Faini ya CAF kwa Biashara inatisha

Pamoja na ukata lakini ifike Muda timu ziendeshwe na wataalamu. Acheni mambo ya uswahili yamepitwa na wakati.
 
Haijawahi kutokea katika historia ya michuano ya CAF kuanzia ile iliyokua inaitwa Klabu Bingwa Afrika na Kombe ya Washindi(Cup Winners Cup) hadi kombe la Shirikisho kwa timu ambayo imeshinda mechi ya kwanza tena kwa idadi ya mabao kama walivyoshinda Biashara kisha wakashindwa kwenda kwenye mechi ya marudiano

Kuna timu inaitwa Chapungu kutoka Zimbabwe iliwahi kufu gwa na Simba bao moja kuke Harare na wakaacha kuja Dar kwenye mechi ya marudiano. Jamaa walipewa adhabu ya fine na wakatakiwa kuilipa fidia Simba ya dola elfu 30 na walifanya hivyo!

Biashara wamevunja rekodi. Nakumbuka Mtibwa Sugar nao waliwahi kufungiwa kwa kosa kama hili lakini angalau wao walikua wamepoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa idadi kubwa ya magoli na wakaona huko ugenini ni kwenda kuabika tu

Timu kama hizi ni kuzipiga nyundo kwa kuzipoka point hata kwenye ligi maana huko ni kukosa umakini kwa hali ya juu kabisa katika uongozi wa soka kwa level ya kimataifa
 
Ajira zilivyokuwa ngumu..vijana wanapambana kutumia vipaji vyao ili waokoe maisha yao na ya watu wengine..ila sasa wanatokea wahuni wachache wanaamua kutotambua juhudi za vijana na wanafanya ujinga vijana wanafungiwa hivihivi..serikali ipo ipo tu, ni huzuni sana kama taifa
 
Back
Top Bottom