Faida ya kukamatwa kwa mkurugenzi wa JF kwa JF

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,297
2,000
Kwanza naamini tuko salama kwa Neema za Mungu na wale wasio amini uwepo wa Mungu nao pia wako salama... Na kama una changamoto yoyote basi juwa ni mambo ya mda tu na yatapita na itakuwa ni historia.

Mchugaji wangu huwa anasema, "mara nyingine Mungu hutumia changamoto hizo hizo kuleta matokeo mazuri unayohitaji'..mfano kwa wana wa israel pale bahari ya shamu ilipotumika kuwamaliza maadui zao ili hali ilikuwa ndio jaribu lao kubwa na walihisi ndio mwisho wa maisha yao.

Nimefikiria sana toka taarifa za kukamatwa kwa mkurugenzi wa mtandao huu.ila bila kujuwa nikaanza kuwaza juu ya mchugaji Gwajima na watu wengine hasa pale wanaposhika vichwa vya habari.kwani kila wanaposhika vichwa vya habari hasa magazeti baada ya hapo utasikia wiki hii watu walifulika sana.kumbe kwa kufanya hivyo huwa ndio kuna wafanya wajulikane na watu wanaanza kuwafatilia kwa ukaribu zaidi.

Kwahiyo kwa sababu nilizozieleza hapo juu,kwa upande wa faida,kuna faida kubwa kwa kukamatwa kwa mkurugenzi wa JF.kama ifuatavyo:

Kujulikana na kutangazwa kwa JamiiForums bure ulimwengu mzima. Kama tunavyojua vyombo vya habari vikubwa vimetangaza mtandao huu zaidi ya mara moja na hivyo kufanya watu wengi zaidi kutaka kuujua kiundani mtandao huu na hivyo ineongeza viewers wengi zaidi ya sisi milioni mbili wa kila mwenzi kwa hivyo naamini hata mapato huenda yakaongezeka mwezi huu.

Tunajisikia tupo salama zaidi. Kumbe imedhihirisha wazi kuwa watumiaji wa mtandao huu tupo salama kwa taarifa zetu za muhimu na kama hujawahi kutoa mawasiliano yako kwa hiari. Kumbe hakuna mtu anayeweza kukupata.

Ujasiri wa mkurugenzi. Imeonyesha wazi kuwa ofisi ya JF iko imara katika kutetea wateja wake na yupo tayari kwa lolote lakini sio kutusaliti kirahisi tu. Kweli serikali ni serikali haishidwi kirahisi kama ikiamua jambo lakini mpaka sasa mkurugenzi amejitajihidi.

Yapo mengi ila mimi niishie hapo lakini unaweza kuongezea. Natambua wakati anaopitia lakini nimewaza upande wa pili.
 

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,561
2,000
Taarifa zingetolewa huenda [HASHTAG]#Lizaboni[/HASHTAG] angeukwaa..ila wengine wangetafuta million saba za mdhamana..
 

kajunju

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
1,001
1,500
mimi kila saa 1 nachungulia kuona vitu vipya. baba jeskaz a.k.a sizonje ataaibika tu. hivi huwa aombi ushauri kwa akina kikwete? jtatu tuanze kuchimbua maburi ya wapelelezi wote walioshikilia kesi hii. hii itafanya waitambue zaidi JF kwa kuwaanika uchafu wao
 

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,297
2,000
sina shaka na MEX, Wahaya kama hawa huwa tunawaita "KYOMA" maana yake chuma cha pua
Nashangaa wakati kesi na mahakimu ndio walianzia kwao...wahanya hawana muda wa kupayuka wala kurusha ngumi
.kwani wao chakula cha nguvu mwiko kwa sababu ya ndizi..lakini ukimpeleka kwenye sheria ndio mahali pake pa kukuonyesha ubabe wao...kwani hautaona anarusha jiwe ila cha moto utakiona
 

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,297
2,000
Juzi kuna watu kama kumi walikaa pamoja wakawa wanaongea kuhusu JF, nilichogundua ni kuwa walikuwa hawana uelewa vema nami sikufanya kosa nikawaeleza kinaga ubaga. Nadhani nao watakuwa wajumbe wazuri huko.
Safi sana umeongeza member tayari 7bu ya kesi tu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom