Faida ya unyenyekevu katika ndoa na mahusiano kabla ya ndoa

Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu, hata ungekua umemkosea nini, ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume ama mpenz hafokewi, hagombezwi, haumfanyii kiburi na jeuri, akinuna na wewe unanuna, asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa ama mahusiano yako. Ni mume wako,,ni mpenzi wako,,unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.

Asipokutafuta mtafute,,asipoongea na wewe, ongea naye wewe,,hakunaga mke ama mpenzi anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe ama mpenz wake. Kunyenyekea hakukugeuzi kua housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke ama kipenz cha mwenzio, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana. Ujeuri weka pembeni.

Ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa ama mahusiano yao. Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu, panapotakiwa hekima na akili zitumie.

Asanteni.
Kwa hakika umeongoa vitu vizuri kwa afya ya mahusiano
 
Me ndo nikutafutage kwenye simu kila siku, while wewe huna habari kunitafuta? labda kama kwenye phonebook yangu upo alone. Mahusiano ni efforts za watu wawili, sio mmoja kama mfalme na mwingine kama mtumwa. Tutofautishe unyenyekevu na Ujinga
Heaven sent naomba tena usome huo ujumbe.
 
Back
Top Bottom