"Faili halionekani": Wimbo unaotawala mgando wa kutoa haki kwa wakati kwa baadhi ya kesi za rufaa kutoka kwenye mahakama ya kazi Dar es Salaam

mkys

Member
Apr 3, 2012
31
18
Inategemewa na vilevile kutumainiwa sana na kila mwananchi kuiona mahakama kama chombo kitukufu, kinachoaminika na chenye; weledi kiutendaji, chenye maadili, na mfano wa kuigwa kiuwajibikaji panapo hitaji hilo.

Pamoja na kuwa ni muhimili unaojitegemea, yanayoendelea kwa sasa kwa baadhi ya vituo vya utoaji haki yanaalika mahakama isaidiwe kwa namna moja au nyingine.

Inasikitisha sana kama si kutoa kabisa imani ya wananchi kwa mahakama, kusikia baadhi ya wanaotafuta haki kwenye mahakama ya kazi Dar es salaam, kesi zao zikiahirishwa na kurefushwa miezi nenda rudi kwa wimbo uliotajwa hapo juu haswa zinapotakiwa kwenye rufaa mahakama kuu.

Je, hizi faili zinaota miguu au mabawa na hivyo zitoroke zilikohifadhiwa?
Kama si hivyo, kuna nini kiutendaji kinachohitaji msaada?

Waziri muhusika tukuombe sana ulifanyie kazi hili swala. Ni kero iliyokithiri kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom