimbali ambayo tunaweza tukavitumia kujua chama kipi kina uafadhali dhidi ya kipi.

Kwa muktadha wa mada hii tutatumia vigezo viwili kupima uwezo wa kujitambua kati ya pande mbili tunazojaribu kuzilinganisha. Kigezo cha kwanza ni uwezekano wa kununulika dhidi ya uwezekano wa kununua, na uwezekano wa usaliti dhidi ya uwezekano wa kusimamia kile mtu anachoamini.

Kigezo cha kwanza kuhusu kununuliwa dhidi ya kununua; tumekuwa tukiona viongozi kadhaa wa vyama vya mbadala wakihamia CCM. Wao kwa maelezo yao wanadai wameona udhaifu kwenye vyama hivyo na wameona unafuu kwenye CCM lakini kwa maelezo ya vyama vyao ni kwamba wanakuwa wamenunuliwa na CCM. Tuchukulie kuwa maelezo ya vyama vyao ndio sahihi, na wanakuwa wamenunuliwa kweli.

Ijapokuwa kununua watu na kununuliwa yote sio mambo mazuri, Ni jambo la wazi kwamba kiongozi anayenunulika kirahisi kiwango chake cha kujitambua kiko chini kuliko anayenunua mwenzake. Hii haijalishi ni kwa nini mnunuaji ananunua na kwa nini mnunuliwaji ananunuliwa.

Kwa mantiki hiyo, kuelekea uchaguzi mkuu, ni afadhali kumuamini anayenunua walioko tayari kununuliwa (ikiwa kweli ananunua) kuliko kuamini anayenunulika kirahisi (ikiwa kweli ananunuliwa) kwa sababu anayenunulika leo hata kesho atanunulika na ni vigumu kujua atakayemnunua ni nani na kwa gharama gani.

Kuhusu kigezo cha pili cha usaliti, kumekuwa na sauti nyingi zaidi zikilalamikia usaliti ndani ya vyama mbadala kuliko CCM. Ikiwa wanaolalamikiwa kuwa ni wasaliti ni wasaliti kweli, na wanafanya usaliti wakiwa hawajapewa madaraka makubwa na imeshindikana kuwabadili katika level za vyama vyao, maana yake wakipewa madaraka makubwa zaidi ni ngumu kujua nani atakayemsaliti nani juu ya nini na kwa kiasi gani.

Ijapokuwa hata CCM kuna malalamiko ya usaliti, malalamiko hayo si kwa kiwango kile ambacho kinasikika kutoka kwenye vyama mbadala na kwa mantiki hiyo, tunaweza kusema kuna uafadhali kwa kiwango fulani.

Kama hayo mawili ni kweli, basi ni sahihi kusema wale ambao wananunua wengine wanajitambua kuliko wanaonunuliwa na wenye kiwango kidogo cha usaliti wanajitambua kuliko wenye matukio mengi wanayodai wenyewe ni ya usaliti.

Mtu anayejitambua zaidi ya mwenzake ana nafasi nzuri ya kuwa kiongozi bora zaidi ya mwenzake na hapo ndipo tunapokuja na hitimisho la uafadhali wa CCM ukilinganisha na vyama mbadala.
Keep grinding
 
Tunaendelea
=========

Tunaenda kwenye mizania ya pili; uwezo wa rasilimali Watu ndani ya CCM dhidi ya vyama mbadala na hitimisho tunalofikia.

Rasilimali watu ndio rasilimali muhimu zaidi kwenye siasa na mambo ya uongozi wa nchi. Katika taasisi yoyote unapotafuta rasilimali watu ya kujaza nafasi fulani ili kufanya shuguli Fulani; unajaribu kuainisha vigezo vya msingi vinavyohitajika ili kufanikisha kazi husika kwa ufanisi.

Wakati fulani hutokea kuwa kwenye uwanda 'scope' fulani hawapatikani watu wenye sifa kamilifu za kufanya kazi husika au wanaopatikana ni wachache kuliko uhitaji. Hali hiyo inapotokea kuna mambo mawili ya kufanya; kwanza ni amma kwenda nje ya uwanda wa utafutaji au pili kuwaendeleza wanaopatikana katika uwanda husika kwa kuwapatia mafunzo ya ujuzi 'skills' zinazotakiwa ili kuwajengea uwezo kuwa vile wanavyotakiwa kuwa.

Kwa bahati mbaya au nzuri, kwenye siasa kuna uwanda maalum wa kupata watu 'Limited scope' ambayo ni vyama vya siasa vilivyopo ndani ya nchi husika, huwezi kwenda nje ya hapo. Kwa hiyo wakati mwingine tunapojikuta tunahitaji viongozi wa aina fulani, na hatuna watu wa aina hiyo wa kutosha au wenye sifa kamilifu, njia pekee ni kuwazalisha kwa kupitia mafunzo.

Vyama vya siasa tulivyo navyo havijawekeza vyakutosha kwenye eneo hili la mafunzo ili kuandaa viongozi wenye uwezo, tabia na upeo wa kuridhisha. Hata hivyo ukifanya ulinganifu, unabaini kwamba CCM angalau imepiga hatua fulani ukilinganisha na vyama mbadala. Ijapokuwa haifahamiki vizuri kama wanatoa mafunzo ya namna gani na kwa kiasi gani, Angalau wana vyuo vyao na wanaonekana wanaona umuhimu katika hili ukilinganisha na upande wa pili.

Kwa upande wa vyama mbadala hawana vyuo, hawaoneshi mpango wa kuwa navyo, hawafanyi mafunzo yanayoeleweka wala hawaoneshi kuwa na mpango huo. Licha ya kushauriwa mara kadhaa kufanya hivyo hata 'online' hawajawahi hata ku 'appreciate' ushauri huo achilia mbali kuukubali au kueleza ni kwa nini hawafanyi hivyo.

Matokeo yake, wana 'recruit' watu randomly, kila mtu akiwa na tabia zake na uelewa wake, na kwa kuwa tu wamejiunga na vyama vyao, wanaanza kujiaminisha na kuiaminisha jamii kuwa tayari wameshakuwa na uwezo mkubwa na wakutosha wa kiuongozi kwa kuwa pale tu 'kwenye vyama mbadala'. Lakini ukweli inakuwa ni kujidanganya na kudanganya watu.

Ushahidi wa kwamba kunakuwa hamna lolote tunaweza kuupata kwa kuangalia utendaji wa badhi ya viongozi wa ngazi za juu wa vyama mbadala waliopewa nafasi za utendaji serikalini, tabia zao, uelewa na namna wanavyotatua matatizo mbali mbali kwa kuwalinganisha na wale wa CCM ambao wapo madarakani siku zote. Jibu la mlinganisho huu ndilo linapelekea kufikia hitimisho tunalofikia.

Hivyo basi, Ijapokuwa tuna tatizo la upungufu wa watu wenye uwezo mzuri wa kiuongozi na tabia zinazofaa nchini na hivyo kusababisha baadhi ya viongozi kufanya mambo ya kushangaza mara kwa mara, bado tunaweza kusema CCM wana rasilimali watu yenye uafadhali na angalau wanaona umuhimu wa kuendeleza na kuwajengea uwezo viongozi wake kuliko vyama mbadala na hivyo kuwa kwenye nafasi ya kufanya vizuri zaidi ukilinganisha na upande wa pili.
 
Ombi lako halijakubalika kwa sababu halina mantiki.
Itaendelea kwa kadiri muda utakavyopatikana. Tatizo unadhani kwamba kila mtu yupo duniani kukutumikia na kukuridhisha wewe halafu wewe uko kwa ajili ya kutumikiwa na kuridhishwa. Wewe kama ukiona mada haikuhusu fanya yanayokuhusu, mengine achia wengine.

Kwa hiyo mada ikiendelea huna muda wakuchangia, ila isipoendelea utakuja kuchangia, hivyo unashauri isiendelee ili uje kuchangia, yaani kwa lugha nyingine uje kuchangia kitu ambacho kimsingi hakipo, sio?

Sipingi mada yako au mpaka hapa ulipofikia, lakini jitahidi kusimama neutral maana watu makini tunakuangalia. Nitachangia baada ya hatua fulani.
 
Sikujua.

Kumbe mada yako umeiulia hapa?

Baada ya kusoma uliyoweka kwenye bandiko lako la mwanzo, nilipenda sana uwasilishaji wa mada ulioufanya. Kwa hiyo ndio nikajibu kwa mchango wangu hapo #12.

Ndipo nikaanza kusoma michango toka chini kupanda juu, hadi huu hapa ulioweka #2.

