Faida za Malumbano ya kidini.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,332
Siku za karibuni jamvini kumekuwa na malumbano ya kidini yasiyo na idadi.
Je nini faida ya malumbano haya?
Mi naona hamna mafundisho yeyote isipokuwa ni kukashifiana na kubezana.
 
Siku za karibuni jamvini kumekuwa na malumbano ya kidini yasiyo na idadi.
Je nini faida ya malumbano haya?
Mi naona hamna mafundisho yeyote isipokuwa ni kukashifiana na kubezana.

Mambo ya siasa, mapenzi, elimu, hoja mchanganyiko, sheria, nk kwako si malumbano ila kukija kwenye masuala ya dini ndio kuna malumbano?
 
Tena hii hoja inaweza kuendeleza malumbano hayo, huwa inaanza taratibu halafu ikiendelea huwa inabadilika topic na kuwa Dini A vs Dini B plus the neutrals. So far so good, harm reported hakuna ubaya hapo ila hoja ni kuwa point ziwe zinatolewa kwa lugha yenye busara. Ukitaka kujua no harm, opponents hawa ktk thread zingine zenye joint concern huwa wanaungana na kuchangia bila ya kuhusisha imanni zao.
 
Mambo ya siasa, mapenzi, elimu, hoja mchanganyiko, sheria, nk kwako si malumbano ila kukija kwenye masuala ya dini ndio kuna malumbano?

Jambo la kujadili hapa ni faida ya mijadala la dini, Je toka maada za dini zimeanza kujadiliwa katika forum hii kuna faida tumepata? Hakuna cha maana zaidi ya kuona wale wanaovutwa na fikra za kijinga wakitoa kashfa kwa dini nyingine.
 
Inabidi mzoea kulumbana kama huwezi malumbano inaonyesha kwamba una ka-element ya udicteta kwenye moyo wako..so jiangalie mwenyewe kama huwezi kuhimili kulumbana kaa kimya ..

Kwangu mimi malumbano ni sehemu ya kuchangamsha brain yangu na kutafuta maarifa zaidi kwa yale ambayo yanatokea

Faida kwasasa si kubwa kwasababu watu wengi hawajui maana ya malumbano wanatukanana lakini ikiendelea muda mrefu watazoea na kujadiliana kwa heshima na kwa faida..

Nachoona mimi ni stages za malumbano..tuko stage one mpaka sasa emotions ndio zinatawala badala ya watu kuwa irrational..time will tell though!
 
Labda hoja nyingine ni kuwa threads hizo zimekuwa ni nyingi kwa sasa. Hata mtu ukianzisha ambayo haina uhusiano au nia hiyo basi wachangiaji wataipeleka huko. Kwa mfano ktk jukwaa habari za kimataifa kuna habari ya Jamadari ya tar 18 Feb 2010 isemayo "Marekani yatuhumiwa kuchochea vita" lakini hebu kaangalie thread za mwisho je zinaendana na topic? Zaidi ni kustick na title ya mtoa hoja
 
Malumbano ya kiimani yana msingi gani na wakati tayari tunasema ni "Imani?" Imani ni bayana ya mambo yasiyoonekana,sasa mambo ambayo hayaonekani manabishania si mtakuwa hamnazo jamani?
Sijui ni kivipi tunaweza kuwa na ustaarabu kwenye mijadala yenye muelekeo wa malumbano ya kidini na hivi ukichukulia ukweli kwamba you cant teach an old dog new tricks.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom