Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,174
107,701
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Update 1:
Tafadhalini tuulize maswali kiheshima . Heshima ni kitu cha bure na hii JF yetu pendwa inasomwa na wengi, tujiheshimu.

Update 2:
Siku kadhaa zimepita toka tuanzishe uzi huu na nimesikitishwa na aina ya maswali yanayoulizwa kwenye huu uzi.

Tumetowa fursa ya kuulizana na kila niwezapo kujibu au kutafuta majibu muafaka kutokana na hayo maswali na fursa ya wachangiaji kujibu maswali yatakayojitokeza ya "general knowledge" lakini hadi hii leo ni maswali machache sana yenye faida kwa wengi yameulizwa. Maswali yaliyojaa ni amma ya kutaka kuanzisha ubishi "ligi" na amma yamelenga mtu binafsi, hususan amelengwa mleta mada. Ni masikitiko makubwa sana.

Nnawashauri wote waliouliza maswali yenye kulenga binafsi na wale waliouliza maswali yenye kubomoa badala ya kujenga wabadilike na waanze kuuliza maswali yenye kujenga, kuelimisha, kutujaza hekima na maarifa.

Nilipoweka aina ya elimu niliyoisomea nilidhani ntakumbana na kibano kikali kuhusu hilo na nijibu ili iwe faida kwa wengi lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna hata mmoja aliyeuliza swali lolote kuhusu hilo.

Isitoshe, mna fursa ya kuuliza kuhusu chochote. Ndege, mimea, dunia, sayari, nyota, maajabu, maswali yasiyokuwa na majibu, viumbe kwa ujumla vinavyojulikana na visivyojulikana, maajabu ya duniani, elimu na vitu vingi kama hivyo na vinginevyo.

Nnauhakika wale walioleta maswali ya kiajabu ajabu ya ubishi wana mengi sana ya kuuliza yanayoweza kuwapa faida wengi na kuna wengi kati yao wana mengi wanayajuwa na wanaweza kuchangia kwenye majibu kwa faida ya wengi.

Ombi langu kwa wote ni tuboreshe aina ya maswali na majibu.

Karibuni.
 
je, ni kweli dini ya kiislamu ina mafungamano na makundi / matukio ya kigaidi?

Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:


Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
 
103 Reactions
Reply
Back
Top Bottom