Faida za kusoma vitabu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida za kusoma vitabu.

1. Hukuongezea marifa mapya
Lengo kubwa linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye maandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyowekwa kwenye kitabu husika.

Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu; kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye vitabu.

2. Hukuwezesha kufikiri kwa kina
Kwa hakika vitabu huongeza sana uwezo wa kufikiri. Unaposoma vitabu unafahamu mambo ambayo yatakufanya ufikiri zaidi; mara nyingine kitabu kitakuacha na maswali ambayo yatakufanya utafakari kwa kina zaidi juu ya mambo mbalimbali.

3. Hukuongezea uwezo wa lugha
Mbinu moja wapo ya kuongeza uwezo wa lugha ni kusoma machapisho mbalimbali yaliyoandikwa kwa lugha unayotaka kujifunza.

Kwa kusoma vitabu utaongeza msamiati, utajifunza sarufi ya lugha au hata mbinu mbalimbali za matumizi ya lugha.

Unachotakiwa kuzingatia hapa ni kusoma vitabu bora mara nyingi kadri uwezavyo.

4. Hukuburudisha
Vitabu ni burudani ya kipekee na ya gharama rahisi unayoweza kutembea nayo mahali popote. Viko vitabu mbalimbali tena vya bei rahisi ambavyo vinaweza kukuburudisha na kukufurahisha.

Vitabu hasa vile vya kifasihi ni burudani tosha ya aina yake. Unaweza kusoma vitabu vilivyochapishwa au vitabu pepe kwa kutumia simu au kompyuta yako.

5. Hukupa hamasa
Maisha yana changamoto mbalimbali; hivyo utahitaji kitu cha kukuhamasisha kutoka hatua moja hadi nyingine. Kwa kusoma vitabu vya hamasa kuhusu maswala mbalimbali ya maisha utaweza kuhamasika zaidi.

Vipo vitabu vilivyoandikwa kukuhamasisha au vilivyo andika maelezo ya watu waliofanikiwa na jinsi walivyopita kutoka changamoto moja hadi nyingine.

6. Hukuokolea pesa
Vitabu havihitaji umeme, mafuta au matengenezo ili kufanya kazi. Baadhi ya vitabu vingine pia hufundisha mbinu mbalimbali za kuokoa pesa.

Hali kadhalika kusoma vitabu kutakuokolea pesa nyingi ambazo ungezitumia kwenye maswala kama vile starehe.

7. Hukuwezesha kutumia muda vizuri
Unapotumia muda wako kusoma vitabu, ni wazi kuwa hutopata muda wa kupoteza. Kusoma vitabu kutakufanya utumie muda wako kuongeza maarifa yako zaidi.
 
Umeongea ukweli mtupu, nimesoma rich dad poor dad, na the richest man in Babylon, hmo kuna elimu brilliant kuhusiana na masuala ya fedha na namna gan kuivuta pesa ije na ikae kwako daima, are you working for money or money is working for you?.

Kuna "The power of your subconscious mind na awake you're inner fire," hvi vitabadilisha maisha yako kabisa toka level fln ya kuwa mtu mwingine kabisa.
 
Usomaji usaidia pia kukuza uwezo wa mtu binafsi katika uandishi wake kama ni mwandishi kwani upata mwanya wa kuongeza maarifa mapya kulingana na wakati sahihi/mabadiliko ya sayansi na teknolojia (majira yaliyopita, yaliyopo na yajayo).
 
Ma/Wa......Tanzania yalivyo mavivu hapa yanapita tuuu!! fyuuum!! hata hawataki kuona yaliyomo hiii ina onyesha ni jinsi gani ni kazi sana Mbongo kusoma vitabu!

wabongo ukitaka uwapatie wape vitabu vya umbeya, Nongo, uchawi, km gazeti la Sani aaaah! umewaweza! utapiga hela mpaka ulie pooo!! lkn sijui how to be rich???utasubiri sana!
 
Ikiwa unataka kupata maarifa na kuboresha maisha yako kwa njia ya kusoma vitabu, basi fahamu faida za kusoma vitabu.

1. Hukuongezea marifa mapya
Lengo kubwa linalowafanya waandishi wa vitabu kuandika vitabu ni kuweka maarifa yao kwenye maandishi. Hivyo kwa kusoma vitabu unapata maarifa mbalimbali yaliyowekwa kwenye kitabu husika.

Hivi leo kuna vitabu vinavyohusu takriban kila kitu; kwa hiyo maarifa yoyote unayoyahitaji unaweza kuyapata kwenye vitabu.

2. Hukuwezesha kufikiri kwa kina
Kwa hakika vitabu huongeza sana uwezo wa kufikiri. Unaposoma vitabu unafahamu mambo ambayo yatakufanya ufikiri zaidi; mara nyingine kitabu kitakuacha na maswali ambayo yatakufanya utafakari kwa kina zaidi juu ya mambo mbalimbali.

3. Hukuongezea uwezo wa lugha
Mbinu moja wapo ya kuongeza uwezo wa lugha ni kusoma machapisho mbalimbali yaliyoandikwa kwa lugha unayotaka kujifunza.

Kwa kusoma vitabu utaongeza msamiati, utajifunza sarufi ya lugha au hata mbinu mbalimbali za matumizi ya lugha.

Unachotakiwa kuzingatia hapa ni kusoma vitabu bora mara nyingi kadri uwezavyo.

4. Hukuburudisha
Vitabu ni burudani ya kipekee na ya gharama rahisi unayoweza kutembea nayo mahali popote. Viko vitabu mbalimbali tena vya bei rahisi ambavyo vinaweza kukuburudisha na kukufurahisha.

Vitabu hasa vile vya kifasihi ni burudani tosha ya aina yake. Unaweza kusoma vitabu vilivyochapishwa au vitabu pepe kwa kutumia simu au kompyuta yako.

5. Hukupa hamasa
Maisha yana changamoto mbalimbali; hivyo utahitaji kitu cha kukuhamasisha kutoka hatua moja hadi nyingine. Kwa kusoma vitabu vya hamasa kuhusu maswala mbalimbali ya maisha utaweza kuhamasika zaidi.

Vipo vitabu vilivyoandikwa kukuhamasisha au vilivyo andika maelezo ya watu waliofanikiwa na jinsi walivyopita kutoka changamoto moja hadi nyingine.

6. Hukuokolea pesa
Vitabu havihitaji umeme, mafuta au matengenezo ili kufanya kazi. Baadhi ya vitabu vingine pia hufundisha mbinu mbalimbali za kuokoa pesa.

Hali kadhalika kusoma vitabu kutakuokolea pesa nyingi ambazo ungezitumia kwenye maswala kama vile starehe.

7. Hukuwezesha kutumia muda vizuri
Unapotumia muda wako kusoma vitabu, ni wazi kuwa hutopata muda wa kupoteza. Kusoma vitabu kutakufanya utumie muda wako kuongeza maarifa yako zaidi.
Asante
 
Back
Top Bottom