Faida za upimaji na usajiri wa ardhi/viwanja

Gis expert

Member
Jan 11, 2014
28
6
Habarini wana JF,

Napenda kumshukuru mungu kwa kunipatia uzima mpaka wakati huu ambao nimeamua kukaa na kuandika machache yanayohusu suala la faida za upimaji na usajiri wa ardhi au viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo kama yale ya ufugaji, kilimo, makazi na biashara.

Kwa ujumla upimaji huu unafanyika kwa ajili ya kuhakikisha haki ya mmiliki wa ardhi husika inatambulika kisheria kwa kuangalia mipaka inayozunguka ardhi hiyo au kiwanja chake.

Leo nitasema machache juu ya faida za upimaji na usajiri wa ardhi. upimaji wa ardhi huwa unalenga mambo haya muhimu kwanza ni utambuzi kisheria kwa mmiliki husika wa ardhi hiyo, kuongeza thamani ya ardhi, kuongeza usalama katika kumiliki ardhi hiyo, pia kwa kiwanja ambacho kimepimwa mmiliki wake anaweza kutumia hatimiliki ya kiwanja katika uombaji wa mkopo benki au katika taasisi yeyote ya fedha hapa nchini.

Hivyo napenda kusema kwamba tupime ardhi tulizonazo kwa usalama na maendeleo yetu. kwa atakaye hitaji huduma hii ya upimaji basi naomba afanye consultation kwa kuniPM.
 
Mampaka ya ardhi na mipango miji imekaimu pia upimaji wa ardhi kwa watu binafsi wenye ujuzi huo?

Nini gharama za upimani huo kwa mchanganuo wastani wa ekari moja ni bei gani.

Jaribu kuleta ufafanuzi kidogo, hayo mambo ya kuvutiana pembeni siku hizi hayana tina wala kukuletea wateja wazuri, enzi za utandawazi jiamin na kuweka mambo yako kwa uwazi hapa mimi nitakuwa mmoja wa wateja wako, ila huko unakotuitia pembeni Mmmm hapana, hapa tulipo kwa uwazi panatosha.
 
huyo ameshajishtukia kuwa ana dili bora angetoa somo tukaelewa
sasa watu tunamtaka hapa hewani atupe bei ya uipimaji kiwanja
yeye kasepa kiaina ndo mambo ya mijini hayo
 
Ngoja nimsaidie hapa, ninavyoelewa ni kweli serikali imewapa vibali baadhi vya kupima na kuuza maeneo mfano kitopeni. kiromo ila nadhani ni makampuni yaliyosajiliwa. Lakini kama ilivyo kwa kusajili kampuni au jina kwa Brela, vivyo kwa kupima ardhi na kutafuta hati zake wapo hawa wataalam wasiosajiliwa wanawapimia watu na kwa vile anakuwa na muda anafuatilia na vileviel ni fani yao kule anakuwa na watu wake maalum. Cha muhimu ni awe walau na kazi alizokwisha fanya tujue pia malipo yake na labda ofisi au uthamini. Ni sawa na kusema uache shughuli zako ufatilie sijui Brela, Tin number na vitu kama hivyo.
 
habarini wana jf, kwanza nataka kusema kwamba tuache kutoa hukumu bila kujua jambo ambalo linalomsibu muhusika,tuwe tunafikiria chanya lakini pia naomba radhi kwa kuwa mmekuwa na shahuku ya kutaka kujua bei ya upimaji hivyo basi nalifanyia kazi suala la kuweka wazi gharama zote za upimaji na usajiri wa ardhi.
 
Halafu kuwa sharp mnaweka tangazo mnapotea, taja location uko wapi huduma unafika mikoa yote au? bei kwa vigezo gani walau kiwango cha chini na cha juu. Weka info zote muhimu ndio upotee.
habarini wana jf, kwanza nataka kusema kwamba tuache kutoa hukumu bila kujua jambo ambalo linalomsibu muhusika,tuwe tunafikiria chanya lakini pia naomba radhi kwa kuwa mmekuwa na shahuku ya kutaka kujua bei ya upimaji hivyo basi nalifanyia kazi suala la kuweka wazi gharama zote za upimaji na usajiri wa ardhi.
 
habarini wana jf, kwanza nataka kusema kwamba tuache kutoa hukumu bila kujua jambo ambalo linalomsibu muhusika,tuwe tunafikiria chanya lakini pia naomba radhi kwa kuwa mmekuwa na shahuku ya kutaka kujua bei ya upimaji hivyo basi nalifanyia kazi suala la kuweka wazi gharama zote za upimaji na usajiri wa ardhi.

Unalifanyia kazi?!!!! Duh!! Kumbe hujajipanga?!! Usijekuwa mtu wa kati
 
GHARAMA ZA KUPIMAADRHI KWA PLOT MOJA
INFORMATION FORSURVEY WORK:
Visiting site: Tsh.150, 000/=
Hiring tools: Tsh.300, 000/= per day
Surveyor charge: Tsh. 500, 000/=
Labor charge: Tsh.100, 000/=
Beacon Tsh.10, 000/= @1
Data + cartographic materials: Tsh.100, 000/=
Transport: Tsh.100, 000/= but it depend on the distance tobe travelled to sites
SUB TOTAL: Tsh.1, 300,000/=. Total hii imepigwa Kwa beacons tano lakini minimum beacons ni nne.
OFFICE WORK:
Licensed surveyor fee: Tsh.100, 000/=
Survey instruction: Tsh.100, 000/=
File compilation: Tsh.100, 000/=
Land officer: 50,000/=
Survey check two: Tsh.50, 000/=
Submission fee: Tsh.20, 000/=
Survey approval: Tsh.100, 000/=
GRAND TOTAL: Tsh.1, 820,000/=
Hivyo basi kwa tathimini hiyo gharama halisi inaweza rangekuanzia Tsh.1, 000,000- Tsh.2, 000, 000 kutegemeana na ugumu wa kazi na mahali site ilipo,kuhusugharama za kupima mashamba mara nyingi huwa tathimini yake inafanyika baada yamtaalamu kuangalia site ilivyo lakini kwa kawaida kwa ekari moja huwainagharimu kiasi kinachoanzia laki 700, 000 mpaka 1,000,000 kutegemeana namakubaliano ya mteja na mtaalamu baada ya utasmini wa gharama husika kufanyika.
Hiyo nimetoa kama roughly coast wana jf,kwamaelezo Zaidi napatikana kwa namba 0714238436
 
nimeanisha gharama za kupima kwa plot moja lakini pia hata ukiwa mkoani huduma hii inapatikana kwa wale surveyors ambao wako huko mikoani lakini kama utahitaji huduma kutoka kwangu ni chaguo lako.
 
GHARAMA ZA KUPIMAADRHI KWA PLOT MOJA
INFORMATION FORSURVEY WORK:
Visiting site: Tsh.150, 000/=
Hiring tools: Tsh.300, 000/= per day
Surveyor charge: Tsh. 500, 000/=
Labor charge: Tsh.100, 000/=
Beacon Tsh.10, 000/= @1
Data + cartographic materials: Tsh.100, 000/=
Transport: Tsh.100, 000/= but it depend on the distance tobe travelled to sites
SUB TOTAL: Tsh.1, 300,000/=. Total hii imepigwa Kwa beacons tano lakini minimum beacons ni nne.
OFFICE WORK:
Licensed surveyor fee: Tsh.100, 000/=
Survey instruction: Tsh.100, 000/=
File compilation: Tsh.100, 000/=
Land officer: 50,000/=
Survey check two: Tsh.50, 000/=
Submission fee: Tsh.20, 000/=
Survey approval: Tsh.100, 000/=
GRAND TOTAL: Tsh.1, 820,000/=
Hivyo basi kwa tathimini hiyo gharama halisi inaweza rangekuanzia Tsh.1, 000,000- Tsh.2, 000, 000 kutegemeana na ugumu wa kazi na mahali site ilipo,kuhusugharama za kupima mashamba mara nyingi huwa tathimini yake inafanyika baada yamtaalamu kuangalia site ilivyo lakini kwa kawaida kwa ekari moja huwainagharimu kiasi kinachoanzia laki 700, 000 mpaka 1,000,000 kutegemeana namakubaliano ya mteja na mtaalamu baada ya utasmini wa gharama husika kufanyika.
Hiyo nimetoa kama roughly coast wana jf,kwamaelezo Zaidi napatikana kwa namba 0714238436
Haitegemei ukubwa wa eneo?
Kuhusu upimaji wa shamba, mpka mwenyekiti au mtendaji awepo? ... maana huwa wanakimbia hawa jamaa na hawapendi watu wapime mashamba. Shamba lisilo pimwa ni dili kwao.
Mwisho, process nzima mpaka nipate hati inachukua muda gani?
 
hapo nimeanisha gharama za kupima plot moja tu ambayo ipo katika standard za mgawanyiko wa aina ya viwanja lakini kwa ukubwa za hapo basi pia huwa kuna gharama zake tofauti na hizo kutegemeana utasmini wa gharama. kuhusu kupima mashamba ni lazima uhakikishe unapata kibali au uthibitisho kutoka kwenye serikali ya kijiji husika na kuhusu upatikanaji wa hati huwa hakuna muda maalumu uliowekwa isipokuwa inategemeana na ukubwa wa kazi na foleni za watu wanaofuatilia hati wizarani. nafikri nimekujibu maswali yako?
 
YES!
Najua kupima mwenyewe na nina ramani zangu na coordinates zake na ku-verify google earth .... je wewe kama mtu uliyesajiliwa, unafanya verification na kuondoa gharama nyingine? ... ninayo hadi topographic map ya mashamba kwa sababu tu niliwahi kuchukua GIS kidogo. Ila hazijahakikiwa, unaweza fanya uhakiki? ... for a cheaper price since I did most of the $hit by myself?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom