Faini ya bodaboda ilistahili kuwa Shilingi 50,000; tutashuhudia mengi kwa wasiozingatia usalama

Ninavyofahamu mm kanuni mojawapo ya adhabu/faini lazima iwe inaumiza ili usirudie kosa..

Sasa hawa badala ya kupandisha faini wao wanashusha, sijajua lengo ni kuzuia makosa au kukusanya pesa.

Faini inapaswa kuwa kubwa maradufu ili watu waogope kufanya makosa tena muda mwingine kwa makusudi kabisa.
 
Binafsi sijafurahishwa na faini za bodaboda kushuka na kuwa 10,000/-kwani kwa jinsi ninavyowafahamu hawa ndugu zetu na rika lao,10,000/- itakuwa si chochote kwao na watadharau sana utaratibu wa barabara zetu hivyo huenda maafa yakawa makubwa zaidi kuliko vile itakavyofikiriwa.

Jambo lingine ambalo napingana nalo ni kuwa, bodaboda wengi kutokana na faini kuwa kubwa wanashindwa kukomboa pikipiki zao, sidhani kama hili lina mashiko maana nyingi ya pikipiki zinazoshikiliwa vituoni ni zile ambazo zinakuwa zimehusika na matukio mbalimbali yakiwamo ya wizi, ujambazi, aidha pikipiki hiyo kumilikiwa isivyo halali na anapotakiwa mwenyewe ajitokeze mhusika hukimbia mazima.

N.B: Sekta hii imeleta ajira nyingi Sana kwa vijana wetu na ujana ni maji ya moto na maafa yanayosababishwa na vyombo hivi hugharimu maisha ya wengi ambao ni abiria wa vyombo hivi, madereva wa vyombo hivi wanastahili mafuzo maalumu ya usalama barabarani kuliko hata madereva TAXI kama kweli tunawapenda usalama wao na abiria wao.
Kwanza hao bodaboda huwa wanakamatika kweli au ndio ujinga tu? Labda Bajaj Ila Bodaboda kumkamata sio rahisi na sijawahi kusikia boda analalamika amepigwa mkono na trafiki, wao huwa wanapambana na wale askari wenye pikipiki na wanachukua rushwa wanaishia hakuna anayekamata.

Pia ajali itazidi Hawa wahuni ni shida tena Bajaj nao ni tatizo kubwa sana. Tutaona.
 
Back
Top Bottom