Faida zipatikanazo kwa kunywa limau kiafya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
FADA YA KUNYWA JUISI YA LIMAO.jpg



FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUNYWA LIMAU KIAFYA



Faida za limau au ndimu zinajumuisha matumizi kama tiba kwa ajili ya vidonda vya kooni, matatizo katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya meno, homa, kuvuja damu ndani ya mwili, baridi yabisi, kutibu malengelenge, uzito kupita kiasi, matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kipindupindu na shinikizo la juu la damu. Pia ni dawa nzuri kwa ajili ya nywele na ngozi.



Tangu karne nyingi limau linajulikana kama dawa, husaidia pia kuongeza kinga ya mwili, kusafisha tumbo na hujulikana pia kwa kazi yake nzuri ya kusafisha damu.



Juisi ya limau ina faida kadhaa nyingi kama vile kuondoa mchanga katika figo, kupunguza kukamaa kwa mishipa (strokes) na kupunguza joto la mwili. Kama kinywaji ambacho huondoa uchovu mwilini, juisi ya limau itakusaidia kubaki mtulivu na mpole.

Faida nyingi za limau zinatokana na virutubishi vyake vingi mhimu kwa mwili kama vile vitamini C, vitamini B6, vitamini A, vitamini E, folate, niacin thiamin, riboflavin, pantothenic acid, shaba, kalsiamu, chuma, magnesium, potassium, zinki, phosphorus na protini.



Limau ni matunda ambayo yana kitu mhimu sana katika kuondoa sumu mwilini kiitwacho kwa kitaalamu kama “flavonoids” ambacho chenyewe ni mhimu sana katika kupigana na kansa mbalimbali mwilini.



Limau husaidia pia kuzuia matatizo ya kisukari, kufunga choo, shinikizo la juu la damu, homa, husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri na matatizo mengine mengi yakiwemo kuimarisha ngozi ya mwili, nywele na meno.

Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari wa magonjwa ya mfumo wa mkojo cha Marekani (American Urological Association) unaonyesha kuwa juisi ya limau au ‘lemonade’ inaweza kuondoa au kuzuia kujitokeza kwa mawe kwenye figo.



Watu hutumia limau kutengeneza juisi ya limau maarufu kama “lemonade” kwa kuchanganya pamoja maji maji ya limau vikombe viwili, maji ya moto kikombe kimoja, maji ya kawaida lita 3 na asali au hata sukari ya kawaida ml/gm 500 ili kupata juisi ya limau (lemonade) ya ujazo wa lita 5.

Watu wengi pia hutumia limau katika kusafisha au kuosha vyombo sababu ya uwezo wa kuondoa madoa, mafuta na uchafu mwingine kirahisi zaidi.



Marashi au harufu ya limau hufukuza mbu, wakati huo huo kuinywa juisi ya limau iliyoongezwa mafuta ya zeituni husaidia kuondoa mchanga katika kibofu cha mkojo. Limau inajulikana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi na hutumika kwa namna nyingi tofauti.

Zifuatazo ni faida mbalimbali za limau mwilini:



1. Kufunga choo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula


Juisi ya limau husaidia kutibu matatizo yahusianayo na tumbo kushindwa kumeng’enya chakula na kufunga choo. Ongeza matone machache ya limau kwenye chakula chako (kuwa makini sababu limau huwa haipatani na maziwa), na itakusaidia katika kumeng’enya chakula.

Limau hufanya kazi kama wakala msafisha damu na mwili kwa ujumla. Na hii ni nzuri kama unapata juisi yako ya limau baada ya chakula cha mchana au cha



usiku. Juisi ya limau inatengenezwa kwa kuchanganya maji ya limau, maji kidogo, chumvi ya mawe kidogo na asali au hata sukari. Weka na barafu kidogo pembeni.

Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.



2. Hutibu homa

Juisi ya limau inaweza kumtibu mtu anayesumbuliwa na homa, mafua au baridi. Limau husaidia kutibu homa kutokana na sifa yake ya kuongeza kiasi cha jasho mwilini.



3. Huongeza afya ya meno

Juisi ya limau mara nyingi imetumika katika kulinda afya ya meno. Kama juisi fresh ya limau itanyunyizwa juu ya jino linalouma inaweza kusaidia kuondoa maumivu. Kusugua (masaji) juisi ya limau juu ya fizi za meno kunaweza kusaidia watu wenye matatizo ya kutokwa damu kwenye fizi huku ikiondoa harufu mbaya katika fizi na mdomo kwa ujumla.

Unaweza kupata faida hizi kama utakuwa unapiga mswaki ukitumia dawa yenye limau ndani yake (lemon tooth paste).

4. Hutunza nywele

Juisi ya limau imejidhihirisha yenyewe kuwa dawa nzuri kwa upande wa matatizo mbalimbali ya nywele. Juisi ya limau ikipakwa kwenye ngozi ya kichwa inaweza kutibu matatizo kama ya mba, kupotea au kukatika kwa nywele, na matatizo mengine yahusuyo nywele na ngozi ya kichwa.

