Faida za kula pilipili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida za kula pilipili

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Jun 23, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Faida ya Afya ya Kula Pilipili

  Japokuwa Pili pili inaliwa na watu wa jamii mbali mbali, Faida na Afya ya kula pilipili wengi hawazijui au hazijulikani na watu wengi.

  Kwenye pilipili kuna kemikali iitwayo Capsaicin, ambayo ndio inayo sababisha muwasho na joto la pilipili.

  Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu

  Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. Hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika Chuo Kikuu cha Tasmania, utafiti iliyochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, mwezi Julai 2006.


  Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

  Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

  Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi!

  Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)
  Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

  Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu.

   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Asantesana mkuu ni habari njema kwa laji pili pili kama mimi na kweli mara nyingi nikipataga mafua huwa naweka pili pili nyingi kwenye supu ya kuku na husaidia sana.


  kitu kingine kinaweza ku-support ni wahindi wengi naona wembamba japo kuwa vyakula vyao vina mafuta mengi, nadhani ni pili pili inawasaidia kwani vyakula vyao vina pili pili sana.
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Ahsante kwa hii topic yako, mie mwenyewe iko penda sana kula pili pili.Tena sipendelei ya unga na penda ile pilipili fresh kuitafuna.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Nilivyoiona tu hii thread nikakumbuka wewe kumbe umeshatinga jamvini lol! Mimi ni mpenzi sana wa pili yaani hata chakula kiwe kitamu namna gani bila pili pili sikifurahii sana lol! na kukiwepo na pilipili tena ile kali basi hapo ndiyo utamu huongezeka. Kumbe zina faida yake mwilini! wacha tuzitafune tu.
   
 5. O

  Omumura JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Idumu pilipili mbuzi na pilipili kichaa!
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  asante kwa habari njema, mi nilifikiri najiumiza bure, kumbe inanitibu kiaina!!
   
 7. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  lakini ni hatari kwa wenye matatizo ya vidonda vya tumbo kwani huongeza kiasi cha tindikali inayozalisha na tezi za tindikali tumboni
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Lakini walaji wa pilipili hatuwaoni kwenye kula staftahi ya chai asubuhi au jioni.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Mkuu fafanua hapo kwenye staftahi ya asubuhi na jioni. Nijuavyo mimi staftahi ni asubuhi tu...au kuna nyingine ya jioni pia?
   
 10. 2my

  2my JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ingekuwa tamu wengi tungeiweza but lol!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  hahahahahahah si mnaogopa kuwashwa! sasa wengine hapo ndiyo tunasikia raha za kupita kiasi na zinapokosekana msosi haupandi vizuri ati!
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Staftai ni kifungua kinywa, sasa kwa wale wanao funga si kifungua kinywa chao ni jioni mkuu?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Mkuu X-PASTER si wapenda pilipili wote wapenzi wa kukamata masanga na si wapenda masanga wote walaji wa pilipili na nimeshakutana na wengi katika makundi hayo mawili. Kwa hiyo unaweza kumkuta mpenda pilipili ambaye staftahi ni kama kazi hawezi kuikosa siku yoyote labda kama ni mgonjwa na chakula kimegoma kabisa kupita.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana X-P mie nakula pilipili kama Baniani mpaka watu wanasema nitapata madhara ...kumbe kuna faida
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  .......Na Hoho je?.kuuuubwa hamna kitu hata toddlers wanaichezea
   
 16. s

  sabra Member

  #16
  Jun 25, 2010
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pilix2 tamu ikiingia mwilini lakini ikitoka blaa!! Pia ni silaha ya kuzuia majambazi usiku, unawatupia machoni hafu unasikilizia muziki wake!!! Thenks sana
   
 17. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mmmm! kama baniani, najua baniani wengi wanapata shida toilet kwa kula pili pili kupindukia, na wengi nasikia huweka feni ya kuwapepea makalioni
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahaha labda ni Baniani mweusi lol!

   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Jun 25, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,411
  Trophy Points: 280
  Hivi wapi wanatengeneza na kuuza juisi ya pilipili?
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usije kwenda msalani na barafu tu!
   
Loading...