Faini kwenye alama za tahadhari barabarani ni wizi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,731
2,000
Pana u umbumbu mkubwa wa alama za barabarani kwa upande wa askari polisi barabarani. Ilikuwa ni vyema serikali ikaliona hili na kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.

Pana yanayoitwa makosa barabarani ambayo yanayotumiwa na polisi kama kisingizio kwa kujua au kutojua. Mwisho wake ukiwa kubambikia watu makosa kiujanja ujanja ili kuwaibia tu. Faini za makosa kama haya kimsingi ni wizi usiokuwa na tofauti na ule wizi wa kutumia nguvu.

Alama za barabarani zimegawanywa katika makundi:

1. Tahadhali
2. Amri
3. Taarifa

Tahadhali zinakuwa ndani ya mabango ya pembetatu. Kundi hili lina lengo la kumtaarifu mtumia barabara kuwa makini na eneo analo pita, hakuna cha zaidi ya hapo.

Alama hizi huwa ziko katika mabango ya pembetatu. Polisi na watumiao barabara wangeelimishwa kuhusiana na hili kuhakikisha haki Ina prevail. Mbivu na mbichi zikafahamika vinginevyo tunakoelekea uvunjifu wa amani utakuwa unatuhusu.

Hivi serikali inajisikia vipi kuwa na polisi wasiotenda haki? Kuwa na polisi wanaotanabaishwa na majambazi?

Alama zinazokuwa enforced na polisi ni za amri pekee ambazo hizi huwa kwenye mabango ya duara.

Polisi kutoza faini ati kuwa kuna alama tu za zebra crossing zisizoambatana na spidi inayoruhusiwa si sahihi. Ikumbukwe kuwa kuna sehemu zenye max speed 50km/h na zebra crossing na zipo zingine kwenye barabara kuu zenye zebra crossing peke yake.

Barabarani kumekaa kama uwanja wa mazoezi kila polisi na lake kinachotakiwa pesa. Chapisheni brosure zenye makosa maonyo, makosa na faini explicitly ili kila mtu azione wazi wazi tuache na ubabaishaji. Vinginevyo kitengo hiki ni shida tu.
IMG_20200227_074314.jpg


Muda muafaka wa kusimama imara kusimamia haki zetu ambazo kwa uzoefu wa njaa za hawa jamaa watabambika kesi hata kwa makosa yasiyokuwapo.
IMG_20200227_074318.jpgIMG_20200227_073519.jpg
IMG_20200227_073519.jpg
IMG_20200227_073519.jpg
 

Attachments

  • File size
    1.2 MB
    Views
    0

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,731
2,000
Uzi Kama huu usokua na mifano Ni wa kuupuuza

Mkuu nimekuta mtiti polisi karibu kuchezea kichapo.

Wamepanga msururu wa magari wakidai vyao kuwa pana kibao cha tahadhari cha waenda miguu ambao hata hivyo hawakuwapo.

Hakuna kibao cha spidi limit wao wana force 50km/h.

Unfairly so.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,555
2,000
Trafic wamekua ni sehemu ya TRA kukusanya mapato, sambamba na DPP. Nchi yetu watu wanaoongoza kwa dhuluma na uhuni ni Trafic Police, hata sheria hawazijui ila wanakaririshwa tu makosa.

Juzi kanikamata Trafic, wakati ananihoji kuhusu lesseni yangu mkononi kwake ameshika simu kafungua App ya kubet mpira (Police anacheza kamari muda wa kazi, saa ngapi atatenda haki anapikamata mtu).
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,206
2,000
Mkuu ngoja nisubscribe kabisa t0pic hii.

Umeichimba mno, tena kiundani sana.

Mimi na udereva wangu wa miaka nendarudi, lakini kuna alama nyingi hapo sijawahi kuziona barabarani na me mwenyewe sizijui, acha kuzielewa.

Ahsante kwa kuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

YonDu Udonta

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
687
500
Mimi Nakereka Wanavyoongoza Magari Sehemu Ya Round About---

Asee Nakereka Sanaa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
885
1,000
Tukubali au tusisitize kwenda mahakamani kusomewa kosa ili kupata usahihi wa maamuzi ya askari wa barabarani, bila hivyo wataendelea tu kutupora fedha na kutubambikia makosa.
 

vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,402
2,000
Mkuu nimekuta mtiti polisi karibu kuchezea kichapo.

Wamepanga msururu wa magari wakidai vyao kuwa pana kibao cha tahadhari cha waenda miguu ambao hata hivyo hawakuwapo.

Hakuna kibao cha spidi limit wao wana force 50km/h.

Unfairly so.

Je palikuwa na makazi ya watu? ni wapi hapo mkuu ili tuchangie bila kuleta maumivu.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,731
2,000
Tukubali au tusisitize kwenda mahakamani kusomewa kosa ili kupata usahihi wa maamuzi ya askari wa barabarani, bila hivyo wataendelea tu kutupora fedha na kutubambikia makosa.

Mkuluro wa alama za tahadhari zipo za kuonyesha:

Kuwepo kwa mteremko mkali, mpando mkali, kuwepo kwa kona kali Julia au kushoto, barabara ya mchepuko mbele kulia au kushoto, nk kunatozwa faini vipi?

Majizi nyie hatukubali tena kuonewa nanyi.

Membe usikatishwe tamaa hawa jamaa wametuudhi wengi. Yanayoweza kubadilika yakatuletea haki tutayakaribisha.

2020 twende na membe.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,731
2,000
Je palikuwa na makazi ya watu? ni wapi hapo mkuu ili tuchangie bila kuleta maumivu.

Makazi ya watu ni moja ya hizo janja janja zao. Wekeni alama za amri - zenye speed limits ndani ya mabango ya duara. Vinginevyo hatulipi faini zenu bambikizi ati kuwa kuna makazi ya watu.

Sehemu ipi ya barabara haina nyuma pembeni? Acheni janja janja zenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom