Faida ya manjano kwenye urembo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Siku hizi mambo yamebadilika manjano yamekuwa ni kiungo muhimu katika ngozi, wakati hapo awali manjono yalikuwa yanatumika katika kupikia, lakini kwa sasa katika urembo bila manjano urembo wako unakuwa haujakamilika kabisa, manjano mbichi haijazimuliwa na sembe ndio nzuri, maana unaweza ukanunua manjano yakawa teyari yashachanganywa na sembe.

Manjano yanaweza kukusaidia katika urembo kama ifuatayyo;

Kutibu chunusi, Kutokana na tabia yake ya kupambana na bakteria manjano inauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bakteria, kwa wenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na maji ya waridi na wale wenye ngozi kayu unachanganya manjano na maziwa fresh kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na maji ya kawaida.

Pia manjano Inang'arisha ngozi, Manjano inatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na cream,kuungua jua au kufubaa kwa ngozi, unatakiwa uchanganye manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.

Manjano Inapunguza mafuta Kwa wenye ngozi ya mafuta pia manjano inasaidia sana kupunguza uzalishaji wa mafuta,hapa mtashanga kidogo, Unakunywa glasi moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara mbili kwa wiki, Pia unaweza kuchanganya manjano,limao na maji ya waridi na kupaka usoni kwa dakika 30.

Manjano inasaidia kupunguza kasi ya ngozi kuzeeka baada ya matumizi ya make up wiki nzima jitahidi mwisho wa wiki uwe unafanya facial ya manjano angalau mara moja,maana manjano husaidia ngozi isichoke haraka na hiyyo kupaka mwonekano mzuri wa ngozi yako.

Deusdedit Mahunda blog
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom