Faida ya Mwanga wa jua katika mwili wa binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya Mwanga wa jua katika mwili wa binadamu

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 19, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mwanga wa jua unasaidia kuimarisha kinga ya mwili  [​IMG]

  Huku kwa muda mrefu ikiwa inaaminiwa kwamba Vitamini D inayotokana na mwanga wa jua inaimarisha mifupa, uchunguzi mpya umeonyesha kwamba mwanga wa jua pia una umuhimu mkubwa katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na uwezo wake wa kukabiliana na magonjwa.

  Uchunguzi huo umeeleza kwamba, seli zinazoshambulia maradhi za mfumo wa kinga ya mwili ambazo hujulikana pia kama 'T Seli" zinategemea sana Vitamin D ili kuzifanya zitekeleze kazi yake.

  Carsten Geisler aliongoza uchuguzi huo amesema kuwa, wakati T seli zinapokutana na kidudu toka nje ya mwili, hufungua antena yake inayoitwa 'D receptor' ambayo inaitumia kwa ajili ya kusaka vitamin D. Wakati kunapokuwa hakuna vitamin hiyo

  inayotokana na jua suala ambalo hutokea kwa watu zaidi ya nusu duniani, seli hizo hushindwa kufanya kazi na kushindwa kufahamu tishio linalosababishwa na vijidudu vinavyosababisha maradhi.

  Wataalamu wana matumaini kwamba uchunguzi huo mpya utawezesha kuandaliwa mazingira ya kuwekwa mikakati mipya kwa ajili ya kupambana na magonjwa katika siku zijazo.
   
Loading...