Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Hata kama hakutatokea Vyama vya Upinzani vikashinda lakini kutakuwa na faida kubwa sana kati ya hawa wawili wakipewa kipaumbele cha kugombea Urais hapa nchini. Kwangu mimi wote wakigombea ni sawa au hata mmoja kati ya hao ni sawa. Ukiacha hao hata Zitto Kabwe pia inagwa sijamtaja ila ana uwezo mkubwa sana wa kuleta uimara kwa kambi ya upinzani iwapo hao wawili wanakuwa hawajapewa nafasi.
Tundu Lissu
Huyu anaogopwa sana na CCM na inavyoonesha CCM wanatarajia kutumia dola kumdhibiti na wala hawajiandai kupingana naye kwa maneno au sera. Kwa jinsi Tundu Lissu alivyo na ushawishi na avyojua kuchambua yale ambayao hata CCM wanafikiria ni wameyafanya vizuri Tundu Lissu anaweza akayabadilisha yakaonekana ni mabaya. Mfano mdogo Tundu Lissu aliwahi kuongea kuwa ile taarifa ya makinikia ilikuwa ni taka taka. CCM wana evidence kuwa lile sakata la makinikia limewaletea ushindi upande wao. Tundu Lissu hapa anaweza kuweka msisitizo kuwa ile taarifa kweli ilikuwa ni takataka kwa sababu kiasi kile cha fedha ambazo baada ya makinikia yale kupimwa ilionekana zilikuwa ni trilioni nyingi sana za KiTanzania. Ikasemekeana hata kila MTanzania angenufaika kwa gari aina ya Noar iwapo zingegawanywa kwa WaTanzania wote. Sasa Tundu Lissu alivyo mjuvi wa kuchambua ataweza kuitofautisha vizuri ile taarifa ya makinikia na kilichofanyika. Wakati akifanya hivyo hataacha kuchombeza yae maneno yake ya kejeli ambayo WaTanzania wengi tunayapenda na kuyashangilia. Kwa hili pengine CCM walipaswa warekesbishe kwanza ile taarifa yao ya Makinikia na waseme makosa yalifanyika na figure halisi ni ya sasa ambayo wanategemea kulipwa bilion zaidi ya 700 na tayari bilioni kadhaa zimeshalipwa. Kwa kweli iwapo atakuja Tundu Lissu hoja hii CCM watapigwa nayo kwani wananchi hawajapata majibu ni kwa nini hawajapata noah zao.
Kuna hoja zingine nyingi ambazo zitanogesha kampeni kwa upande wa Tundu Lissu ikiwepo ubinywaji wa demokrasia, ukatili na atatoa pia ushuhuda kidogo wa shambulio lake ambalo pia litavuta huruma kubwa sana kwa wananchi, bahati mbaya Mwenyekiti wa CCM wala Chama chake hawajawahi kutoa hata kemeo tu kwa kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu na wanategemea ubabe wa Polisi labda kumzuia asiongelee jambo ambalo bado wanapeleleza.
Kosa kubwa litakalofanywa na CCM ni maneno ambayo yanawatoka ya kutaka Tundu Lissu akifika akamatwe. Hii ni mbaya sana kwani itauza kwa nguvu hoja za Kampeni kwa upande wa upinzani na inaweza hata ikasababisha kupinduliwa kwa meza au kuleta vurugu. Uchaguzi wa URais na ubunge sio sawa na Serikali za Mitaa ambao wahusika walikuwa ni wananchi wa mtaa huo huo na walikuwa wakifahamiana. Hapa kumbuka hata kampeni za udiwani tu, kabla ya ubunge na URais, zitahusisha vijiji na vijiji au mtaa na mtaa na hapo kutokuoneana hiyana au aibu hakupo kwa sababu watu hawajuani kama ilivyokuwa Serikali za Mitaa. PATACHIMBIKA KWELI KWELI.
Faida za kumsimamisha Tundu itakuwa:
- Watu watakuwa na hisia kali kwa kuamni Mwenyezi Mungu kamponya Tundu Lissu ili aje kuwa Rais na atapata kura kwa kigezo hicho;
- Tundu Lissu atakuwa chanzo cha harakati za wananchi wa WaTanzania kutambua haki zao za Kikatiba na Kijamii na kijamii na hivyo atapandisha sana upinzani na mwisho wa siku haki ya kutofautiana kimawazo itaonekana ni kitu cha kawaida tu nchini mwetu.
- Tundu Lissu ataongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni na hata kulifanya bunge lijalo kuwa zuri zaidi.
- Tundu Lissu atavutia sana kwenye siasa za kimataifa na kwa kuanzia tu kuerejea kwake nchini itakuwa ni stori kubwa sana.
Bernard Membe
Kwa kweli huyu katika kuelezea mambo anamzidi sana Rais wa sasa. Yupo calm na hana pra -pra -pra . CCM wengi zaidi (wanachama na washabiki) ya asilimia 27 (kwa mujibu wa utafiti wangu mwenyewe nikiwa kama MCCM pia) wanamkubali. Huyu pamoja na kuonekana anapingana na utawala wa sasa lakini utawala umeonesha hali ya kumjenga awe hivyo. Kilichopaswa na utawala ni kummeza ndani kwa nadni - kwa mafano kutangaza hadharani kumpa Ubalozi au nafasi ingine yeyote. Angekataa yeye hapo ingeonakena ana matatizo lakini utawla wenyewe umekuwa ukimkataa bila sababu yeyote na kumfanya yeye sasa awe anajibu mapigo. Majibu yake kweli yana maumivu sana kwa utawala.
Kampeni za Membe kuwania URais zitakuwa tamu sana kwa sababu anawafahamu vema wanaCCM na mpaka hapo alipo kila siku anapata taarifa za ndani kutoka upande huo. Wala sio habari za kuhisi ni kweli Membe ana watu wa system, ambao wenyewe wapo kwa maslahi ya Taifa na sio maslahi ya CCM. Watu wengi hawaelewi maana ya Uslama wa Taifa but wahusika wenyewe wanaelewa. Huko pia watu wamegawanyika na wapo wa kutosha tu wanaomuunga mkono Membe. kwa ujumla Membe anakubalika kwa asilimia 27 na WanaCCM na hivyo kazi yake ambayo sio kubwa sana kushawishi kama asilimia 23 ya wapiga kura wote. Faida kwa Membe kugombea:
- Ataonesha vijana kuacha woga wa kukosa ujasiri wa kutumia haki ya kuwania nafasi.
- Ataonesha CCM ni munguMtu tu na wala sio Mungu kwa maana hiyo mtu yeyote hata Magu mwenyewe anaweza kahama na akagombea kupitia upiznani.
- Ataonesha kuwa kumbe Rais anakosolewa tu.
- Ataonesha ugumu wa maisha ya wananchi wa kawaida ikiwepo vitendo vya kuitangaza Nchi kuwa inakuwa kiuchumi wakati ukweli ni hamna kabisa - atagusia pia mambo ya Benki ya Dunia yaliyoibadili TZ kuwa kwenye nchi ya kipato cha chini cha kati yana maana gani kwetu wananchi wa kawaida.
-Atauchana chana uongozi wa CCM na kuwafanya wale wanachama wa kawaida kuchukua maamuzi ya kukihama, n.k
- Membe pia ana uwezo mkubwa wa kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bugeni kwani ni lazima wapo wagombea ambao wamejiandaa wakikatwa CCM wahamie upinzani.
- Membe kama Tundu Lissu watavutia sana kwenye medani ya siasa za Kimataifa.