Faida za kiafya za kutumia Karafuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
1625717694335.png

Faida za karafuu mwilini.
Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ambayo huweza kutibiwa kwa kutumia karafuu mmea huu wa karafuu.

Magonjwa ya meno
Kemikali ya Eugenol ambayo hupatikana kwa zaidi ya 85% katika mmea wa karafuu hasa katika mafuta ya karafuu ina uwezo mkubwa wa kuua na kuzuia maambukizi katika meno.

Vilevile kemikali hii na nyinginezo katika karafuu zina uwezo mkubwa wa kutuliza maumivu na hivyo kutumiwa kama tiba ya maumivu ya meno.

Kutibu magonjwa ya minyoo na amoeba
Eugenol pamoja na kemikali nyinginezo katika karafuu ziimethibitika kuwa na uwezo wa kuangamiza vimelea mbalimbali vya magonjwa vikiwemo vile ambavyo husababisha magonjwa ya minyoo na amoeba.

Kutibu maradhi yaliyotengeneza usugu wa dawa
Kwa baadhi ya magonjwa hasa ya fangasi na bakteria ambayo hayaitikii tena tiba za kawaida za dawa za kisasa.

Matumizi ya karafuu (mafuta) ni msaada mkubwa kutokana na uwepo wa kundi la kemikali mbalimbali zinazofanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu.

Hutumika kama kinga ya maradhi mbalimbali
Matumizi ya mara kwa mara ya mmea wa karafuu kwa kutafuna au kupaka mafuta ya karafuu huweza kutumika kama kinga ya magonjwa mbalimbali.

Mfano magonjwa ya meno, ngozi, magonjwa ya aleji, chunusi na maumivu. Hii inatokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha kemikali za Eugenol na flavonoids.

Kutibu maradhi ya sukari na damu kuganda
Kemikali za tannis, ellagic acid, gallic acid na flavonoids zimeonyesha uwezo mkubwa wa kusaidia damu kuganda hasa watu wenye tatizo la anemia.

Vilevile kemikali hizi zina uwezo wa kusaidia mwili katika mchakato wa kuweka mlinganyo wa sukari mwilini, hivyo kukukinga na tatizo la kisukari.

Kutibu magonjwa ya fangasi
Karafuu inaweza kutumika kwa kunywa au kwa kupaka mafuta yake katika ngozi ili kutibu maradhi ya fangasi.

Baadhi ya zinazoweza kutibiwa na karafuu ni fangasi za mdomoni, fangasi za kwenye ngozi na fangasi ya damu.

Hutumika kutibu majipu na chunusi
Karafuu ikichanganywa na mafuta ya rosemary na aloe vera hutumika kutibu na kuangamiza bakteria wa S. aureus ambaye husababisha majipu.

Bakteria wa P. vulgaris ambaye husababisha chunusi na bakteria wa S. epidermidis ambaye husababisha chunusi, mapunye na vibarango.

Kutibu na kuzuia ukuaji wa virusi
Kemikali ya Eugeniin ndani ya karafuu imeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia na kuthibiti ukuaji wa virusi mwilini.

Baadhi ya virusi ambao huweza kuthibitiwa na kemikali hii ni Virusi wa mkanda wa jeshi, virusi wa mafua, virusi wa herpes wanaoshambulia midomo na virusi wa homa ya ini aina C.

Kuondoa sumu mwilini
Kuna kiwango kikubwa cha viantioksideshaji vya flavonoids katika karafuu ambavyo husaidia kupunguza kiwango cha chaji huru mwilini.

Viantioksideshaji hivi pia hupunguza madini joto huru mwilini kama vile zebaki, madini ambayo ni hatari kwa uhai wa seli za mwili.

Kutuliza maumivu
Matumizi ya mafuta ya karafuu kwa kupaka katika mwili husaidia kutuliza maumivu mbalimbali ya mwili kama vile, maumifu ya misuli, maumivu ya neva hasa kwa wenye kisukari.

Pia maumivu ya mgongo, maumivu ya maungio na maumivu ya kichwa.

Kutibu saratani
Kemikali za Eugenol na dihydrodieugenol ndani ya karafuu zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuua na kudhibiti seli za saratani mwilini.

Hii inatokana na uwezo wa kemikali hizi kuingilia hatua mbalimbali za utengenezwaji wa protini katika seli hizi za saratani.

Kutibu na kulinda ini dhidi ya magonjwa
Kemikali za sanguinarine na benzo phenanthridine ndani ya karafuu zimethibitishwa kitaalamu kutibu na kutoa ulinzi katika ini dhidi ya maradhi mbalimbali.

Kutibu maradhi ya mzunguko wa damu
Eugenol na kemikali nyinginezo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kutibu maradhi ya mzunguko wa damu kutokana na uwezo wake wa kupunguza shinikizo la damu.

Hii inasaidia kuimarisha usafirishwaji wa damu na huweza kutumiwa na watu wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

Kuzuia kuharisha na kutapika
Unaweza kutumia karafuu na tiba nyinginezo katika kutibu matatizo mbalimbali ya mfumo wa chakula yanaweza kutibiwa na karafuu mfano, kutapika, kuharisha, kujamba na tumbo kujaa gesi.

Faida nyinginezo
Hutumika kama dawa ya kufukuza wadudu, kuimarisha kumbukumbu, kutibu vidonda na kutuliza homa.

Sehemu ipi ya mmea hutumika kama tiba?
Majani, maua na fundo la maua ambalo bado halijachanua ndio hutumiwa kama tiba. Na sehemu hizi huweza kutumiwa kama juisi, mafuta au matone.

Jinsi ya kunufaika na faida za Karafuu.
Maandalizi

Jinsi ya kutengeneza juisi:

- Vuna fundo ambalo bado halijachanua maua au maua ya karafuu kisha loweka katika maji kwa siku 14, au loweka katika pombe kali (70%) kwa siku 7.

- Uwiano ni vipande 2 vya karafuu katika mililita 50 za maji. Chuja juisi yako na tayari kwa matumizi.

- Jinsi ya kutengeneza mafuta ya karafuu:

- Mafuta ya karafuu huvunwa kutoka katika majani na matawi laini yaliyo karibu na majani.

- Loweka majani ya karafuu katika pombe kali kwa muda wa siku 7 hadi 15, Hakikisha unatikisa mchanganyiko wako kila baada ya siku mbili ili kusaidia uvunaji wa mafuta kwa ufanisi.

Matumizi
- Kwa ajili ya kutibu kuharisha, kutapika, kichefuchefu, vidonda vya tumbo na maradhi mengineyo ya ndani ya mwili kama yalivyoorodheshwa hapo juu.

- Kunywa juisi ya karafuu kwa kiwango cha mililita 130, sawa na nusu glasi kila baada ya masaa 8.

- Tumia kwa kudondoshea matone 3 hadi 5 mdomoni kwa maradhi ya kinywa na meno kisha acha walau dakika 3 bila kumeza wala kutema. baada ya dakika 3, unaweza kutema ama kunywa.

- Tumia mafuta ya karafuu kwa kudondoshea matone 2 mdomoni kwa maradhi ya mdomo.

- Kwa matumizi ya ndani ya mwili tumia matone 2 ya mafuta katika nusu glasi ya maji kwa kunywa.

- Kwa maradhi ya ngozi, paka kiwango kidogo cha mafuta katika ngozi yako mara 2 kwa siku.
 
Back
Top Bottom