Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kwenye siasa za Tanzania, kuna watu wanafanya wanachofanya kwa kuwa tu wanalipwa, kuna wengine kwa sababu ya ushabiki tu, wengine changamoto ya uelewa wa mambo, na wachache kwa sababu wanaelewa wanachokifanya na wanajua umuhimu wake kwao wenyewe, jamii na hatima ya Tanzania.
Kwa bahati mbaya, kundi la washabiki na wenye changamoto ya uelewa ndilo kundi kubwa zaidi ya hayo mengine na kupelekea tafiti mbalimbali kuonesha kuwa mara nyingi wapiga kura walio wengi wanakuwa hawajui wanachokifanya. Kwa mantiki hiyo, kuelekea kipindi cha uchaguzi kama sasa; ni muhimu kuyasaidia makundi haya kujua kipi ni kipi, ikiwaje matokeo gani yanatarajiwa na kwa nini. Ni muhimu kufanya hivyo kwa lugha rahisi ili angalau watakapoamua wajue wanaamua nini na ili iwe nini.
Dhana ya vyama mbadala nyakati za uchaguzi, haipo kwa ajili tu ya kuwapa watu uhuru wa kuchagua au kujifurahisha tu, bali kuchagua ambacho kina uafadhali Zaidi ya vingine. Hivyo basi ili kuepuka uwezekano wa kuchagua hatari Zaidi badala ya afadhali, ni muhimu kujiridhisha kwamba anachochagua mchaguaji ni bora kuliko unachokikataa.
Hoja ya kwamba unachokikataa mtu kina udhaifu fulani, hoja hiyo pekee haitoshi kuchagua mbadala wake, ispokuwa kama amejiridhisha kuwa huo mbadala ni bora zaidi. Kwa mfano, kama una simu inakaa na chaji masaa nane tuu, hilo linaweza kuwa ni tatizo lakini hilo peke yake haitoshi kuwa sababu ya kubadili simu hiyo, ispokuwa kama umejirishisha kwamba simu mbadala unayotaka kutumia inaweza kutunza moto zaidi ya hiyo ya awali.Kwa mantiki hiyo ni vyema kujenga uelewa juu ya hili kwa ajili ya makundi tajwa hapo juu.
Hili la kujenga uelewa ni muhimu sana maana makundi tajwa hapo juu ambayo ndio makubwa, hayawezi kuamua yakijua yanaamua nini 'Making rational and informed decisions' hivyo kufanya bahati nasibu 'Liwalo liwe'. Kwa bahati mbaya michakato inayozalisha viongozi hasa wa ngazi za juu wa kisiasa sio ya kufanyia bahati nasibu kwa kuwa hao ndio huamua hatma ya Maisha ya watu kwenye kila sekta.
=======
Inaendelea (Ni mjadala mpana sana, kwa hiyo tutaenda taratibu)