My sister WoS, kwanza nikushukuru sana kwa mada nzuri. Mawazo yangu ni kwamba tatizo kubwa kwa UKIMWI Tanzania ni ELIMU. Najua wengi watapinga kua mbona kuna NGOs nyingi zinatoa ushauri na elimu ya afya na UKIMWI. Ukweli ni kua wote tuliosoma thread hii tutakubali kuna mambo mapya tumejifunza kutoka kwa WoS na wachangiaji wengine. Sasa jiulize kama wewe/sisi tunaoweza kupata hizi taarifa kwa intaneti (elites) tumepata elimu mpya kutokana na thread hii, vipi walioko vijijini au wasio na uwezo wa kupata hizi taarifa? Vipi kuhusu watanzania wengi ambao hata magazeti hawanunui wala redio hawasikilizi? Ukweli ni kwamba wengi wanakufa/kuathirika na UKIMWI kwa sababu moja tu...WANADHANI WANAJUA SANA KUMBE HAWAJUI..... mnasemaje kuhusu hili?