Faida zitakazojitokeza kama mafisadi wakiwekeza ndani ya nchi yetu..

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,974
5,215
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kwanini kundi linaloitwa mafisadi wakishafisadi wanaficha hela nje ya mipaka ya Tanzania. Watu hawa wanasababisha hali ya uchumi wetu kuzidi kudorora na kufanya maisha ya Mtanzania yazidi kuwa magumu kupita kiasi.

Kama kundi hili linaloitwa mafisadi litaamua kuwekeza ndani ya mipaka ya Tanzania faida zifuatazo zinaweza kujitokeza;
1. Kama wakifungua vitega uchumi Tanzania kama viwanda, uchimbaji madini, kilimo n.k. itasaidia kutoa ajira kwa Watanzania wengi ambao hawana ajira.

2. Wakiwekeza kwa kufungua mashamba makubwa ya kilimo cha umwagiliaji, chakula kitakuwepo kwa wingi ndani ya nchi na itakuwa rahisi kuwa na reserve kubwa ya chakula so matatizo ya kukabiliwa na uhaba wa chakula ndani ya nchi utapunguwa au kuisha kabisa.
3. Kama watakuwa na mtazamo chanya wa kuwa waaminifu na kulipa kodi kihalali kama inavyotakiwa, serikali itaweza kujikusanyia mapato mazuri kutoka kwenye uwekezeji wao na hivyo kuboresha huduma za jamii kama hospitali, barabara, usambazaji wa maji salama mijini na vijijini, utoaji wa elimu bora na bure primary to university n.k.
4. Pia kama watazihifadhi fedha hizo kwenye Benki zetu hapa Tanzania kama NMB, CRDB, AKIBA COMMERCIAL BANK,n.k. bank zitakuwa na hela ya kutosha kukopesha Watanzania wengi zaidi na hivyo kuwasaidia wajasiriamali wengi ambao wanapata shida ya kuendeleza biashara zao kutokana kukosa mitaji ya kutosha.
5. Wakiwekeza kwenye rasimali zetu kama madini itasaidia angalau faida kubwa inayopatikana kutokana na rasilimali hii kubakia ndani ya nchi yetu tofauti na inavyotokea sasa hivi wageni wanavyovuna na kuondoka na kila kitu kurejea kwao na kutuacha mikono mitupu.
So, mtazamo wangu ni kwamba kama wewe ni fisadi na umeshatuibia usizidi kutukasirisha kwa kukimbiza hela yetu nje ya nchi, fikiria kuwekeza ndani ya nchi yetu basi angalau tufaidi kidogo matunda ya kodi yetu.
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
tatizo tungewekeza hapa nchini ila majungu yenu ndo yanatufanya tuwekeze nje!
nchi masikini halafu nionekane tajili peke yangu si mtanivamia na mapanga nyumbani!
 

AMINATA 9

JF-Expert Member
Aug 6, 2011
2,120
640
niwekeze ndani ya nchi niulizwe nimezitoa wapi bora nje huulizwi labda uvunje record ya uwekezaji huko nje kuliko wenye nchi hiyo tena ndio utaulizwa
 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,974
5,215
tatizo tungewekeza hapa nchini ila majungu yenu ndo yanatufanya tuwekeze nje!
nchi masikini halafu nionekane tajili peke yangu si mtanivamia na mapanga nyumbani!

Kama unajua sio halali kuwa na utajiri usio halali kwa nini ujilimbikizie utajiri haramu?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom