Faida ya kukamatwa kwa mkurugenzi wa JF kwa JF

df1e3f6db1d32332672b401358e811a7.jpg


Kwanza tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Kanisa la Katoliki haswa kwa Papa Fransis kwa jitihada zake za kutafuta Amani na suluhisho la kudumu huko nchini Congo. Ndugu zetu Wakongo wameteseka vya kutosha.
Hizi ndio huduma za Kidini halisi Mwenyezi Mungu anazozipenda. Hizi jitihada zinastahiki pongezi. Huu ndio Utawala Bora. Hawa ndio "Genuine Religious Leaders". Hawa ndio watu wa Mungu. Huu ndio Ubinaadamu. Asante Papa Fransis.

Kinyume cha Suluhisho ni kuchochea, kinyume cha Ubinaadamu ni Unyama.

Kanisa la Katoliki lilimtukuza Mwalim Nyerere na kumuona kama "Mtakatifu".

Wanaodai kuwa wao wanafuata nyayo za Mwalimu Nyerere, waangalie kauli zao na vitendo vyao vizuri.
Mwanzilishi wa Taifa letu Julius Kambarage Nyerere hakuwa na tabia za Kidikiteta. Kiongozi Nyerere alikuwa ni Mwana Mapinduzi. Tofautisha "Udikiteta na Uana-Mapinduzi". Mpiganiaji Uhuru Nyerere alipinga Dhuluma, Unyanyaswaji, Ukabaila, Utumwa na Unyonyaji. Mzee Nyerere hakutawala kwa "Hamu Binafsi". Komredi Nyerere hakukubaliana na kusheherekea Ukandamizwaji wa Wapalestina. Muheshimiwa Nyerere alisimama na kuunga mkono harakati za Ukombozi wa watu wa Palestina, Kusini mwa Afrika na wana Sahara Kaskazini. Baba wa Taifa Nyerere alimuunga mkono Patrice Lumumba na kupinga vitendo vya wanausalama wa Zaire wanaopoteza Waafrika. Yeyote yule aliyetafuta haki za Kibinaadamu, enzi ya Mkombozi Nyerere, Tanzania ilikuwa ni nyumbani kwake.

Kukamatwa na kushitakiwa kwa Max Melo Mkurugenzi wa JF, (Mwananchi anayetafuta riziki yake kwa halali na mlipaji kodi), kumedhihirisha Upoteaji wa Utakatifu wa Mw Nyerere katika Taifa letu. Tunaiomba Mahakama yetu Tukufu kutupilia mbali mashitaka hayo. Mfuko wa kusaidia gharama za utetezi kutoka kwa wahisani utengwe.

Kipato kizuri kinategemea maarifa na juhudi zetu pamoja na bahati zetu lakini "Ubinaadamu", kumpa Mwanadamu heshima yake ni kitu cha bure. Tunaogopa Tanzania kuambukizwa jinamizi la chuki linalotanda huko katika nchi za maziwa makuu.
Kuna dalili ya tabia na harufu ya spirit hiyo hapa Tanzania.
Watu walifukiziwa roho mbaya ya "Ubaguzi, Ukabila au Udini na Udikiteta" hawawezi kuwa ndio Role Model kwa Taifa lilobarikiwa na kupata Uhuru wake bila kumwaga damu.
Sayansi inadhihirisha haya kupitia "Sociology". Wanasayansi mtatuambia ukweli huu.

Utamaduni wa Chuki na Spirit ya "Roho Mbaya" itazimwa na Ubinaadamu. Binaadamu yeyote anahitaji "Ubinaadamu".

Tukatae Political Anatomy za "Ubaguzi, Udini, Ukabila na Udikiteta".
Nembo ya Taifa letu ni "UHURU NA UMOJA".

Kuna harufu nzuri nzuri kutoka kwenye nchi kama Botswana, makao Makuu ya SADC, kwanini tusichukue manukato hayo? Na ni hii Tanzania ndio waanzilishi wa manukato haya mazuri yanayoyonukia katika Mataifa ya Kusini mwa Afrika.

"I Write What I like".
Long Live The Spirit of Bantu Stive Biko.
 
Prof.bwana yule hana mchango.katika hii ishu?maana nae katwangwa humu
 
Kwanza naamini tuko salama kwa Neema za Mungu na wale wasio amini uwepo wa Mungu nao pia wako salama... Na kama una changamoto yoyote basi juwa ni mambo ya mda tu na yatapita na itakuwa ni historia.

Mchugaji wangu huwa anasema, "mara nyingine Mungu hutumia changamoto hizo hizo kuleta matokeo mazuri unayohitaji'..mfano kwa wana wa israel pale bahari ya shamu ilipotumika kuwamaliza maadui zao ili hali ilikuwa ndio jaribu lao kubwa na walihisi ndio mwisho wa maisha yao.

Nimefikiria sana toka taarifa za kukamatwa kwa mkurugenzi wa mtandao huu.ila bila kujuwa nikaanza kuwaza juu ya mchugaji Gwajima na watu wengine hasa pale wanaposhika vichwa vya habari.kwani kila wanaposhika vichwa vya habari hasa magazeti baada ya hapo utasikia wiki hii watu walifulika sana.kumbe kwa kufanya hivyo huwa ndio kuna wafanya wajulikane na watu wanaanza kuwafatilia kwa ukaribu zaidi.

Kwahiyo kwa sababu nilizozieleza hapo juu,kwa upande wa faida,kuna faida kubwa kwa kukamatwa kwa mkurugenzi wa JF.kama ifuatavyo:

Kujulikana na kutangazwa kwa JamiiForums bure ulimwengu mzima. Kama tunavyojua vyombo vya habari vikubwa vimetangaza mtandao huu zaidi ya mara moja na hivyo kufanya watu wengi zaidi kutaka kuujua kiundani mtandao huu na hivyo ineongeza viewers wengi zaidi ya sisi milioni mbili wa kila mwenzi kwa hivyo naamini hata mapato huenda yakaongezeka mwezi huu.

Tunajisikia tupo salama zaidi. Kumbe imedhihirisha wazi kuwa watumiaji wa mtandao huu tupo salama kwa taarifa zetu za muhimu na kama hujawahi kutoa mawasiliano yako kwa hiari. Kumbe hakuna mtu anayeweza kukupata.

Ujasiri wa mkurugenzi. Imeonyesha wazi kuwa ofisi ya JF iko imara katika kutetea wateja wake na yupo tayari kwa lolote lakini sio kutusaliti kirahisi tu. Kweli serikali ni serikali haishidwi kirahisi kama ikiamua jambo lakini mpaka sasa mkurugenzi amejitajihidi.

Yapo mengi ila mimi niishie hapo lakini unaweza kuongezea. Natambua wakati anaopitia lakini nimewaza upande wa pili.
Umeongea kweli tupu.
 
Back
Top Bottom