Faida ya manjano (turmeric) (curcuma) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya manjano (turmeric) (curcuma)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jun 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG] [​IMG]


  MANJANO ;
  WENGI WETU TUNAIJUWA MANJANO NYUMBANI KWETU NA TUNAITUMIA KWA MATUMIZI YA KAWAIDA KAMA VILE , KUBADILI RANGI YA VYAKULA KAMA MCHUZI , WALI, SAMAKI , NYAMA, HATA KUBADILI RANGI ZA NGUO KAMA T-SHIRT NA MENGINEYO,
  ILA NITAJARIBU JAPO KIDOGO KUTOWA KWA MUKHTASARI FAIDA ZAIDI MBALI NA HIZOO'

  1=MANJANO MBICHI NA UKIISAGA KISHA UKIICHANGANYA NA ASALI MBICHI UKINYWA NI DAWA NZURI YA KUSAFISHA DAMU MWILINI,


  2=MANJANO MBICHI NA ASALI UKINYWA NI DAWA KUMBWA NA SHINIKIZO LA DAMU LIWE LA CHINI AMA LA JUU( HIGH & LOW BLOOD PREASURE,)
  3=MANJANO MBICHI NA ASALI NI DAWA YA KUONDOA MAFUTA HELEMU (CORESTROL) NDANI YA MIRIJA YA MISHIPA YA DAMU,
  4=MANJANO MBICHI NA ASALI UKINYWA , HUSAIDIA KUZUIYA KUPATA UGONJWA WA KIARUSI , AMA KUPOOZA (STROKE),
  5=MANJANO MBICHI, UNGA WA HABBATT SODA NA ASALI MBICHI NI DAWA KURAHISHISHA MFUMO WA MMENG'ENYO ( DIGETION FOOD)KWA WALE WENYE MATATIZO HAYOO,
  6=MANJANO MBICHI NA MAFUTA YA HABBATT SODA HUSAIDIA KUONDOA MATATIZO YA VIDONDA VYA TUMBOO ( ALSAA),
  7=MANJANO MBICHI NA YAI LA KUKU WA KIENYEJI , IKIPAKAA KWENYE NGOZI YAKO HUILINDA NGOZI YAKO KUIWEKA LAINII, PAMOJA NA KUILINDA NA KUCHAA KUWA KIBUDA, KUSINYAA, KUWA KAVU SANAKUUNGUWA NA JUA ( SUN BURN),
  8=MANJANO YA YAI LA KUKU WA KIENYEJI, UNAPAKAA USONI NI DAWA YA CHUNUSI( PENPULS),
  9=WATU WA VIJIJINI MBALI NA HOSPITALI, KAMA UMEJIKATA NA KISU , PANGA, JEMBE, UKITIA MANJANO YA UNGA ,TUMERIC POWDER, KWENYE JERAHA HUSIKA UNAZUIYA DAMU KUTOKA ( BLOOD CLOT) KAMA HUDUMA YA KWANZAA,
  10= MANJANO YA HABBATT SODA UKITUMIA KIKOMBE CHA KAWAHA NUSU , HUKUWEZESHA MFUMO WAKO WA FAHAMU KUWA BORA ZAIDI ,
  HIZO NDIO BAADHI YA FAIDA KIDOGO TUU ZA MANJANO ,
   
 2. C

  Crispin Nyoni JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2014
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Au nafananisha na homa ya manjano?Haisababishwi na hii kitu mkuu?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Manjano na Homa ya manjano ni vitu viwili Tofauti kabisa Mkuu Crispin Nyoni

  CHANZO, ATHARI , KINGA NA TIBA YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO.


  
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Mwathirika wa Ugonjwa wa homa ya Manjano
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   CHANZO, ATHARI , KINGA NA TIBA YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO.

  Ugonjwa wa homa ya Manjano ambao hufahamika kitaalamu kama HEPATITIS B ni hatari sana na umesababisha vifo vya mamilioni ya watu duniani kote. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani ( W.H.O ) kuna zaidi ya wau Milioni 350 duniani ambao wameathiriwa na ugonjwa huu hatari kabisa na zaidi ya watu 620,000 hufa kila mwaka kwa ugonjwa wa Manjano.  CHANZO CHA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO  Ugonjwa wa homa ya Manjano husababishwa na virusi viitwavyo " Hepatitis B " ( HBV ) ambavyo hushambulia zaidi ini la mwanadamu. Virusi hivi visipo tibiwa mapema hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha asratani ya ini ambayo hupelekea kifo.

  MAMBO YASABABISHAYO MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA MANJANO.


  Ugonjwa wa Manjano huambukizwa kwa njia zifuatazo :
  i. Kujamiiana bila kutumia kinga.
  ii. Kunyonyana ndimi
  iii. Kuchangia damu isiyo salama
  iv. Mama mjamzito mwenye ugonjwa huu anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa kujifungua.
  v. Kuchangia vitu vyenye ncha kali kama vile wembe na sindano.


  DALILI ZA UGONJWA WA MANJANO
  Dalili za ugonjwa wa manjano huchukua muda mrefu kuonekana tangu maambukizi yatokee, na zinapo anza kuonekana wazi wazi, mgonjwa anakuwa amesha athirika kwa kiwango kikubwa sana. Dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo :
  i. Uchovu wa mwili
  ii. Kichefuchefu
  iii. Mwili kuwa dhaifu
  iv. Homa kali
  v. Kupoteza hamu ya kula
  vi. Kupungua uzito
  vii. Kupatwa na maumivu makali ya tumbo upande wa ini.
  viii. Kukojoa mkojo wa rangi nyeusi
  ix. Macho na ngozi kuwa vya njano.


  KINGA YA UGONJWA WA MANJANO

  i. Kupatiwa chanjo ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
  ii. Kutumia kinga wakati wa kujamiiana
  iii. Kuacha kuchangia vitu vyenye ncha kali kama sindano, wembe n.k
  iv. Kutochangia mswaki
  v. Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  vi. Kuto ongezewa damu ambayo haijapimwa na kuthibitika kuwa salama.  TIBA YA UGONJWA WA MANJANO
  Ugonjwa wa manjano hauna tiba isipokuwa mgonjwa akiwahi hospitali atapatiwa dawa za kupambana na virusi kuvipunguza nguvu za kupambana na ini., kupandikizwa ini ambapo ini lililoathirika huondolewa na kuwekwa jingine japo ni vigumu kupata ini salama.

  Ukisha gundua kuwa umeambukizwa ugonjwa huu unashauriwa kuacha kutumia pombe, dawa za kulevya na vitu vingine vinavyo athiri utendaji kazi wa ini.
  Unaweza pia kunitembelea Blog Yangu bonyeza hapa http://************************.tr/
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2014
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Manjano na mdarasini eheee siku nitafika siku nitafika nitakula wali ehee wali na sombee na lupilipili ma na luchumvi inakolea kosingo --RIP-Abeti masikini
   
Loading...