Kama utakuwa ukisafisha nywele zako kwa kutumia juisi au maji ya limau moja kwa moja basi utazifanya nywele zako zipate mng’aro wake wa asili bila gharama yoyote ya ziada.

5. Hulinda ngozi

Kwakuwa Juisi ya limau ni dawa ya asili dhidi ya bakteria, inaweza pia kutibu matatizo mbalimbali ya ngozi. Juisi ya limau inaweza kutumika kupunguza maumivu kwenye ngozi sababu ya kuungua na jua, pia husaidia kupunguza maumivu kutokana na kung’atwa na nyuki. Juisi ya limau au majimaji ya limau yanaweza kutumika kupakaa juu ya ngozi na kutibu chunusi na ukurutu.

Limau pia hutumika kama dawa ya kukufanya usionekane mzee kwakuwa yenyewe huondoa mikunjo na madoadoa ya ngozi.

Kunywa maji ya limau yaliyochanganywa na asali kunasaidia ngozi kuwa na afya zaidi na hata ukipekuwa huko sokoni utazipata baadhi ya sabuni ambazo zimetengenezwa kutokana na limau.



6. Hutibu majeraha ya moto

Upakaji wa maji ya limau (juisi) kwenye eneo la ngozi lililoungua huweza kusaidia makovu kupotea na hii husaidia pia kwa mtu aliyepatwa na malengelenge au vipele vyenye maji maji yanayouma ndani. Na kwa sababu limau ni wakala wa kupooza au wakala mtulizaji (cooling agent), huweza kupunguza maumivu au kuhisi kuungua kwenye ngozi hasa wakati unakuwa na majeraha yanayounguza ngozi.



7. Huzuia kuvujika kwa damu

Limau inayo sifa ya kudhibiti bakteria mwilini (antiseptic properties) na kugandisha damu, sifa hizi au kazi hizi mbili za limau husaidia kusimamisha kuvuja kwa damu ndani ya mwili. Unaweza kutumia maji ya limau ukiweka kwenye kipande cha pamba na kuiweke puani kuzuia pua kuvuja damu.



8. Hupunguza Uzito

Ikiwa utakunywa juisi ya limau iliyochanganywa na asali na maji ya uvuguuvugu, hasa asubuhi tu unapoamka inaweza kusaidia kupunguza uzito.



9. Hutibu matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji

Juisi ya limau husaidia katika kutuliza matatizo katika mfumo wa upumuwaji kama vile pumu. Kwakuwa limau ina kiasi kingi cha vitamini C, husaidia kutibu na kutuliza matatizo ya muda mrefu kwenye mfumo wa upumuwaji.



10. Kipindupindu

Magonjwa kama kipindupindu na malaria yanaweza kutibika kwa kutumia juisi ya limau tu kwa sababu limau hufanya kazi ya kusafisha damu na mwili kwa ujumla.



11. Hutuliza maumivu ya miguu

Limau huwa na harufu ya kuvutia (aromatic) na pia inayo sifa ya kudhibiti bakteria na hutumika kutuliza maumivu au miguu kuwaka moto. Ongeza juisi (maji ya limau) kwenye dishi lenye maji ya moto kidogo na utumbukize miguu kwa dakika kadhaa kwa kuondoa haraka maumivu ya miguu na utajisikia umepata tulizo fulani (relaxed).



12. Baridi Yabisi

Limau au ndimu pia ni kikojoshi, yaani ni kitu kinachosisimua uzalishwaji wa mkojo na kwa sababu hiyo inaweza kutibu baridi yabisi na maumivu ya kwenye mishipa. Husaidia kutoa nje bakteria wabaya na sumu mbalimbali mwilini.



13. Hutibu malengelenge (Corns)

Juisi ya limau inaweza kusaidia kukausha malengelenge au vipele ambavyo huwa na majimaji ambavyo hujitokeza mara nyingi chini ya unyayo au katikati ya vidole vya mikono. Kunywa juisi ya limau na maji ndani yake husaidia wagonjwa kupunguza mawe kwenye nyongo.



14. Hutibu maambukizi ya kwenye koo

Limau ni tunda bora kabisa ambalo hupigana dhidi ya matatizo yanayohusiana na maambukizi kooni sababu ya sifa yake kubwa ya kudhibiti bakteria mwilini.



15. Hutibu shinikizo la juu la damu

Kunywa juisi ya limau kuna msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo ya moyo kwa sababu limau lina kiasi cha kutosha cha potasiamu.

Limau hudhibiti shinikizo la juu la damu, kizunguzungu, na uchovu sugu kwa sababu yenyewe limau hutoa hisia za utulivu kwa mwili na roho pia.



1585677637542.png
juisi ya limau.jpg



Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +44-7459-370-172 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
Last edited:
Back
Top Bottom