Faida za kuwepo taifa la Israel!

Jayfee

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
309
1,038
Na Mwalimu Mwakasege:-
FAIDA YA KUWEPO KWA TAIFA LA ISRAEL KWA MKRISTO.

Amosi 9 :14 - 15
14 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake.15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako

Yoel 1:7
Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe
Kuna tofauti kati ya Taifa la Israel na uzao wa Israel.

Uzao wa Israel ni watoto wa Yakobo na wajukuu zake.
Taifa la Israel linaanzia pale walipotoka Misri wakiwa na Musa kuelekea Kanani.
Katika taifa la Israel kuna watu wa uzao wa Yakobo na wengine ambao sio uzao wa Israel (Yakobo).

Katika Amos inazungumzia habari za taifa Israel na uzao wa Yakobo yaani wote kwa pamoja (walio wa uzao na wasio wa uzao wa Yakobo).

Mungu anasema atawapanda ina maana kuwasimika maana yake hawatang'olewa tena. Hiki ni kipindi kingine hata wakimkosea Mungu hawatang'olewa tena (maana zamani zile walikuwa wakikosea Mungu alikuwa anawatoa katika taifa na kuwapeka mahali pengine utumwani au kuleta mtawala kuwatawala)

Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

MATHAYO. 24:1 - 2 , 32 - 42.
Katika mlima wa mzeituni wanafunzi walimuuliza Yesu maswali kama matatu unahitaji kufuatilia kwa ukaribu kabisa. Maswali haya na ndiyo yanayojibiwa kuanzia Mathayo 24: 32 hadi sura ya 25 ya Kitabu cha mathayo

Maswali waliyouliza ni haya.
Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema,
1. Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini?
2. Nayo ni nini dalili ya kuja kwako,
3. Na ya mwisho wa dunia?
Sawa sawa na Mathayo. 24:3
Maswali haya Yesu kayajibu vizuri kabisa. Naomba tutazame mambo haya kwa sehemu
Suala la kuja kwa Yesu mara ya pili na mwisho wa dunia ni vitu viwili tofauti kidogo.

Yesu atakuja mara ya pili kuchukua watu wake (tutamlaki mawinguni)
Pia Yesu kuja tena kutawala kwa miaka 1000 kwa kupitia Israel kuja mlima wa mizeituni.

Kuna mwisho wa dunia yaani Yesu kuja kuhumu dunia.
Mfano akisema kila jicho litamuona. Hamaanishi kuja kuchukua kanisa maana si kila mtu ataona. Ila wale wachache watakaoenda kumlaki mawinguni.

Siku ya Yesu kuchukua kanisa atakuja kama mwizi si kila mtu atamwona.
Kwa mtini jifunzeni mfano anazungumzia kipindi hicho taifa la Israel likiwa katika nchi yake yaani kutimizwa kwa mistari niliyokuonesha pale juu.

Sasa huu mstari wa kwa mtini jifunzeni mfano unaanza kuutazama kuanzia May 14 1948
Kwa hiyo tunatakija kujifunza kitu kutoka kwa Israel kile ambacho Biblia imesema. Ukiona mtini tafuta tawi. Kipindi cha baridi hupukutisha majani. Na huchipuka baada ya kipindi cha baridi kupita.

Tawi linaonesha kuna nyakati mpya inakuja. Tawi halibadilishi nyakati ila linaonesha kuwa wakati umefika.

Kwa hiyo Israel ni saa ndio maana ni tawi likionesha kuwa majira ya kuja kwa Yesu kumekaribia baada ya mwaka 1948.

Sasa unapolotazama jambo hili ni muhimu kujua yafuatayo.

1. Mipaka ya Taifa la Israel. Kuna tofauti na mipaka ya uzao la Israel
Mpaka wa uzao wa Israel ipo hadi nje ya Israel ya sasa maana kuna kabila kama mbili ziko maeneo Karibu na Lebanon sasa ni hadi mto frati ambako kwa sasa ni maeneo ya Badgad nchini Iraq.

Na walipokuwa wanapewa mipaka na umoja wa mataifa ni tofauti kidogo . Mipaka waliyopewa taifa la Israel iko tofauti kidogo na ile ya kwenye biblia. Na walipokuwa kwenye kupokea mipaka hiyo waarabu hawakukubali.

Na ikatangazwa vita na walipigana na kushinda na kuongeza kwenye mipaka na kufikia karibia asilimia 80% ya mipaka waliyopewa na Musa.

Mpaka mwaka 1967 kulikuwa na vita 3 kuu waliopigana. Na waliongeza mipaka.
Sasa kwa kuwa Israel ni saa ya mambo ya kiroho kila baada ya muda mchache utasikia habari za Isarel kwenye vyombo vya habari. Sio kwamba ni pambo ya habari hapana ila saa huwekwa mahali panapoonekana na ndio maana lazima habari zake usikie na ukisikia hakikisha unatafsiri kibiblia kwanza.

2.Umiliki wa mji wa Yerusalemu.
3.Eneo la kuabudia la Moria ni eneo ambalo kulikuwa na hekalu la Suleman ndipo Ibrahimu alitoa sadaka ya Isaka. Na pia ni eneo ambalo Daudi alitoa sadaka alipomuona malaika baada ya kukosea kutokana na kuwahesabu watu bila idhini ya Mungu. Na Mungu alimpa adhabu Daudi ya tauni. Sasa alipomuona malaika pale aliambiwa atoe sadaka na eneo lile alilinunua kwa myebusi. Sasa upo msikiti wa Waislam ila eneo hili litaendelea kujadiliwa

4.Uongozi wa juu wa Israel nafasi ya Waziri mkuu na raisi. Baada ya miaka 40 kuna kitu kinabadilishwa.
Toka mwaka 1967 jumlisha na 40.alafu cheki mabadiliko ya uongozi.
5.Ubadilishanaji wa ardhi kwa amani.

Hakikisha unatafsiri mambo ya Israel kibiblia na bado ina nafasi yake kama kawaida kwa Mungu. Na kanisa ni mtaokeo ya agano jipya ambalo Mungu alifunga na nyumba ya Yakobo. Nafasi ya Israel ipo pale pale na kanisa lilipandikizwa katika tawi kwa hiyo usijigambe kuwa nafasi ya Israel kwa Mungu imechukuliwa na kanisa.(mataifa)

SASA KWANINI TUNAFUATILIA HABARI HIZI
1. Israel ni saa ya siku za mwisho
2. Inakupa sensitivity ya majira na nyakati
3.Sensitivity juu ya mavuno. Mungu anataka watu wake waje kwake kwa haraka kabla Yesu hajaja.

4.Kutambua kuwa yu karibu mlangoni. Kama mkristo lazima ujiandae na ujio wa Yesu. Kama una Yesu jiandae vizuri kuja kwa Yesu. Kuokoa ndio mwisho wa safari. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.Mathayo 24:13
5. Sensitivity ya Kiroho sikiliza mwalimu na mchungaji. Kuwalisha watu chakula kwenye majira yake. Usiwape chakula kiholela. Baada ya saa mbili usiku watalaam wanashauri usile chakula kizito maana kinakuletea uzito mwilini. Sasa ukiwa Mwalimu wa neno la Mungu lazima uwaliashe watu chakula kwa wakati sahihi maana si kila muda ni muda wa kula.

Nimekuambia haya kujua kuwa ujue Yesu Karibu anarudi.
Wewe kama mkristo ibariki Israel usilaani na ukiona watu wanalaani taifa la Israel wewe bariki.
 
Hizi habari zako zina udhaifu sana.Mpaka leo unazungumzia kumpokea Yesu mawinguni.Mawingu katika dunia yapo chini sana.Ukisafiri kwa ndege hata ndogo unayawacha chini.Na huku kwetu milimani mawingu siku nyengine yanakuwa chini ya milima. Kwa maana hiyo siku hiyo atatokea bondeni kupanda mlima.
 
Hivi hilo hekalu la Nabii Suleimani likavunjwa pakajengwa msikiti,,,,huo msikiti ulijengwa wakati suleman hayupo duniani au yesu yupo au Muhammad yupo(wakati upi)?
 
Back
Top Bottom