JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Siku za hivi karibuni watu wamekuwa wakitumia maji ya madafu na kuchanganya na ndimu au limao, huku wengine wakijiuliza ikiwa mchanganyiko huo hauna madhara yoyote kiafya.
Tafiti zinaeleza kuwa maji ya madafu yana faida kede kede mwilini, lakini lamao linaweza kuongeza ladha na lina vitamin C kwa wingi, na tafiti hizo kuongezea kuwa hakuna madhara yoyote ya kiafya katika mchanganyiko huo.
Faida za maji ya madafu yaliyochanganywa na ndimu au limao ni kama zifuatazo:-
Huchochea mmeng'enyo wa chakula.
Husaidia kinga dhidi ya saratani.
Husaidia kupunguza hatari dhidi ya Kiharusi.
Kurekebisha Sukari katika mwili.
Inasaidia urekebishaji wa Ngozi na kupona Makovu.
Husaidia kuua bacteria wa aina mbalimbali wakiwamo wale wanaosababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI.
Husaidia pia kupunguza maumivu wakati wa kupata haja ndogo (mkojo).
Husaidia kupunguza tatizo la msukumo mkubwa wa damu mwilini. Wataalamu wa lishe wanashauri maji hayo yanywewe asubuhi kabla ya kutumia chakula au kinywaji chochote.
Kwa watu wanene, huwasaidia kupunguza uzito na kuwaongezea hamu ya kula kutokana na uasilia wake.
Pia, Watu wanaocheza michezo mbalimbali, huwasaidia kuwaondolea uchovu na kuwaongezea nguvu wawapo uwanjani.
Yanazuia Upungufu wa Maji
Mwilini.
Yanaimarisha ubongo na misuli
Maji ya madafu pia yanasaidia kuzuia
muonekano wa kizee
(anti-aging ): Matumizi ya mara kwa
mara ya maji ya madafu
yatakufanya uonekane kijana
hata kama umri wako umeenda.