Faida za Kufunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida za Kufunga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Aug 15, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WAISLAMU kwa ujumla bado wanaendelea kutimiza nguzo ya nne ya Uislamu ya Funga katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan...

  Kuna faida za mwenye kufunga kiimani na kiafya, kwa sababu wapo baadhi ya watu hufikiria kufunga ni mateso au manyanyaso kwa mfungaji.

  Faida za kufunga zipo nyingi, miongoni mwao ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.

  Faida ya pili ya mfungaji wa swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.

  Mtume Mohammad (SAW) anausifia mwezi huu kwa kusema, "Huo mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kusubiri na hakika subira malipo yake ni pepo."

  Faida ya tatu kwa mfungaji ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya tajiri na maskini.

  Kwa hali ya kawaida tajiri ni nadra kushinda njaa, hivyo basi pindi anapokuwa katika swaumu anajua machungu ya njaa hata anapotembelewa na maskini akiombwa msaada na mtu huyo mwenye njaa aweze kumsaidia kirahisi akiwa anafahamu namna njaa inavyouma.

  Inakuwa vigumu kwa tajiri ambaye hajawahi kushinda njaa kusikia uchungu na kuwa mwepesi kumsaidia mwenye njaa kwa sababu anachukulia kama njaa ni jambo la kawaida.

  Kuhusu hilo la kufunga, lmam Ja'far Assadiq, amelizungumzia na kusema, "Hakika si jingine, Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufunga ili tajiri na maskini wapate kulingana (katika shida ya njaa na kiu), basi akapenda viumbe vyake wawe sawa na amuonjeshe tajiri maumivu ya kushikwa na njaa ili apate kumhurumia mnyonge na apate kumsikitikia mwenye njaa."

  Faida ya nne na ambayo ni muhimu zaidi wanayoitegemea ni kusamehewa dhambi yote ya mwaka ikiwa mwenye kufunga amefuata masharti yote na kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mtume Muhammad (S.A.W).
  Anasema, "Enyi watu! Hakika umewaelekeeni nyinyi Mwezi wa Ramadhani kwa baraka, rehema na msamaha, mwezi ambao ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko miezi yote, siku zake ni bora kuliko siku zote, masiku yake ni bora kuliko masiku mengine yote na saa yake ni bora na muhimu kuliko saa zote."

  Hivyo kutokana na maneno hayo Mtume Muhammad (S.A.W), anaonyesha kufunga kwa Muislam katika mwezi huu ni bora na heri kwake.


  Faida ya tano ya Swaumu inahusu upande wa afya zetu, kwa kawaida chochote kifanyacho kazi sharti kipumzike kwa muda, hii inajumuisha hata kwa upande wa mitambo.

  Kwa mfano, mitambo ambayo imeundwa kwa vyuma imara tena vyenye nguvu hufika wakati ambao hulazimika kusimamishwaa kwa marekebisho ili kuiendesha kwa ubora.

  Swali hapa linakuja, kwa nini sisi ambao tumeumbwa dhaifu tusivipumzishe viungo vyetu, hasa tumbo ambalo huendelea na kazi mfululizo kwa miezi 11? Hapo utauona ulazima wa kupumzisha matumbo yetu ili kuhifadhi afya zetu.

  Kuhusu hilo la kusaidia kiafya hata madaktari wakubwa duniani wamewahi kulizungumzia hilo la kufunga.

  Baadhi ya madaktari wakuu ulimwenguni, wamekaririwa wakithibitisha kuwa kufunga kuna faida kwa mfungaji na hata Mtume Mohammad (S.A.W.) anathibitisha hilo pale anaposema, "Fungeni ili mpate afya nzuri."

  Naye Imam Ja'far (A.S) anasema, "Kila kitu kina utakaso, kitakaso cha mwili ni kufunga (Swaumu)."

  Kwa mujibu wa daktari mmoja mkubwa kutoka Marekani, Dk. Car, amewahi kusema, "Ni wajibu juu ya kila mgonjwa ajizuie kula japokuwa kwa muda wa siku moja katika kila mwaka."

  Dk. Car katika maelezo yake aliongeza, "Vijidudu viambukizavyo maradhi huendelea na kunawiri pale mwenye mwili anapoendelea kula na kuvilisha, hivyo basi vitaendelea kukua.''

  Baadhi ya madaktari Waislamu na wasio Waislamu wameafiki shauri hili.

  Naye Dk. Abdul Aziz bin Ismail anadai kwamba kufunga siku moja ni kinga ya maradhi kwa mwaka.

  Isitoshe kwa siku za hivi karibuni, kuna hospitali mbalimbali zinazohimiza na kusisitiza umuhimu huu, kadhalika mara nyingi tunashuhudia wagonjwa wengi ambao huzuiwa kula kwa manufaa ya afya zao.

  Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Cairo, Dk. Muhammad Dhawahir, anasema: "Ugonjwa wa kuzidi maji mwilini, unene, moyo, ini, pafu na mengineyo huzuiwa kwa mtu kufunga Swaumu."
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kufunga kuna Faida nyingi sana kwa afya ya Binadamu haswa kwa hao wanaofunga huu mwezi wa Ramadhani.

  185. Na siku hizi ni za mwezi wa Ramadhani (1) mwezi wenye daraja tukufu kwa Mwenyezi Mungu ndipo ilipo teremshwa Qur'ani ili kuwaongoa watu wote kwa hoja zake zilizo wazi zinazo fikishia kheri, na zenye kutenga baina ya Haki na baat'ili kwa nyakati zote na vizazi vyote. Basi mwenye kuuwahi mwezi huu naye ni mzima, si mgonjwa, yupo mjini si msafiri, yampasa afunge Saumu. Na aliye mgonjwa anaye dhurika kwa kufunga au alioko safarini anaweza kula, na juu yake kuzilipa zile siku alizo kula kwa kufunga utapo ondoka udhuru. Kwani Mwenyezi Mungu hataki kuwapatisha watu mashaka na taklifa bali Yeye anapenda kuwafanyia watu sahala. Na Mwenyezi Mungu amekubainishieni Mwezi wa Saumu, na amekuongoeni ili mpate kutimiza siku za kufunga, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa uwongofu alio kuongoeni, na akakupeni tawfiki njema.
  (1) Imethibiti kwa matibabu ya kisasa kuwa Saumu kwa namna ya Qur'ani ina faida nyingi, katika hizo ni kuwa inasaidia katika kutibu maradhi ya sukari, inatengeneza matumbo, inapunguza maumivu ya viungo, na maradhi ya moyo, inapumzisha nyama za mwili, na inasafisha uchafu mwingi wenye madhara, na pia inakuwa ni kinga kwa maradhi mengi mengineyo. Je, vipi kwa mtu asiye jua kusoma na kuandika ayajue yote haya?
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Huku kufunga kwa upande wa kidini sina neno nako. lakini kwa upande wa kiafya ninatatizika na pale tumbo linapokuwa halina kitu siku nzima halafu jioni unakula mchanganyiko wa sukari, pilipili, chumvi, mafuta, vyakula laini na vigumu at once. halafu usiku wa manane tena. Hii imekaaje? Haina athari kwa kile ulichotegemea kupata kiafya kwa kufunga?
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Unapaswa uangalie chakula unacho kula na pia uligawe tumbo lako sehemu tatu, sehemu ya chakula, pili sehemu ya maji, na tatu sehemu ya hewa, na si kupapia mavyakula kama vile kesho hakuna kula tena.
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  binafsi si mwislam napenda zaidi niongelee ktk upande usio wa kiimani yaani realistic coz kiiman vitu vingi si realistic, kufunga 30days to be honest ina shape vizuri mwili wako kiafya, kama kila mwaka unaweza funga kwa siku 30 nadhan unanafasi ya mwili wako kua ktk hali nzuri throughout the yr! hongereni waislam kwa hili mnaweka miili yenu vizuri!
   
 6. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  waislam hawafungi siku nzima...! wanakula usiku. wanafunga mchana.

  semeni ukweli..! kufunga alifunga Yesu tu.!
   
 7. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umenena yaliyokweli,,Waislamu hatufungi siku nzima, tunafunga linapochomoza jua asubuhi hadi linapozama,, hivyo ndivyo tulivyoambiwa.
  Bila shaka ISSA (AS) nae alielekezwa kufunga hivyo alivyofunga. kikubwa hapa ni kuonesha UTIIFU (kufuata maamrisho)
   
 8. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio kufunga huko kwa maana na uelewa. Hapa inategemea utaratibu wa utekelezaji. Kwaresma (nikosoe kama nimekosea silabi) ina utaratibu wake na huitwa funga. Kufunga maana yake ni kujizuia na si lazima iwe kula na kunywa, hata kuongea pia yaweza kuwa funga. Muda na kitu cha kujizuia ndio kinachotofautisha wafungaji.
  Ili kutofautisha hayo unatakiwa kujua utaratibu unaotumika
  Upo hapo mkuu?
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mbona hueleweki ndugu yangu!!
  mara hawafungi, mara wanafunga mchana.
  Tukuelewe lipi??
   
 10. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waislamu hawafungi wanachofanya ni kugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku.Mijitu inaamka sanane za usiku inabugia mivyakula utadhani wanaachana na kula maisha hamna kitu waache kudanganya watu.Hakuna mtu aliwahi kufunga hapa dunia zaidi ya Yesu mwana wa Mungu wengine wanajaribu kidogo sana lakini waislamu hawafungu na hawajawihi kufunga hata siku moja.Kwanza ukifunga hutakiwi kumtangazia mtu lauka kama ukimtangazia mtu tayari umeshapata thawabu zako kwa mtu uliye mtangazia.Waislamu wanapoutangazia ulimwengu wameanzakufunga wanakuwa wamekiuka kanuni muhimu ya ufungaji
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kanuni muhimu ya kufunga aliyoiweka nani?
   
 12. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  KABONDE,naona unapoteza maana ya habari ya mwanzo.Pili unapotumia maneno kama "MIJITU" una maana gani?
  Ni vizuri tujifunze kuitumia nafasi hii vizuri katika kuelimishana na kupeana habari.Kama huna la kuchangia nyamaza na fanya mambo mengine.
  Naipenda sana forum ya technology hamna upuuzi kama unaoonekana katika forums nyingine.
  Tujitahidi kuwa wastaarabu kwani habari hizi zinasomwa na watu wengi mpaka vijana wa shule.
   
 13. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwaisa kanuni ipi na ya nani?
  Yaonekana wewe ni kobe hata kwenye kwaresma Duh! badilika kidogo, dunia yaisha hii unakoelekea ni uzeeni, vuta kabusara kidoooogo ka kumjua Mungu na kufanya Ibada
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tabia ya mtu uonekana kwenye maneno yake.
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Uelewe kuwa wanafunga masaa 12 tu na siyo siku nzima.................maana siku nzima ina masaa 24
   
 16. elimumali

  elimumali Senior Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Miaka mingi imepita sikujaaliwa kufunga kutokana na vidonda vya tumbo. Namshukuru Mwenyezi Mungu mwaka huu nina nafuu kubwa, nimeamua kufunga nami nipate thawabu za mwezi huu mtukufu.
  Kitu kimoja kinanitatiza, Waislamu naombeni mnipe maelekezo na matumaini. Pamoja na kwamba nafunga kwa moyo mkumjufu, na nimenuia hasa, lakini NAKOSA MUDA WA KUSWALI, ofisini niko busy, natoka usiku na nafuturu saa mbili usiku. JE, NI KWELI KWAMBA KUFUNGA BILA KUSALI NI SAWA NA KUWA NASHINDA NA NJAA BURE?
   
 17. Kaka

  Kaka JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2015
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 705
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80

  Kwanza nikupe pole kwa kuugua kiasi cha kushindwa kutekeleza hiyo ibada ya kufunga, nikupongeze pia kwakunuia kwa dhati kuitekeleza. Waislamu wanatakiwa kuswali swala zote 5 kila siku za maisha yao [niko tayari kusahihishwa kwenye hili] bila ya kujali ni wakati wa kufunga au la. Sasa unakuwa busy kiasi cha kushindwa kufanya ibada ya swala mkuu? Kwani huwa unafanya nini muda mapumziko ya chakula cha mchana? Huoni kuwa ni vyema ukatenga walau dakika 10 au 15 tu ndani ya muda wa mapumziko hayo kwa ajili ya kuswali? Muda wa kufungua swaum [bila shaka ni saa 12 jioni] ukifika unakunywa maji, ndio ushafungulia [waislamu mnisahihishe] hiyo saa 2 usiku inakuwa ni kula tu.
   
 18. n

  nimebadika juzi Senior Member

  #18
  Jun 19, 2015
  Joined: May 29, 2015
  Messages: 183
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  umemuelewa au unarukia kwa mbele
   
 19. David Harvey

  David Harvey JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2015
  Joined: Jul 17, 2014
  Messages: 1,702
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  Huu uzi umeletwa kwa lengo zuri ila kuna watu wanataka kuuharibu bure...muda c mrefu utaharibika
   
 20. mkorinto

  mkorinto JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 7,126
  Likes Received: 3,807
  Trophy Points: 280
  Faida nyingine ni maovu kupungua mtaani.
   
Loading...