Faida ya maandamano ya cdm!sukari leo sh 1500 kutoka sh 2000!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Jamani nguvu ya umma imeanza kuzaa matunda kwani kiwanda cha kilombero kupitia kampuni ya ilovo dar imetangaza sukari itakua sh 1500 kg.source nipashe leo
 
Mkuu.
Tumeandama ili bei ya sukari ishuke? Na ni sukari peke yake?
Kama ni sukari peke yake basi kweli watanzania ni watu poa.

yaani watu wanajipongeza kwa kushuka kwa bei ya sukari ambayo haikutakiwa ipande...tuna safari refu.
bei ya umeme vipi? Lini itateremka?
na nauli za daladala na mabasi yaendayo mikoani lini zitateremka?

Ziteremke na bidhaa nyengine...petroli, diseli pia hapo nguvu ya umma ndio itakuwa imezaa matunda.
Watanzania ni wasahaulifu...hujaaamini bado?
Haya mkuu "nguvu ya umma imeanza kuzaa matunda!!!"

Jamaa "wanatuchakachua" akili, tumeanza kufikiri katika mwelekeo wanaoutaka. wanataka bongo zetu zilale.
Wao watajisifia kuwa wamedhibiti bei ya sukari isipande! Haya ndio "maendeleo"
Haya ndio "maisha bora kwa kila mtanzania"...sukari sh.1500 tu.
 
Jamani nguvu ya umma imeanza kuzaa matunda kwani kiwanda cha kilombero kupitia kampuni ya ilovo dar imetangaza sukari itakua sh 1500 kg.source nipashe leo

Kweli we Bongolala, JK ndo alikua anataka bei ya sukari ishuke
.
CDM tuna issue na hali ya uchumi kwa ujumla wake, ajira, inflation, kuporomoka kwa Tsh, Ufisadi nk. . . . .sio tu bei ya sukari!
 
Jamani nguvu ya umma imeanza kuzaa matunda kwani kiwanda cha kilombero kupitia kampuni ya ilovo dar imetangaza sukari itakua sh 1500 kg.source nipashe leo
hiyo ndiyo kilombero sugar!...no difference
 
Jamani nguvu ya umma imeanza kuzaa matunda kwani kiwanda cha kilombero kupitia kampuni ya ilovo dar imetangaza sukari itakua sh 1500 kg.source nipashe leo
Bei ya Sukari bado tishio Dar

Agizo la Serikali la kuwataka wafanyabiashara ya sukari kutouza kilo moja kwa zaidi ya Sh. 1700 limegonga mwamba ambapo hadi sasa bado bidhaa hiyo inauzwa kati ya Sh. 1800 hadi Sh. 2000 kutegemea na eneo jijini Dar Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam umebaini kuwa agizo hilo la serikali ambalo lilitolewa na Rais Jakaya Kikwete limepuuzwa na wafanyabiashara hao.

Wafanyabiashara hao walisema kinachowafanya wauze kwa bei ya zaidi ya Sh. 1,700 ni kutokana na wao kununua mfuko mmoja wa kilo 50 kwa kati ya Sh. 84,000 hadi Sh. 90,000.

Kauli ya serikali imeonekana kuzua mkanganyiko kwa kuwa wafanyabiashara wanadai kwamba endapo wakiuza kwa bei ilipendekezwa na serikali hawatapata faida.

Uchunguzi huo uliofanywa katika maeneo ya Mbezi Beach, Mwenge, Sinza na Makongo ulibaini kuwa sukari inauzwa kwa bei ambayo inapingana na aliyosema Rais Kikwete.

Hivi karibuni bei ya sukari imekuwa ikipanda siku hadi siku huku juhudi za serikali za kutaka ishuke zikigonga mwamba.

Serikali iliwaagiza wafanyabishara kushusha bei huku ikishindwa kuviagiza viwanda na wasambazaji wakubwa kutouza kwa bei ya juu.
CHANZO: NIPASHE 15th March 2011 :: IPPMEDIA
 
huyo jamaa anayeponda suala la sukari akitaka na vitu vingine vishuke ana matatizo huyo na nahis ni punguan, kwan mtoto akizaliwa anaanza kutembea kwanza? sasa c taratibu jaman vitu vingine vitashuka jaman wadau, tumetoka kanda ya ziwa then tukienda southern zone tutashughulikia mengine, usiwe na papara kaka, tulia mambo mazuri yanakuja, CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
 
Ukununua soda dukani ni TShs.500. Ukienda baa za hali ya chini ni TShs. 600. Ukiingia baa za hadhi ya juu bei ni zaidi ya 700. Bei za bidhaa zinategemea na mazingira ya eneo unalofanya shopping, Huwezi kukuta duka lina "Car parking, mlinzi wa kukulingia gari" halafu bei ya bidhaa iwe sawa na dukani kwa Mpemba; lazima ulipie gharama za parking na mlinzi indirect.
 
huyo jamaa anayeponda suala la sukari akitaka na vitu vingine vishuke ana matatizo huyo na nahis ni punguan, kwan mtoto akizaliwa anaanza kutembea kwanza? sasa c taratibu jaman vitu vingine vitashuka jaman wadau, tumetoka kanda ya ziwa then tukienda southern zone tutashughulikia mengine, usiwe na papara kaka, tulia mambo mazuri yanakuja, CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
haya ni maneno ya mafisadi.........Sisi ni Pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
 
Kama hizi habari ni za kweli basi :whoo:nchi hii haiwezekani kunyooka bila ya maandamano halafu CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao wanadai Chadema wanatishia amani nchini! Nasema washindwe nao mpaka walegee!
 
huyo jamaa anayeponda suala la sukari akitaka na vitu vingine vishuke ana matatizo huyo na nahis ni punguan, kwan mtoto akizaliwa anaanza kutembea kwanza? sasa c taratibu jaman vitu vingine vitashuka jaman wadau, tumetoka kanda ya ziwa then tukienda southern zone tutashughulikia mengine, usiwe na papara kaka, tulia mambo mazuri yanakuja, CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!

huu sasa upum***vu!kwani toka lini sukari imekuwa mafuta ama umeme hata kushuka kwake utarajie kushuka kwa bidhaa na huduma nyingine?Tuache ushabiki wa kijinga jamani!
 
Tunachotaka sasa ni Jk kujiudhuru kwa kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei na gharama za maisha. na c kufuraia tu kushuka kwa bei ya sukar
 
Back
Top Bottom