kabila01
JF-Expert Member
- Apr 21, 2009
- 4,235
- 4,949
Nawasalimu kwa jina la jamhuri
Mwaka jana mwezi wa kwanza nilipanda migomba kama 30 katikaeneo la nyumbani napoishi. Kabla ya kupanda niliwauliza wataalamu hasa watu wanaotokea maeneo ambayo wanalima sana ndizi kama Moshi, Bukoba na Tukuyu kujua aina za ndizi na matumizi yake na namna ya kupanda. Baada ya kupata maelekezo ya kitaalamu nikapanda aina zifuatazo za ndizi.
1. Mzuzu hii niliambiwa inafaa sana kukaangwa au kuchomwa
2. Bukoba hii kwa kupikwa
3. Mshale hii kwa supu
4. Malindi hii inafaa kuliwa ikiwa mbivu
5. Kisukari vile vidogo hivi navyo vinafaa kuliwa vikiwa vimeiva
6. Matoke hizi kwa kupikwa
Faida nayoipata kwa sasa;
1. Mazingira ya kuzunguka nyumba yangu yanavutia maana ni green tupu pamoja na kua tumeanza kiangazi
2. Nina chakula cha kutosha imenilazimu kununua fridge ya ziada ili ndizi zingine nizi freez humo maana zimenizia
3. Kipato changu (thamani ya shilingi kwangu imeimarika maana nimepunguza kwa kiasi kikubwa kutoa pesa nje kwa ajili ya kununua mahitaji )
4. Ninatoa sadaka hasa kwa wale ambao wanashida ya chakula angalau ninawapa ndizi kidogo kama sadaka na napata baraka kutoka kwa Mungu
NB
Kwa wale ambao tuna maeneo makubwa tumejenga basi tupande angalau migomba itatusaidia kuliko kujaza pavement na ukoka kwenye nyumba.
Kwa wale wanaotegemea kununua maeneo ya kujenga nawashauri mtoke kidogo nje ya mji mpate maeneo ambayo yatawawezesha kulima kidogo na kufuga.