Inawezekana sana hili darasa ukabaki nalo mwenyewe, au na wasomaji wachache sana.
Kujifunza kusikia unachopenda kusikia na usichopenda kusikia ndio demokrasia yenyewe. Kupenda kusikia unachotaka kusikia tu huo ni udikteta. Aidha, udikiteta ni tabia na demokrasia ni tabia pia. Haihitaji uwe na cheo kikubwa sana ndio uwe dikteta au mwana demokrasia. Ndio maana sisi wengine hata tunafikiri kuzuia kuibuka kwa madikteta hatari mbele ya safari, tunatakiwa tushughulike Zaidi na kujenga mtizamo kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wa baadae angali bado mapema.

Kwa bahati mbaya wengi wetu hupenda kujisikiliza wenyewe, au kuimbiwa wimbo mzuri sana unaotupa sifa tusizokuwa nazo huku tukichekacheka kwa mbali.

Kuhusu wengi na wachache kujadili mada; Mabadiliko hayajawahi kuletwa na watu wengi, watu wachache ndio huleta mabadiliko chanya. Watu wachache ndio wenye uelewa mzuri wa mambo, watu wachache ndio wenye tabia zinazokubalika, watu wachache ndio wakweli, watu wachache ndio wanaweza kuwa waaminifu. Kwa hiyo mada yoyote yenye mambo hayo inapaswa kujadiliwa na wachache kuliko wengi.

Ukitaka watu wengi, tafuta mtu umlaumu au kumchafua, utapata watu kibao.
 
Ombi lako halijakubalika kwa sababu halina mantiki.
Itaendelea kwa kadiri muda utakavyopatikana. Tatizo unadhani kwamba kila mtu yupo duniani kukutumikia na kukuridhisha wewe halafu wewe uko kwa ajili ya kutumikiwa na kuridhishwa. Wewe kama ukiona mada haikuhusu fanya yanayokuhusu, mengine achia wengine.

Kwa hiyo mada ikiendelea huna muda wakuchangia, ila isipoendelea utakuja kuchangia, hivyo unashauri isiendelee ili uje kuchangia, yaani kwa lugha nyingine uje kuchangia kitu ambacho kimsingi hakipo, sio?
Wewe ni mmoja wapo kwenye hilo kundi wanaolipwa pasipo kujitambu wanapigania nini. Ulichoandika umeangalia zaidi njaa zako.
 
Kujifunza kusikia unachopenda kusikia na usichopenda kusikia ndio demokrasia yenyewe. Kupenda kusikia unachotaka kusikia tu huo ni udikteta. Aidha, udikiteta ni tabia na demokrasia ni tabia pia. Haihitaji uwe na cheo kikubwa sana ndio uwe dikteta au mwana demokrasia. Ndio maana sisi wengine hata tunafikiri kuzuia kuibuka kwa madikteta hatari mbele ya safari, tunatakiwa tushughulike Zaidi na kujenga mtizamo kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wa baadae angali bado mapema.

Kwa bahati mbaya wengi wetu hupenda kujisikiliza wenyewe, au kuimbiwa wimbo mzuri sana unaotupa sifa tusizokuwa nazo huku tukichekacheka kwa mbali.

Kuhusu wengi na wachache kujadili mada; Mabadiliko hayajawahi kuletwa na watu wengi, watu wachache ndio huleta mabadiliko chanya. Watu wachache ndio wenye uelewa mzuri wa mambo, watu wachache ndio wenye tabia zinazokubalika, watu wachache ndio wakweli, watu wachache ndio wanaweza kuwa waaminifu. Kwa hiyo mada yoyote yenye mambo hayo inapaswa kujadiliwa na wachache kuliko wengi.

Ukitaka watu wengi, tafuta mtu umlaumu au kumchafua, utapata watu kibao.
Jamaa kaja kuchangia mada akiwa ana msimamo wake na anataka anachoamini yeye kifanane na wengine ingekuwa tufanana kifikra shuleni tungekuwa tunapata grade sawa.Kama anataka mtazamo wake uwe sawa na wengine asingejiunga na jamiiforum badala yake angejifungulia forum yake yenye watu wenye itikadi sawa na yake.
 
Kujifunza kusikia unachopenda kusikia na usichopenda kusikia ndio demokrasia yenyewe. Kupenda kusikia unachotaka kusikia tu huo ni udikteta. Aidha, udikiteta ni tabia na demokrasia ni tabia pia.
Mkuu, hii ni mipasho tu kama maneno ya kwenye kanga. Mtu makini huwezi kupoteza muda wako na habari kama hizi.
Hayo mengine huko chini sikuyasoma.
 
Jamaa kaja kuchangia mada akiwa ana msimamo wake na anataka anachoamini yeye kifanane na wengine ingekuwa tufanana kifikra shuleni tungekuwa tunapata grade sawa.Kama anataka mtazamo wake uwe sawa na wengine asingejiunga na jamiiforum badala yake angejifungulia forum yake yenye watu wenye itikadi sawa na yake.
Hapana, unakosea.

Soma mchango nilioweka #12.

Mada kaianza vizuri, halafu anaivuruga baadae.
 
Jamaa kaja kuchangia mada akiwa ana msimamo wake na anataka anachoamini yeye kifanane na wengine ingekuwa tufanana kifikra shuleni tungekuwa tunapata grade sawa.Kama anataka mtazamo wake uwe sawa na wengine asingejiunga na jamiiforum badala yake angejifungulia forum yake yenye watu wenye itikadi sawa na yake.
Wakati huo huo watu wenye mtizimo kama wake utawakuta mahali wanalaani udikteta, hawajui msingi mkuu wa udikiteta ni mtu au kundi la watu kutaka watu wote wafikiri kama wao. Yaani tuna kazi kubwa sana, na tabia hiyo wanayoonesha peke yake ni ishara tosha kwamba CCM pamoja na changamoto zake, bado ina uafadhali mkubwa. Hili tutalifafanua zaidi tutakabyozungumzia kipengele cha maoni na ukosoaji
 
You're turning out to be boring to read! I am tuning out mate.
 
You're turning out to be boring to read! I am tuning out mate.
Ila ulishaaga kitambo ndugu yangu, naona unaenda unakaa kaa unarudi, unalalamika umekuwa bored na hutatangia tena, ukikaa kaa unarudi tena, unadai huna muda, ukikaa kidogo unarudi tena unasema huwezi kuchangia kitu kitakachoongeza thamani kwenye mada,.......

Sasa kama ushaamua hivyo , siukae utulie? Au angalau utafute mtu umlaamu nafsi yako ipoe?
 
Unaniitaita sana; basi ngoja nikuage rasmi hapa.

Ningeamua kuku'engage' kwa uandishi wako huu usingepiga kona.

Nimeamua maksudi nisikupe nafasi usiyostahiri.

Wewe kazana na mada yako, usigeuke na kufanya mjadala wa pembeni na mimi ndio iwe sababu ya kutoiendeleza mada yako ambayo tayari imebuma.
 
Ndugu yangu Kalamu1, mimi nilitambua mapema kabisa kwamba hapo hakuna kitu na hata misahafu inatuambia hivi;

Do not answer a fool according to his folly,
Or you will also be like him.
Answer a fool as his folly deserves,
That he not be wise in his own eyes.​

Naye Mark Twain aliwahi kutonya hivi, "never argue with a fool, onlookers may not be able to tell the difference.”
 
Kuhusu 'internal control mechanisms',

Vyama vya siasa Tanzania vina Tatizo kubwa la internal control mechanism. Vinapata shida kubwa kujichunguza, kujitathmini, kujiboresha na kujisahihisha vyenyewe kutokea ndani. Kwa kiwango kikubwa, vinaona nje bila kuona ndani.

Hata hivyo, ukijaribu kuangalia kwa umakini, bado utaona kwamba CCM iko mbali sana ukilinganisha na vyama vingine. Angalau CCM inaonekana ina mifumo yenye uafadhali mkubwa wa kujipima, kujitathmini na kujisahihisha kutokea ndani ukilinganisha na vyama vingine ambao amma havina kabisa mifumo hiyo, au ipo lakini haijawahi kufanya kazi.

Mfano mzuri ambao tunaweza kuutumia wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu, ni namna CCM inavyojaribu kudhibiti rushwa za uchaguzi ndani ya chama katika kipindi hiki na jinsi polepole alivyopata ujasiri wa kuliweka wazi jambo hilo mara kwa mara. Hili ni jambo zuri ambalo ilipaswa vyama mbadala vifanye vizuri Zaidi kwenye hili. Hata hivyo kwa sasa, bado havijaweza kuwa na ufanisi wowote kwenye kujitathmini kutokea ndani licha ya ushauri ambao wamekuwa wakipatiwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

Les brown aliwahi kusema "If you can fight the enemy within, the enemy without can do no how"
 
Back
Top Bottom