Faini kwenye alama za tahadhari barabarani ni wizi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,827
Pana u umbumbu mkubwa wa alama za barabarani kwa upande wa askari polisi barabarani. Ilikuwa ni vyema serikali ikaliona hili na kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Pana yanayoitwa makosa barabarani ambayo yanayotumiwa na polisi kama kisingizio kwa kujua au kutojua. Mwisho wake ukiwa kubambikia watu makosa kiujanja ujanja ili kuwaibia tu. Faini za makosa kama haya kimsingi ni wizi usiokuwa na tofauti na ule wizi wa kutumia nguvu.

Alama za barabarani zimegawanywa katika makundi:

1. Tahadhali
2. Amri
3. Taarifa

Tahadhali zinakuwa ndani ya mabango ya pembetatu. Kundi hili lina lengo la kumtaarifu mtumia barabara kuwa makini na eneo analo pita, hakuna cha zaidi ya hapo.

Alama hizi huwa ziko katika mabango ya pembetatu. Polisi na watumiao barabara wangeelimishwa kuhusiana na hili kuhakikisha haki Ina prevail. Mbivu na mbichi zikafahamika vinginevyo tunakoelekea uvunjifu wa amani utakuwa unatuhusu.

Hivi serikali inajisikia vipi kuwa na polisi wasiotenda haki? Kuwa na polisi wanaotanabaishwa na majambazi?

Alama zinazokuwa enforced na polisi ni za amri pekee ambazo hizi huwa kwenye mabango ya duara.

Polisi kutoza faini ati kuwa kuna alama tu za zebra crossing zisizoambatana na spidi inayoruhusiwa si sahihi. Ikumbukwe kuwa kuna sehemu zenye max speed 50km/h na zebra crossing na zipo zingine kwenye barabara kuu zenye zebra crossing peke yake.

Barabarani kumekaa kama uwanja wa mazoezi kila polisi na lake kinachotakiwa pesa. Chapisheni brosure zenye makosa maonyo, makosa na faini explicitly ili kila mtu azione wazi wazi tuache na ubabaishaji. Vinginevyo kitengo hiki ni shida tu.
IMG_20200227_074314.jpg

Muda muafaka wa kusimama imara kusimamia haki zetu ambazo kwa uzoefu wa njaa za hawa jamaa watabambika kesi hata kwa makosa yasiyokuwapo.
IMG_20200227_074318.jpg

IMG_20200227_073519.jpg
IMG_20200227_073519.jpg
IMG_20200227_073519.jpg
 
Attachments

  • en1473326813-A GUIDE TO TRAFFIC SIGNING.pdf
    1.2 MB · Views: 8
Uzi Kama huu usokua na mifano Ni wa kuupuuza

Mkuu nimekuta mtiti polisi karibu kuchezea kichapo.

Wamepanga msururu wa magari wakidai vyao kuwa pana kibao cha tahadhari cha waenda miguu ambao hata hivyo hawakuwapo.

Hakuna kibao cha spidi limit wao wana force 50km/h.

Unfairly so.
 
Trafic wamekua ni sehemu ya TRA kukusanya mapato, sambamba na DPP. Nchi yetu watu wanaoongoza kwa dhuluma na uhuni ni Trafic Police, hata sheria hawazijui ila wanakaririshwa tu makosa.

Juzi kanikamata Trafic, wakati ananihoji kuhusu lesseni yangu mkononi kwake ameshika simu kafungua App ya kubet mpira (Police anacheza kamari muda wa kazi, saa ngapi atatenda haki anapikamata mtu).
 
Mkuu ngoja nisubscribe kabisa t0pic hii.

Umeichimba mno, tena kiundani sana.

Mimi na udereva wangu wa miaka nendarudi, lakini kuna alama nyingi hapo sijawahi kuziona barabarani na me mwenyewe sizijui, acha kuzielewa.

Ahsante kwa kuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Nakereka Wanavyoongoza Magari Sehemu Ya Round About---

Asee Nakereka Sanaa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tukubali au tusisitize kwenda mahakamani kusomewa kosa ili kupata usahihi wa maamuzi ya askari wa barabarani, bila hivyo wataendelea tu kutupora fedha na kutubambikia makosa.
 
Uzi Kama huu usokua na mifano Ni wa kuupuuza

Nyuzi nyingine tutaambatanisha na majina au namba zenu. Si mnazivaa vifuani?

Acheni ubabaishaji alama ya tahadhari katu haiwezi tozewa faini.
 
Mkuu nimekuta mtiti polisi karibu kuchezea kichapo.

Wamepanga msururu wa magari wakidai vyao kuwa pana kibao cha tahadhari cha waenda miguu ambao hata hivyo hawakuwapo.

Hakuna kibao cha spidi limit wao wana force 50km/h.

Unfairly so.

Je palikuwa na makazi ya watu? ni wapi hapo mkuu ili tuchangie bila kuleta maumivu.
 
Tukubali au tusisitize kwenda mahakamani kusomewa kosa ili kupata usahihi wa maamuzi ya askari wa barabarani, bila hivyo wataendelea tu kutupora fedha na kutubambikia makosa.

Mkuluro wa alama za tahadhari zipo za kuonyesha:

Kuwepo kwa mteremko mkali, mpando mkali, kuwepo kwa kona kali Julia au kushoto, barabara ya mchepuko mbele kulia au kushoto, nk kunatozwa faini vipi?

Majizi nyie hatukubali tena kuonewa nanyi.

Membe usikatishwe tamaa hawa jamaa wametuudhi wengi. Yanayoweza kubadilika yakatuletea haki tutayakaribisha.

2020 twende na membe.
 
Je palikuwa na makazi ya watu? ni wapi hapo mkuu ili tuchangie bila kuleta maumivu.

Makazi ya watu ni moja ya hizo janja janja zao. Wekeni alama za amri - zenye speed limits ndani ya mabango ya duara. Vinginevyo hatulipi faini zenu bambikizi ati kuwa kuna makazi ya watu.

Sehemu ipi ya barabara haina nyumba pembeni? Acheni janja janja zenu.
 
Mkuu nimekuta mtiti polisi karibu kuchezea kichapo.

Wamepanga msururu wa magari wakidai vyao kuwa pana kibao cha tahadhari cha waenda miguu ambao hata hivyo hawakuwapo.

Hakuna kibao cha spidi limit wao wana force 50km/h.

Unfairly so.
Mkuu hii sheria hauifahamu vizuri.
Sehemu yoyote yenye tahadhari ni lazima upunguze spidi.

Lakini pia umeweka bandiko ambalo wewe mwenyewe hujalipitia kabisa.
Kwani umetaja makundi matatu ya sheria ya barabara, wakati sio sahihi, hata kabrasha lako linajielezea vizuri kabisa.
Soma kwa kwanza uelewe ndio utoe lawama.
 
Nyie ni wale polisi uchwara mnaotoza faini kwenye alama za tahadhari?

Kwamba kuna tahadhari mlima wa kupanda, au kona kulia hapo spidi gani ya kuendesha?

Acheni wizi - nendeni shule mkasome!
 
Nyie ni wale polisi uchwara mnaotoza faini kwenye alama za tahadhari?

Kwamba kuna tahadhari mlima wa kupanda, au kona kulia hapo spidi gani ya kuendesha?

Acheni wizi - nendeni shule mkasome
Naona hauna uelewa wa kutosha kwenye mambo ya sheria za barabarani.
Husemi hoja ila unabisha tu.
Alama yoyote barabarani ina maana na ukiikiuka lazima uadhibiwe Hata kwa onyo tu.
 
Naona hauna uelewa wa kutosha kwenye mambo ya sheria za barabarani.
Husemi hoja ila unabisha tu.
Alama yoyote barabarani ina maana na ukiikiuka lazima uadhibiwe Hata kwa onyo tu.

Kuna alama ya kuwa utakuwa unapanda mlima au kuna kona kushoto - hizo ni mfano wa alama za tahadhari. Nimeuliza swali la msingi mwendo uwe kilomita ngapi kwa saa?

Kuna ubabaishaji unaokera sana polisi.
 
Back
Top Bottom