Faida za kujiweka wazi (disclosure) ukiwa umeathirika na virusi vyaUKIMWI

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Wana JF,
Kuwa na VVU/UKIMWI ni kitu kinachoogopesha sana.Watu wengi huogopa kupima kwa sababu hawataki kujua hali zao kama wako positive au la.Mtu anakuwa na hofu sana endapo atapima agundulike ndio ivo tena kaathirika.
Tukumbuke kuwa kwa miaka ya sasa, status ya kuwa positive haikatishi tamaa kama miaka ya nyuma wakati hatujafahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI au kuwa na maambukizi ya VVU/HIV.Sasa hivi kuna matumaini ya kuishi zaidi na hata miaka mingi endapo tu mtu utajua hali yake MAPEMA.

Kuwa na HIV haimaanishai kuwa na UKIMWI.....wataalamu wanashauri kuwa ni vema watu kupima na kujua hali zao ili kama ni negative ujue namna ya kujilinda na maambukizi.Ukiwa positive pia siyo mwisho wa dunia..utapata ushauri nasaha wa kukufanya uishi kwa matumaini......utakuwa umepata faida zaidi hasa kama utapima kabla Virusi havijafanya mashambulizi ya kukudhoofisha hadi ukaingia kwenye stage ya UKIMWI (AIDS).

Ukishajua status yako kuwa ni positive, inashauriwa ufikirie kujulisha wengine kwa hatua - ndugu wa karibu, mwajiri wako, mume/mke n.k. Ila uwe mwangalifu kwa kujiandaa na matokeo ya disclosure.Disclosure yenyewe ni kama tiba...ni ajabu! Watu ambao wamepitia hali hii wanatoa ushuhuda huu ambao kama hujaona na kuwasikiliza ukaona faida walizozipata unaweza kufikiria ni porojo tu.

JF mnaonaje hii?
 
mh!
mama angu WOS,
hili gonjwa linazungumzika vizuri kwa mtu ambae hajawahi kuuguza muathirika!USIOMBE KABISA IKUTOKEE,because you will never talk!
............INATISHA SANA
 
.............lakini kupima na kujua afya yako NI VIZURI SANA,kama unaweza!ila kwa mimi ambaye ninajua mateso yake kupitia watu ninaowafahamu na niliowauguza LIVE!i will neva think of it
 
Ni kweli WoS kwa uliyoandika. Lakini tatizo kubwa katika jamii zetu ni unyanyapaa pale unapojulikana una HIV. Mfano ni pale Mme atakapomueleza Mke kuwa nimepima na ninao, kwa haraka haraka mambo yanaweza kuwa mazuri. Lakini Mke akimueleza Mme kuwa kapima na kakutwa +ve matatizo yanaweza anza hapo. Japo yawezekana wote wanao. Vile vile makazini, kama ukimueleza bosi, utaanza kunyoshewa vidole na wafanyakazi wengine, na hata kutengwa.

Nadhani huu ugonjwa mawazoni mwa watu huwa ni kama kutenda zambi ama maovu. Japo twatakiwa ishi na walioathirika kama tunavyoishi na watu wanaougua magonjwa mengine bila kuwanyanyapaa. Leo yeye, kesho mimi.
 
Mfumwa,
Ni kweli kabisa.Unyanyapaa ni kikwazo kikubwa sana katika vita dhidi ya UKIMWI. Pia ni kazi kweli mwanamke kupima na kumwambia mumwewe kuwa kapima na ana VVU.Ila wanaume wangejiuliza - je ni sahaihi kuendelea kuishi kana kwamba hakuna kitu kama hicho halafu uangamie kwa kukosa msaada au ni bora kujua ili uanze mikakati ya kuishi kwa matumaini? Tukumbuke pia kuwa asilimia kubwa ya maambukizi kwa takwimu za karibuni zinaonyesha kuna maambukia zaidi kati ya wanandoa na wasomi ( elites).Ukichunguza sana hii inatokana na makundi haya kuficha kichwa mchangani kama mbuni!
Kunyooshewa vidole ni kawaida mwanzoni na baada ya hapo watu wanazoea na kuanza kuwa na moyo wa huruma na upendo.
 
Gonjwa hili linatisha kwa mwenye HIV na kwa wale wanaomzunguka. Watu wengi wana-equate HIV/UKIMWI na dhambi. Hilli linaleta woga wa kujifunua kwa wagonjwa. Tatizo lingine ni unyanyapaa wa wale wanaodhani ni wazima (kwani wengi hawajapima).

Kumbe mgonjwa na wazima wanahitaji wote kufanya mapinduzi ya fikra. Kuuona ugonjwa huu kama ugonjwa wa kawaida japo bado hauna tiba. Tukiwa na mwelekeo huu watu hatutaogopa kupima wala hatutaogopa kujulikana tukiwa positive, wala hatutawanyanyapaa wagonjwa.

Kweli kujijulisha kama mtu uko positive ni jamb jambo jema. Hakika linaleta faraja kwa mgonjwa, utulivu na amani fulani. Kuficha kunaumiza kwa sababu mgonjwa anakosa faraja kutoka kwa wazima, anakosa neno la kumpa matumaini, la kumwambia "maisha bado yapo tena marefu". Hili ni jambo la maana sana.

Kumbe tukapime ili tuweze kujilea vilivyo: kwa kujitunza kama tuko positive, au kwa kujilinda sawasawa kama tuko negative.
 
Kuna hili suala la mke na mume na status zao.Kwa vile basi kuna urahisi zaidi kurudia maambukizi kila mara wanandoa wanaposhiriki kitendo, laiti kama wangelijua hali zao..huenda wangetumia kinga kuzuia maambukizi ya kurudia ruadia.Watu wanadhani kuwa wote mkiwa na virusi basi haina haja ya kujikinga.Huu ni upotoshaji.Ikumbukwe kuwa kila kitendo huongeza viral load na kupelekea kubadili hali kutoka kwenye VVU na kuingia kwenye UKIMWI kwa haraka zaidi na hasa kama wahusika hawajui wakaishi vizuri zaidi kwa maana ya lishe inayofaa na kupumzika.

Nini kifanyike ili wanaume wakiwa kama viongozi wa familia waongoze zoezi hili la kupima? Pia inaonekana wanawake wako wepesi zaidi kukubali kupima kuliko wanaume.
 
mh!
mama angu WOS,
hili gonjwa linazungumzika vizuri kwa mtu ambae hajawahi kuuguza muathirika!USIOMBE KABISA IKUTOKEE,because you will never talk!
............INATISHA SANA

Unajua Geoff...HIV status ni tofauti na AIDS....kupima kunatakiwa kufanyike pale mtu ana afya yake bado maana kutoka HIV hadi UKIMWI kuna stages kama 4-5.Ukisubiri hadi uingie kwenye UKIMWI hapo unaweza usisaidike sana. Kosa wengi wanalofanya ni kuogopa na kuacha kupima hadi UKIMWI unapoanza ku harrass ndipo mtu anapimwa na kugundulika na ugonjwa.Laiti kama angepima mapema.
Ni uamuzi mgumu but worthy taking.Just bite the bullet!
 
Wana JF,
Kuwa na VVU/UKIMWI ni kitu kinachoogopesha sana.Watu wengi huogopa kupima kwa sababu hawataki kujua hali zao kama wako positive au la.Mtu anakuwa na hofu sana endapo atapima agundulike ndio ivo tena kaathirika.
Tukumbuke kuwa kwa miaka ya sasa, status ya kuwa positive haikatishi tamaa kama miaka ya nyuma wakati hatujafahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI au kuwa na maambukizi ya VVU/HIV.Sasa hivi kuna matumaini ya kuishi zaidi na hata miaka mingi endapo tu mtu utajua hali yake MAPEMA.

Kuwa na HIV haimaanishai kuwa na UKIMWI.....wataalamu wanashauri kuwa ni vema watu kupima na kujua hali zao ili kama ni negative ujue namna ya kujilinda na maambukizi.Ukiwa positive pia siyo mwisho wa dunia..utapata ushauri nasaha wa kukufanya uishi kwa matumaini......utakuwa umepata faida zaidi hasa kama utapima kabla Virusi havijafanya mashambulizi ya kukudhoofisha hadi ukaingia kwenye stage ya UKIMWI (AIDS).

Ukishajua status yako kuwa ni positive, inashauriwa ufikirie kujulisha wengine kwa hatua - ndugu wa karibu, mwajiri wako, mume/mke n.k. Ila uwe mwangalifu kwa kujiandaa na matokeo ya disclosure.Disclosure yenyewe ni kama tiba...ni ajabu! Watu ambao wamepitia hali hii wanatoa ushuhuda huu ambao kama hujaona na kuwasikiliza ukaona faida walizozipata unaweza kufikiria ni porojo tu.

JF mnaonaje hii?

Jirani, wengi wa waathirika hawafanyi hayo ya kuwajulisha wahusika mbali mbali na wengi kwa kujua sasa wanasubiri umauti tu huwa hawajisumbui kabisa kutafuta tiba na wengine hufanya makusudi kuambukiza ugonjwa huo kwa watu wengine ambao si waathirika, hili linafanywa na wote wake kwa waume na waume mara nyingi hutumia pochi ili kuhakikisha wanafanya maambukizo haraka sana. Na kwa maoni yangu hili limechangia sana katika kusambaza ugonjwa huu maana nimesikia wengi wakihadithia kwamba "fulani kaamua naye kuambukiza hakubali kufa pekee yake". "Nimesafiri na fulani kwa ndege toka mkoa fulani nikamuuliza lakini wewe si mgonjwa? akaniambia yeye kaambukizwa na yeye ni lazima aambukize na jamaa ana pesa si mchezo." Nilipokuwa nasikia stories kama hizi nilikuwa nabaki mdomo wazi.

Mwaka 2005 Management ya TANESCO ilikuwa inafikiria kupunguza wafanyakazi nadhani kati ya 300 mpaka 500 na tayari ilikuwa imeshaanza vikao na wawakilishi wa wafanyakazi mbali mbali ili kufanikisha zoezi hilo.

Miezi mitatu au minne baadaye nikasoma kwenye gazeti kwamba Management imeamua kusitisha zoezi la kupunguza wafanyakazi kutokana na vifo vingi vya wafanyakazi vilivyotokea katika miezi ile ya karibuni. Hili mimi lilinishtua sana na kuniogopesha. Nina jamaa zangu pale TANESCO na wengi wana nafasi za juu nikaamua niwaulize kama kweli kuna idadi kubwa ya vifo kiasi hicho. Wakaniambia ni kweli kabisa maana wengine wakishagundua wameathirika basi hawakubali kuondoka pekee yao ni lazima na wao 'waue wengine' na pia kuna mchezo wa watu kuzungukana. Mke wa fulani katembea na mume wa fulani, BF wa fulani katembea na GF wa fulani, Mume wa fulani katembea na GF wa fulani, basi ni vurugu mechi tupu!

Nchi za wenzetu ikithibitika kwamba umetembea na mtu huku unajua kama una HIV bila kumwambia au kutumia protection basi unafunguliwa mashtaka na wengi wameshafungwa katika nchi mbali mbali. Sijui Tanzania kama hili la watu wanaofanya makusudi kuwaambukiza wengine hili la kufunguliwa mashtaka lipo katika sheria zetu.

Je, hili la tiba kufanya kazi vizuri linatangazwa vya kutosha ili waathirika waweze kutafuta tiba hizo? Je, tiba yenyewe inahitaji uwe na pochi la nguvu? Kitu ambacho Watanzania walio wengi hawana.
 
Last edited:
Jirani, wengi wa waathirika hawafanyi hayo ya kuwajulisha wahusika mbali mbali na wengi kwa kujua sasa wanasubiri umauti tu huwa hawajisumbui kabisa kutafuta tiba na wengine hufanya makusudi kuambukiza ugonjwa huo kwa watu wengine ambao si waathirika, hili linafanywa na wote wake kwa waume na waume mara nyingi hutumia pochi ili kuhakikisha wanafanya maambukizo haraka sana. Na kwa maoni yangu hili limechangia sana katika kusambaza ugonjwa huu maana nimesikia wengi wakihadithia kwamba "fulani kaamua naye kuambukiza hakubali kufa pekee yake". "Nimesafiri na fulani kwa ndege toka mkoa fulani nikamuuliza lakini wewe si mgonjwa? akaniambia yeye kaambukizwa na yeye ni lazima aambukize na jamaa ana pesa si mchezo." Nilipokuwa nasikia stories kama hizi nilikuwa nabaki mdomo wazi.

Mwaka 2005 Management ya TANESCO ilikuwa inafikiria kupunguza wafayakazi nadhani kati ya 300 mpaka 500 na tayari ilikuwa imeshaanza vikao na wawakilishi wa wafanyakazi mbali mbali ili kufanikisha zoezi hilo.

Miezi mitatu au minne baadaye nikasoma kwenye gazeti kwamba Management imeamua kusitisha zoezi la kupunguza wafanyakazi kutokana na vifo vingi vya wafanyakazi vilivyotokea katika miezi ile ya karibuni. Hili mimi lilinishtua sana na kuniogopesha. Nina jamaa zangu pale TANESCO na wengi wana nafasi za juu nikaamua niwaulize kama kweli kuna idadi kubwa ya vifo kiasi hicho. Wakaniambia ni kweli kabisa maana wengine wakishagundua wameathirika basi hawakubali kuondoka pekee yao ni lazima na wao 'waue wengine' na pia kuna mchezo wa watu kuzungukana. Mke wa fulani katembea na mume wa fulani, BF wa fulani katembea na GF wa fulani, Mume wa fulani katembea na GF wa fulani, basi ni vurugu mechi tupu!

Nchi za wenzetu ikithibitika kwamba umetembea na mtu huku unajua kama una HIV bila kumwambia au kutumia protection basi unafunguliwa mashtaka na wengi wameshafungwa katika nchi mbali mbali. Sijui Tanzania kama hili la watu wanaofanya makusudi kuwaambukiza wengine kufunguliwa mashtaka lipo katika sheria zetu.

Je, hili la tiba kufanya kazi vizuri linatangazwa vya kutosha ili waathirika waweze kutafuta tiba hizo? Je, tiba yenyewe inahitaji uwe na pochi la nguvu? Kitu ambacho Watanzania walio wengi hawana.

Jirani,
1.Kujulisha/kutokujulisha - Hiki ni kitendo muhimu sana ila kinahitaki uangalifu kabla hujakifanya kwa sababu unyanyapaa hi dhahiri kwa vile jamii kubwa bado wako katika kutokufahamu vizuri kuhusu UKIMWI.Wengi hudhani kuwa muathirika ni mdhambi! Nani hana dhambi? au dhambi ni moja tu? kuzini? ni vipi kuhusu ufisadi/wizi, mauaji,uongo,dhuluma,uonevu?Nani anaweza kujihesabia uhalali kuwa hatendi dhambi? Je, wanaohukumu wamepima? Ni unyanyapaa ndio unaowafanya watu waambukize kwa makusudi.
2.Kuambukiza kwa makusudi -Haya ni matokeo ya kukosa ufahamu mzuri kuhusu UKIMWI.wangejua kuwa kuendelea kufanya kitendo bila tahadhari/kinga mwathirika anaongeza maambukizi mapya na huenda akapata virusi vikali zaidi ( kuna aina mbalimbali za virusi).Hata kuendelea kujamiiana na mtu yuleyule - mke/mume/mpenzi bila kinga pia ni hatari kwani kunaongeza kiwango cha virusi mwilini.Hapo mwathirika pamoja na kusambaza afe na wengine, anajikomoa mwenyewe.
3.Sheria kubana wanaosambaza kwa makusudi- Tanzania imepitisha Sheria ya UKIMWI tayari ambapo pamoja na mambo mengine inakazia kuzuia usambazaji kwa makusudi, suala la Usiri ( confidentiality), matunzo.huduma kwa waathirika n.k.Mtu anayesambaza kwa makusudi anaweza kushtakiwa na akionekana na hatia basi ataadhibiwa.Sheria hii ni mpya hajajulikana sana watu wengi hawajui hata kama kuna sheria kama hii.
4.Tiba - Sasa hivi kuna ARVs na zinapatikana baada ya Serikali ya Marekani kutoa msaada mkubwa sana chini ya PEPFAR ( Presidential Emergency Plan for AIDS)
 
WOS ukishajua tayari wewe ni victim usiwajulishe ndugu zako watakutenga
 
Wiki iliypita,kulikuwa na makala,BBC Radio,English Service,kwamba wapo madaktari,nadhani madaktari wa Tanzania ambao wamesema kupima watu kama wana virusi vya ukimwi ni waste of money. Kinachotakiwa ni kuwatibu tu wenye ukimwi huko vijijini. It is not clear watu watatibiwa vipi kama hawajapimwa.
Lakini watu wanaogopa kupimwa,wanaona haya kupimwa.If you cannot convine them,kwamba wasione haya kupimwa,then you have to find a way around this problem,jinsi unavyoweza kufanya kazi hii in a more discreet manner.
Pia unaposema unataka watu wachukue megaphone wamtangazie kila mtu kwamba wana ukimwi,this is fantastic. Who would want to do that?
Halafu ukisema ''usiwanyanyapae watu wenye ukimwi',this is not clear to me. Watu kama wanaumwa ugonjwa wa kuambukiza ni lazima uwanyanyapae. Kuna magonjwa nyemelezi yanayoambatana na ukimwi.
Halafu no one makes any comment about what these affected people should do. Should they continue to have sex? Do they seek out another person who is infected and have sex with them,or do they get protection by using clever condoms,or should they abstain from sex altogether and be celibate?
Halafu there is talk kwamba Bill Gates amepewa patent ya dawa ya kutibu ukimwi lakini anaificha,he doe not want to make it public,hataki watu wapone ukimwi.Nimeiona hii patent katika internet.
 
Wana JF,
Kuwa na VVU/UKIMWI ni kitu kinachoogopesha sana.Watu wengi huogopa kupima kwa sababu hawataki kujua hali zao kama wako positive au la.Mtu anakuwa na hofu sana endapo atapima agundulike ndio ivo tena kaathirika.
Tukumbuke kuwa kwa miaka ya sasa, status ya kuwa positive haikatishi tamaa kama miaka ya nyuma wakati hatujafahamu zaidi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI au kuwa na maambukizi ya VVU/HIV.Sasa hivi kuna matumaini ya kuishi zaidi na hata miaka mingi endapo tu mtu utajua hali yake MAPEMA.

Kuwa na HIV haimaanishai kuwa na UKIMWI.....wataalamu wanashauri kuwa ni vema watu kupima na kujua hali zao ili kama ni negative ujue namna ya kujilinda na maambukizi.Ukiwa positive pia siyo mwisho wa dunia..utapata ushauri nasaha wa kukufanya uishi kwa matumaini......utakuwa umepata faida zaidi hasa kama utapima kabla Virusi havijafanya mashambulizi ya kukudhoofisha hadi ukaingia kwenye stage ya UKIMWI (AIDS).

Ukishajua status yako kuwa ni positive, inashauriwa ufikirie kujulisha wengine kwa hatua - ndugu wa karibu, mwajiri wako, mume/mke n.k. Ila uwe mwangalifu kwa kujiandaa na matokeo ya disclosure.Disclosure yenyewe ni kama tiba...ni ajabu! Watu ambao wamepitia hali hii wanatoa ushuhuda huu ambao kama hujaona na kuwasikiliza ukaona faida walizozipata unaweza kufikiria ni porojo tu.

JF mnaonaje hii?

WOS, mara nyingi wanaotoa ushauri wa kuikubali hali ya kuwa na virusi nya ukimwi huwa wako negative. Sijawahi kusikia mtu atoa ushauri kama huu wako ambao ni positive.
 
Ni kweli dada yangu, kunafaida kubwa sana kama ukijua leo una ukimwi kuliko ukijua kesho.lakini bado siungi mkono kujiweka wazi ukiwa umeathilika kwa sababu bado jamii haijaukubali ugonjwa huu wa ukimwi,hivyo unapojiweka wazi kwa nia nzuri tu jamii inakutenga, hilo ndio tatizo la sasa.Lakini naunga mkono kupima na kujijua ili uanze badilisha mfumo wa maisha yako ule nini kwa kipindi hicho,uache vitu gani,ili uweze kuishi muda mrefu kuliko kutojua na kuishi muda mfupi.
 
kwa jamii nzima sioni mantiki hapo. jiweke wazi kwa mwenzi wako ama ndugu zako, inatosha. zaidi kama una ndoa. jana nimepata somo sana pale angaza mnazi mmoja. kama ningekuwa ninao wala nisingesema nimeenda huko. tatizo ni kwa wanandoa ambapo mama kwa mara ya kwanza aendapo kliniki LAZIMA kupimwa, kama atakutwa nao huwa ni ngumu kwake kumweleza mume. atazaa na hatakuwa anamnyonyesha mtoto na mwisho wa siku mzee atamuuliza, mbona humnyonyeshi mtoto? kwa woga mama atamnyonyesha akiugulia kwa uchungu akijua anaweza kumwambukiza mtoto. wanawake mtafute njia sahihi za kuwaeleza waume zenu kama kuna walioathirika. pia mjue kuwa ukimwi uko katika mkojo, kinyesi, matapishi, jasho, mate, kiufupi majimaji yote mwilini. so watch out unapocontact na watu na unapotoa msaada kwa mtu yoyote. jambo zuri ni kuwa virusi huishi kwa muda wa dakika 3-5, so make it 10 nje ya mfumo wake. nendeni mkacheki afya zenu. ni dakika 5 tu kujua majibu yako ila si lazima kuutangazia umma ila kuwa mstaarabu pale inapobainika umeathirika usiwaambukize wengine. kisheria ni kosa na kiimani ni dhambi.
 
WOS ukishajua tayari wewe ni victim usiwajulishe ndugu zako watakutenga

Fidel,
Kujitangaza kuna utaratibu wake... haukurupuki tu na kuanza kuhutuia kuwa jamani ehhh mie ndio ivo nimepima nikagundulika na virusi.Unajiandaa kwanza.Unaanzia na ushauri nasaha baada ya kupata majibu yako... pia unaangalia ni nani unaweza kumwamini kumwambia ...siyo lazima uanze na ndugu wa karibu.Unaweza kuanza kwenda kwenye asasi zenye kutoa support kwa waathirika PLWHA... huko utakutana na waathirika waliokwisha kujitangaza wazi na watakueleza nini cha kufanya.Haya ni kwa uchache.
 
Wiki iliypita,kulikuwa na makala,BBC Radio,English Service,kwamba wapo madaktari,nadhani madaktari wa Tanzania ambao wamesema kupima watu kama wana virusi vya ukimwi ni waste of money. Kinachotakiwa ni kuwatibu tu wenye ukimwi huko vijijini. It is not clear watu watatibiwa vipi kama hawajapimwa.
Lakini watu wanaogopa kupimwa,wanaona haya kupimwa.If you cannot convine them,kwamba wasione haya kupimwa,then you have to find a way around this problem,jinsi unavyoweza kufanya kazi hii in a more discreet manner.
Pia unaposema unataka watu wachukue megaphone wamtangazie kila mtu kwamba wana ukimwi,this is fantastic. Who would want to do that?
Halafu ukisema ''usiwanyanyapae watu wenye ukimwi',this is not clear to me. Watu kama wanaumwa ugonjwa wa kuambukiza ni lazima uwanyanyapae. Kuna magonjwa nyemelezi yanayoambatana na ukimwi.
Halafu no one makes any comment about what these affected people should do. Should they continue to have sex? Do they seek out another person who is infected and have sex with them,or do they get protection by using clever condoms,or should they abstain from sex altogether and be celibate?
Halafu there is talk kwamba Bill Gates amepewa patent ya dawa ya kutibu ukimwi lakini anaificha,he doe not want to make it public,hataki watu wapone ukimwi.Nimeiona hii patent katika internet.

Ndugu yangu Ganesh,
Asante kwa kuibua maswali very practical kwenye hili tatizo la UKIMWI ambalo inaonekana dhahiri kuwa watu wengi, tena hasa wale tunaowategemea wawe na uelewa mpana zaidi, bado wana mengi ambayo inawabidi kujua ili mapambano dhidi ya UKIMWI yafanikiwe.Nitaomba kushare machache kama ifuatavyo:
1.Kuogopa UKIMWI- Hii ni sawa kabisa kuuogopa ugonjwa.Kuuogopa tu bila kuchukua hatua hakutasaidia.Hatua hizo ni pamoja na kuufahamu ugonjwa/hali y akuwa na VVU mwanzo mwisho.Basic facts:-UKIMWI hauna tofauti na ugonjwa mwingine chronic kama pressure, kisukari n.k.Mbona hatuwaogopi wagonjwa wa magonjwa haya? Uambukizo wa UKIMWI hauji kwa casual contacts - unakuja tu pale damu,au majimaji ya sehem za siri yanapokuja into contact na mwili kwa maana ya kujamiiana, kuwekewa damu au kupitia michubuko ya mwili.

2. Unyanyapaa -Mate, machozi, jasho haviambukizi.Kula na mgonjwa, kumshika mkono, kuketi naye haviambukizi UKIMWI.Sasa kwanini tuwanyanyapae?..Je kwa wasiopima halafu wanaingia kwenye mahusiano ya kingono kwa mfano, mbona hawaogopi kwa kiwango hicho? Tena naona ni bora umjue mtu mwenye VVU/UKIMWI ni salama zaidi utachukua tahadhari kuliko yule ambaye hali yake hatuifahamu!Huyo ambaye hajajitangaza na anaonekana bomba huoni ni hatari zaidi?

3.Mahusiano ya kingono -Kwa wale wanaojua hali zao kuwa wako na vvu/ukimwi, hawakatazwi kujamiiana.Ila wanatakiwa kutumia condom wakati wote.Haijalishi kama wote wana VVU au ni mmoja tu.Hii inasaidia kupunguza kuongeza viral load.Pia mke na mume wenye VVU/UKIMWI wanatakiwa kutumia condom wakati wote.Pale ambapo wanataka kupata watoto basi wanaelekezwa namna gani wafanye.Kwa kifupi, wanapimwa CD4 counts zao kisha wanashauriwa kuchunguza mzunguko wa mwanamke kuhusu siku yuko likely kupata mimba.Siku hiyo wanashauriwa kujamiiana kwa dakika moja tu bila kinga!( siwezi kutoa details zote hapa)..na wapo waliofanikiwa kupata watoto tena wasiokuwa na VVU.Mradi baada ya hapo mama afuate mafundisho huko klinik kuhusu namna atakavyojifungua kuepusha damu ya mama yenye VVU isimwingie mtoto na baada ya hapo, mama amnyonyoshe mtoto miaezi sita mfululizo bila kumpa kitu kingine chochote.Hii huwa ni ngumu hasa kwa mama asiye na maziwa ya kutosha.Vinginevyo basi mama anashauriwa asimnyonyeshe mtoto maziwa yake kabisa.

Hayo ni kwa uchache tu.
 
WOS, mara nyingi wanaotoa ushauri wa kuikubali hali ya kuwa na virusi nya ukimwi huwa wako negative. Sijawahi kusikia mtu atoa ushauri kama huu wako ambao ni positive.[/QUOTE]
Ni kweli ndugu yangu hujakosea... huenda ni kwa sababu ya unyanyapaa ndio maana hujawahi kuona au kusikia washauri nasaha walioathirika.Jichanganye na uwe na moyo wa kuwasaidia utashangaa walivyo wengi - kuanzia viongozi wa dini, wanataaluma mbalimbali, volunteers, wanawake, wanaume, vijana, watoto n.k.Ulishawahi kusikia Asasi kama NACOPHA, TANOPHA, TANARELA,SHDEPHA+? ZOTE HIZI wengi wao ni waathirika na wanafanya kazi zao kwa uwazi bila kujificha.
 
Asante WoS kwa topic hii
Kwanza uelewa wetu kuhusu tofauti ya mtu kuwa na virusi vya ukimwi na mwenye ukimwi bado ni mdogo. Wengi wanafikiri HIV ndio AIDS. Very surpring hata baadhi ya washauri nasaha hawajui kirefu cha HIV achilia AIDS.

Pili ugonjwa huu unahusishwa na ngono, hali inayoleta stigma kuwa kila mwenye HIV+ve basi kaukwaa kwenye ngono. Kitanzania sex ni taboo, watu wanakabiliwa na inhibition just to talk about sex let alone exposure.

Hata ndani ya familia zetu wazazi tunashindwa kuongea na watoto wetu kuhusu sex na aids. Wife alinishangaa nilipojaribu kuwa close na mabinti zangu wakiwa primary tulizungumza vizuri tuu, dada mkubwa yuko form II nikiibua tuu topic anaona noma, nikamwambia wife hiyo ni dalili keshaanza mambo mama tuu anamuogopa mwanae, itakuwa ni kuexpose kwa family members?.

Kutokana na kutojua tofauti ya kuwa HIV +ve na ukimwi, watu wanaogopa kupima ili wasijue, kwa kutokujua kuwa kutokujua kwao kunawacost kwa sababu by the time wanajua, ni tayari waathirika, na sometimes its too late kwa ARV kuokua jahazi.
Kwa taarifa tuu, kila mgonjwa anayepata admission kwenye hospitali ya umma, anapimwa HIV atake asitake, ili wadaktari wajue wadeal na nini, lakini mgonjwa haambiwi ila anashauriwa apime kwa hiyari yake.

Pia wamama wajawazito wote wanapokwendwa kliniki, wanapimwa kwa lazima na kutongozwa wapime kwa hiyari yao. Wale walioathirika, hata kama wamekataa kupima, bali muda wa kujifungua ukifika, wanapowa dawa za kinga kwa mtoto bila ya wao kujua, na anepowa ushauri kuwa asimnyonyeshe mwanae maziwa yake kwa hoja kuwa maziwa yako yameharibiki, wenye akili, wanakuwa wanaelewa somo.

Kupima kwa hiari ili kujua status yako ni muhimu, muhimu, muhimu sana ili ukijua ukoje na kukubali ulivyo, ni hatua muhimu sana, kama hujaambukizwa utakuwa mwangalifu zaidi. Kama unao, utaundishwa jinsi ya kuishi kwa matumaini na kuepuka ambukizo jipya.

Disclosure ya status yako kama una virusi sio muhimu sana kwa sababu utakuwa norma tuu, ila kama ni tayari umeathirika, yaani una ukimwi, hapa ni muhimu sana kuwajulisha unaoishi nao sambamba na mwajiri wako ili uweze kufaidika na huduma za bure za ARV na mwajiri pia ukupe light duty na kukuvumilia safari zako kibao za hospitali bila kuharibu kazi yako.

Kutangaza pia kunasaidia kukulinda kwa mujibu wa sheria ya ukimwi makazini, hata kama kunaupunguzaji wafanyakazi, wewe, hautapunguzwa na kuna maofisi yana sera kuwa kama wewe ni mtumishi muathirika na unatibiwa kwa bima ya afya,basi bima yako kwa magonjwa nyemelezi ya ukimwi, utatibiwa bure mpaka mwisho wa maisha yako hata baada ya kustaafu ajira hiyo rasmi.

Mwisho nakushukuru tena WoS wewe unaonekana ni mshauri nasaa, kama sio, then your born with.
 
Asante WoS kwa topic hii
Kwanza uelewa wetu kuhusu tofauti ya mtu kuwa na virusi vya ukimwi na mwenye ukimwi bado ni mdogo. Wengi wanafikiri HIV ndio AIDS. Very surpring hata baadhi ya washauri nasaha hawajui kirefu cha HIV achilia AIDS.

Mwisho nakushukuru tena WoS wewe unaonekana ni mshauri nasaa, kama sio, then your born with.

Ndugu yangu..mimi kama watu wengine wenye kupenda kujua mambo mengi hasa yale mtambuka( cross-cutting) na kuyazamia ili kuwa na uelewa mpana/mzuri, najisikia kudaiwa kama sita share ninachokijua na wengine.Ni kwa msingi huu tu.

Nakushukuru na wewe kwa kukazia point za maana sana kwenye hii ishu.

Pia nafikiri kila mtu anayo status yake kuhusu UKIMWI - ila wengi wanaogopa kujua.Uzuri wa kujua ni kujilinda kama status yako ni negative na kuishi positively kama wewe uko positive.Kwa wale walio negative wako mashakani zaidi kuliko hata wale wanaojijua wameathirika.Wasiojua status zao hao ni hatari zaidi kwao wenyewe na hata kwa watu wengine.
 
Back
Top Bottom