Faida ya unyenyekevu katika ndoa na mahusiano kabla ya ndoa

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,322
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu, hata ungekua umemkosea nini, ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume ama mpenz hafokewi, hagombezwi, haumfanyii kiburi na jeuri, akinuna na wewe unanuna, asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa ama mahusiano yako. Ni mume wako,,ni mpenzi wako,,unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.

Asipokutafuta mtafute,,asipoongea na wewe, ongea naye wewe,,hakunaga mke ama mpenzi anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe ama mpenz wake. Kunyenyekea hakukugeuzi kua housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke ama kipenz cha mwenzio, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana. Ujeuri weka pembeni.

Ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa ama mahusiano yao. Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu, panapotakiwa hekima na akili zitumie.

Asanteni.
 
shida ya binadamu mtu akikuonesha unyenyekevu basi unamuona falah unakaa kifua mbele kama panzi.....
Nilijua point hii itakuja.
Ndio mana kuna mdau hapo juu nimemjibua kua unyenyekevu huo unaapaswa usitumike vibaya kunyanyasa mwanamke ..wapo wanaume ambao wanatumia vizuri unyenyekevu anaopewa na mwenzie na inaongeza upendo baina yao lakin wapo wanaotumia vibaya in which sio jambo jema
 
Inaaminika familia nyingi zilizo bora huendeshwa na wanawake but in so tricky way.Yaani kidume asijione hana mamlaka hasa mbele za watu.Hawapendi kabisa kukaripiwa hao watu na vile wananguvu anaweza kukubutua na habari yote ikabadilika.
 
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu, hata ungekua umemkosea nini, ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.

Mume ama mpenz hafokewi, hagombezwi, haumfanyii kiburi na jeuri, akinuna na wewe unanuna, asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa ama mahusiano yako. Ni mume wako,,ni mpenzi wako,,unaruhusiwa kumng'ang'ania kama ruba.

Asipokutafuta mtafute,,asipoongea na wewe, ongea naye wewe,,hakunaga mke ama mpenzi anaambiwaga anajipendekeza kwa mumewe ama mpenz wake. Kunyenyekea hakukugeuzi kua housegirl na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke ama kipenz cha mwenzio, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke haraka sana. Ujeuri weka pembeni.

Ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa ama mahusiano yao. Kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu, panapotakiwa hekima na akili zitumie.

Asanteni.
asantee...
 
Back
Top Bottom