Faida na madhara ya kuoga kwa maji ya moto

Dah we mtu wew umejibu vizuri sanaaa ..
kwa mwanaume kuoga maji ya moto sana sio vzuri coz zile testies(mapu...) haztakiwi kupata joto sana coz ztashindwa kuzalisha mbegu ndo maana haziko ndani ya mwili coz ndan ya mwili joto huwa ni kubwa so ukiogea maji ya moto sana unaongeza external temperature ambayo inadestroy zile mbegu znazozalishwa na testies hope umenipata fresh.
 
Hakuna.kitu kama hicho basi hata nguo tunazovaa kwa ajili ya kujisitiri utupu wetu huwa zinaleta joto tofauti na maji kuoga huwa yanapita tu wala hata hayakai sekunde mbili wakati nguo ni muda wote sasa kipi kinatakiwa kiwe na madhara
 
Habari zenu wana jf,mimi ni mdau mkubwa sana wa kuoga maji ya moto na nimekuwa addicted kuoga maji ya moto for almost 4 years now. So nauliza je kuna madhara gani Kiafya kuoga maji ya moto for a long tym?, Nb:naishi Dar
nguvu za kiume
ngozi kuzeeeka
 
kama tukipata sababu za kisayansi itasaidia zaidi lakini nadhani hata kunywa yana madhara.....niliwahi kunywa sana maji ya moto wakati niko high schoo wakawa wananiita mahot....nadhani kuna athari nilipata
Ambayo huijui mpka sasa??kama bado unadhani basi ujue haina madhara maana wewe ndo ungetoa ushuhuda hapa.
 
Mimi naona hayana madhara. Mimi nimeyaogea muda mrefu yaani miaka zaidi ya 20. Hapa nilipo nina umri wa 49 sioni tatizo.Hiyo kokoliko anayoisema jamaa yangu bado ni kali tu. Any way! labda madhara mengine.Maji ya baridi kwa wale wanaoogea kama in case una presha ya kushuka ni hatari sana.
 
1579067773667.png


Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.

Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo.

Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo.

Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji ya moto angalau mara tatu kwa wiki

Kulainisha na kutunza ngozi
Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.

Usingizi
Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usinngizi.

Kukuweka katika hali nzuri
Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.

Kuchangamsha ubongo
Unapooga kwa kutumia maji ya moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.

Kushusha shinikizo la damu
Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.

Kusaidia mzunguko wa damu
Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.

Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kutooga kwa maji ya moto sana kwani huathiri ngozi.


 
Labda nikiwa Siberia au Alaska, kwingine kote ni maji ya baridi, tena bila ya kupiga kelele, kimya kimya bafuni.
 
Back
Top Bottom