Faida ya Maamuzi ya CCM yanayokandamiza Wananchi kwa Upinzani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya Maamuzi ya CCM yanayokandamiza Wananchi kwa Upinzani.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Apr 22, 2012.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wana JF nimeona nifanye analysis ya maamuzi ya kisanii yanayofanywa na CCM pamoja na JK wake.

  1. Ni faida kwa CDM, kama CCM watakomaa na kuwang'ang'ania mafisadi wake kwani kila wakilipuliwa jukwaana lazima tuwapate wananchama wengi huko tunakoenda kwani kuanzia juzi hadi leo hii CDM imeshajikusanyia wanachama na wafuasi wengi kutoka CCM na wananchi wengi wa Kawaida.
  Mfano:
  a. Bungeni======= Wabunge watano waliosain kura ya kutokuwa na imani naye, Tutakuwa na wabunge hao na
  wapiga kura wao.
  b. NEC ya CCM=== Wajumbe Kama wawili hadi sasa wanaiunga mkono CDM, James Milya na
  Makongoro Nyerere (Freemedia ya Jana ilimhoji kuwa kama si CDM mafisadi ndani ya CCM
  wasingemchagua) Makongoro Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara.
  c. Madiwani:==== Mpaka sasa CDM ina madiwani wasiopungua kumi kutoka CCM katkia maeneo ya Arusha,
  Sengerema, Geita, Monduli etc na wanazidi kujiunga na CDM kila kukicha.
  d. Wanachama wa kawaida ndiyo usisema, karibu kila Mkutano CDM inagawa kadi kwa wananchama wapya kati ya
  1000 na 2000


  2. Ni faida kwa wananchi na CDM kama CCM ingewaondoa mawaziri wale maana hadi ngazi ya Chini wangeogopa kufuja mali za wananchi kwa sababu wanajua watawajibishwa na wakubwa zao hasa mawaziri na makatibu wakuu.

  3. Sasa kutokana na JK mwenyewe kukataa na kudai wizi woote uliofanywa na mawaziri na viongozi walioko chini yao kama kule TBS, MSD, etc hii ina maana JK MWENYE ANAJUA KILA KINACHOENDELEA NA WIZI HUU NA KAUBARIKI KWAHIYO ANAONA ITAKUWA KAMA ILE WIZI WA RICHMOND, NA HAPA TUSIMTAFUTE MCHAWI, MCHAWI WETI RAIS WETU JK.
   
Loading...