Uchaguzi 2020 Faida nyingine kwa Tundu Lissu, anabebwa na mkoa anaotoka

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,151
33,332
Kwa Mara nyingi kwa miaka mingi CCM wamekua wakipiga propaganda mfu juu ya VIONGOZi na wagombea wa CHADEMA kuwa ni wa kutoka Kaskazini.

Sasa faida kubwa aliyonayo Tundu Lissu na CHADEMA ni sehemu anayotoka na Uraia wake pia.

Lissu anatoka katika Mkoa ambao haulaumiwi, hauogopwi, hauchukiwi wala haupigwi vita kwa chochote kama mikoa ya kaskazini (ingawa chuki hizo ni ujinga na Ukaburu tu.)

Lissu anatoka Singida. Mkoa wa Singida upo katikati ya Tanzania. Tundu Lissu hana utata wa Uraia.

Kwa Mkoa anaotoka Lissu hakuna mtu anaweza kumchukia kwa sababu Watanzania hupenda kuongozwa na Rais atokaye katika makabila yenye idadi ndogo ya watu.

Kama Wazanaki, Wazaramu, Wakwere na Wamakonde.

Kwa kifupi Lissu anabebwa na uraia wake na Mkoa anaotoka.
 
CCM kwa sasa ni intarahamwe wa Tanzania- Miaka 59 na bado tu wamo wanang'ang'ania Kuongoza , labda hadi yesu arudi ndio wataacha si waluhusu basi mawazo mbadala... wakubali kuridhika na uongozi wa miaka 59 iliypita ...wamekuwa nongwa sana kwa watu wa 1980 hawa ccm kwa kweli...
 
Na inapendeza Rais akitoka kwenye kabila dogo kuliko livyo sasa ambapo Wasukuma wanaona kama hii nchi ni yao peke yao.
Bomoabomoa za Nyumba za wananchi hazifanyiki Mwanza.
Nyadhifa kubwa wanapewa Wasukuma tu.
Kule Chato ndio usiseme kila wakitakacho kitajengwa kuna siku watatamani Hifadhi ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro vihamishiwe Chato.
 
acha kufananisha mada za Lisu na utopolo wa Lumumba. Mimi nyuzi za kuisifia ccm hata sijisumbui kufungua.
Kwanini mada nzuri nzuri kumhisu Lisu zimeongezeka kuliko za ccm kueleza kazi walizozifanya katika miaka 5?
 
CCM wana hali ngumu sana kipindi hichi.

Hivi mtu mwenye akili timamu unaachaje kumpigia kura LISU?
Mtu mwenye akili timamu ataachaje kumpigia kura Magu ? Mnafikili Urais ni kama kuokota Dodo chini ya muembe ?.. Mtu kakaa Belgium huko karibu miaka mitatu, hajui shida za watanzania , alafu simply tu eti watu wamchague kwa kipi hasa ,!. Hatutoi kura kwa simpathy , aeleze atafanya Nini zaidi ya alichofanya JPM ndo tumpe kura.
 
Back
Top Bottom