Fahamu zaidi kuhusu kinga ya Ukimwi iitwayo PEP

Kaboom

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
10,828
14,975
PEP (Post - Exposure Prophylaxis) ni matibabu anayopewa mtu after been exposed to HIV ili kukukinga kuwa HIV positive.

Matibabu haya yanatakiwa kutolewa as soon as possible baada ya mtu kuwa exposed na HIV (ndani ya masaa 72) i.e kama zishapita siku tatu( masaa 72) matibabu haya hayawezi kufanya kazi

Matibabu haya hutolewa kwa muda wa mwezi mmoja (4weeks).

Swali: Mbona hiki kitu akizungumziwa sana na watoa huduma ya afya na wadau wanaohusika na mapambano dhidi ya ukimwi?

Je, ni gharama ama kuna side effects kubwa?

1596800309955.png


Ufafanuzi wa kina kuhusu (PEP)

PrEP ni nini?
Pre-exposure prophylaxis (PrEP) inamaanisha matumizi ya kila siku ya dawa za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV kwa mtu ambaye hana virusi hivyo, lakini yumo katika hatari ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi vya HIV.

PrEP ina ufanisi wa kiwango kipi?
Ikitumika kuambatana na maagizo, PrEP inaweza kupunguza hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV kwa zaidi ya asilimia tisini (90%). Hata hivyo, kwa sababu haikupi kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa au mimba zisizotarajiwa inapaswa kutumiwa pamoja na kinga za aina nyingine kama vile mipira ya kondomu.

PrEP huzuia virusi HIV vipi?
Ukitumia dawa za kukinga maambukizi ya virusi vya HIV (PrEP) kulingana na maagizo uliopewa, dawa hizo hujenga kizuizi ambacho huzingira seli za mwili ili kuzilinda kutokana na maambukizi.Kwa mfano,ukijihusisha na tendo la ngono na mtu aliye na virusi ama kugusa majimaji kutoka kwa mwili wa mtu aliye na virusi vya HIV,PrEP inaweza kuzuia virusi kusababisha maambukizi mwilini mwako.

PrEP ina manufaa gani?
Ukitumia PrEP kwa kuzingatia maagizo uliyopewa,unaweza kupunguza kwa kiwango kubwa hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV ,na kwa hivyo kukupa amani moyoni mwako.Hata hivyo, kwa sababu haikupi kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa mengine ya zinaa au mimba zisizopangwa,inapaswa kutumiwa pamoja na njia zingine za kinga kama vile kondomu kila wakati.

Dawa za PrEP zina athari gani?
Baadhi ya watu wanaotumia dawa za PrEP, huadhirika japo tu kwa
muda mfupi.

Ningali na kinga dhidi ya HIV nikikosa kumeza tembe
moja ya PrEP?

Ukikosa kumeza tembe moja au zaidi,unapunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wa PrEP kukupa kinga kamili dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV.Utafiti
umeonyesha kuwa PrEP hukupa kinga bora dhidi ya HIV ikitumiwa kila siku kuambatana na ushauri wa mhudumu wa afya.

Tembe ya dawa za PrEP hutumiwa namna gani?
• Meza tembe moja kwa siku.

• Unahitaji kuzitumia kwa takriban siku saba kabla ya kujihusisha na tukio lolote ambalo linakuweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.

• Endelea kutumia dawa hizo kama ungali katika
hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.

Nifanye nini nisipomeza tembe ya PrEP kwa siku moja?
Meza tembe moja pindi unapokumbuka na kisha uendelee kumeza jinsi ulivyoshauriwa na mhudumu wa afya.

Nani anaweza kutumia PrEP?
Mtu yeyote ambaye hajaambukizwa virusi vya HIV lakini yumo katika
hatari kubwa ya kuambukizwa.

Ama kama una mpenzi ambaye:
• Anafahamika kuwa na virusi vya HIV lakini hatumii dawa za
kupunguza makali ya virusi vya HIV (ARVs)

Aidha:
• Anatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV bila kuzingatia maelezo ya kuzitumia na kwa hivyo mwili wake haujafaulu kukandamiza virusi.

Na pia ikiwa:
• Una mpenzi au wapenzi ambao hawaijui hali yao ya HIV
• Una zaidi ya mpenzi mmoja
• Unaugua magonjwa ya zinaa mara kwa mara
• Unatumia dawa za kulevya za kujidunga
• Unashiriki ngono ili kupokea zawadi za fedha au zawadi za aina nyingine
• Unatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV mara kwa mara baada ya kujihusisha na mambo yanayokuweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV
• Mtu anayenuia kupata mtoto lakini yumo kwenye ndoa ambapo mmoja ana virusi vya HIV
• Hautumii mipira ya kondomu kila wakati au wakati mwingine unasahau kutumia unaposhiriki ngono
• Mtu ambaye mara kwa mara mipira ya kondomu hupasuka wakati anashiriki tendo la ngono
• Mtu ambaye ameshindwa kumshawishi mpenzi wake kutumia mipira wa kondomu ingawapo haijiui hali yeke ya HIV. Kwa maelezo zaidi tafuta ushauri kutoka kwa mhudumu wa afya.

Naweza gawa tembe za PrEP kwa watu wengine?
Usishiriki dawa zako na mtu mwingine, PrEP inapaswa kutumiwa na mtu aliyepata ushauri huo kutoka kwa mhudumu wa afya.

Ikiwa natumia dawa za PrEP,naweza kuacha kutumia mipira ya kondomu ?
Haupaswi kuacha kutumia mipira ya kondomu. PrEP sio chanjo.

Kuna tofuati gani katika ya dawa za kuzuiamaambukizi kabla ya tukio la hatari (Pre-Exposure
Prophylaxis) na zile za kuzuia maambukizi baada ya tukio la hatari Post-Exposure Prophylaxis (PEP)? Ingawaje PrEP na PEP hutumiwa na watu ambao hawana virusi vya HIV ili kuzuia maambukizi,dawa hizo ni tofauti.

PrEP inatumika kabla ya tukio ambalo linaweza kusababisha hatari ya
kuambukizwa virusi vya HIV ilikupunguza uwezekano wa maambukizi.PEP
inatumika baada ya tukio ambalo huweka mtu katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV kabla ya masaa 72 hayajapita.

HIV Tukio ambalo huweka mtu katika hatari ya kuambukizwa Siku 7 Kabla masaa 72 hayajapita PrEP PEP

Dawa za PrEP zinazuia magonjwa ya zinaa na mimba?
Dawa za PrEP hazina uwezo wa kuzuia magonjwa mengine ya zinaa
wala mimba zisizotarajiwa. Dawa hizo zinapaswa kutumiwa kwa pamoja
na mipira ya kondomu .

Wanawake ambao wanatumia dawa za PrEP lakini hawako tayari kushika mimba,wanapaswa kutumia mbinu nyingine za kupanga uzazi.

Baadhi ya michango muhimu kutoka kwa wadau waJF
Lengo kubwa la PEP ni kukinga watoa huduma za afya dhidi ya maambukizi baada ya kupata majeraha wakati wa kutoa huduma. Majeraha haya yanahusisha kumwagikiwa damu, kujichoma sindando, ama kujikata na vitu vyenye ncha kali wakati wakitoa huduma.

Huduma hii pia hutolewa kwa watu waliobakwa kama kinga ya virusi.

WHO | Post-exposure prophylaxis (PEP)

Post-exposure prophylaxis (PEP) is short-term antiretroviral treatment to reduce the likelihood of HIV infection after potential exposure, either occupationally or through sexual intercourse. Within the health sector, PEP should be provided as part of a comprehensive universal precautions package that reduces staff exposure to infectious hazards at work.

Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection, Fact sheet - 1 December 2014

Key facts
WHO | Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection

Globally, there were an estimated 35 million people living with HIV, of whom 13 million were on antiretroviral treatment (ART) at the end of 2013.

People can be accidentally exposed to HIV though healthcare work or due to exposures outside healthcare setting, for example, through unprotected sex or sexual assault.

Antiretrovirals (ARVs) have been used to prevent infection in case of accidental exposures for many years. This intervention is called post-exposure prophylaxis (PEP) and involves taking a 28-day course of ARVs.

PEP should be offered, and initiated as early as possible, for all individuals with an exposure that has the potential for HIV transmission, and ideally within 72 hours.

If started soon after exposure, PEP can reduce the risk of HIV infection by over 80%. Adherence to a full 28-day course of ARVs is critical to the effectiveness of the intervention.

Recent evidence shows PEP uptake has been insufficient: only 57% of the people who initiated PEP have completed the full course and rates were even lower at 40% for victims of sexual assault.
----
Hapo tatizo lako litakuwa ni kuona au kuambiwa lakini usijue au usielewe uhalisia wa kilichotokea.Maswali kama haya nilishaulizwa sana na usifikiri kwamba kuna utata hata kidogo.Cha msingi ni kujua kwa undani historia nzima na aina ya maisha ambayo wapenzi hao walikuwa wanaishi.

Sasa ili niweze kujibu swali lako,nahitaji mfano ulioshiba taarifa sahihi ili niweze kukwambia kwa nini hilo lilitokea,vinginevyo itakuwa ni hisia tu.Kuna uwezekano mkubwa watu hao watakuwa wametumia ARVs wote wawili.Pia umeshasahau kwamba vipimo vya HIV vinaweza pia kutoa majibu ya HIV+ kwa mtu yeyote yule hata kama hajawahi kushiriki ngono au kuchangamana damu na mtu mwingine,ndio maana nikakwambia vipimo ni mojawapo ya kanyaboya ambalo waliotudanganya wanatumia ili kurubuni akili zetu ili tuweze kutumia dawa zao zenye sumu ambazo ndio zinatuangamiza huku tukimsingizia HIV ambaye ni hewa.

Mimi pia kuna familia ninaifahamu,baba,mama na mtoto wao mchanga walikufa kwa dalili moja.Baada ya kuchunguza kumbe wote walikufa kwa TB.TB huambukizwa kwa njia ya hewa,baba,mama na mtoto hulala kwenye kitanda kimoja kila siku,nadhani unaelewa namaanisha nini.Mwenye TB ni rahisi kumpima HIV+ kutokana na sayansi ya vipimo vya HIV ilivyo.Hii ni case study moja tu ya mfano ambayo ninaijua kwa undani.Sasa inabidi ulete case study ambayo una taarifa za kutosha ili tuijadili,vinginevyo utakuwa unatumia hisia tu,na hapo ndipo maana ya HIV/AIDS kuitwa mindset disease inapokuja.
----
Nimechanganyikiwa mana nimepasukiwa na condom wakati tukifanya mapenzi ikabidi tukapime nikakuta kumbe mwenzangu ana VVU wamenipa dawa PEP. Imetokea leo asubuhi hayajapita masaa 24 nimemeza PEP

Je kweli zitanikinga?

Update
======

Nimepima tarehe 6/10/2017 nipo HIV negative, nina furaha saana maana nilitembelea rim, nimejifunza jambo kubwa saana katika maisha yangu....


================================
Ilivyokuwa

====!!!!!=====
Alikuja kunitembelea toka mkoani tarehe 21 June 2017, tunagegedana kwa kinga, siku hiyo ya tarehe 21 mara mbili kisha tukalala, Asubuhi kabla sijatoka tunagegedana, nikiwa nakaribia kufika climax condom ikapasuka, nikamalizia, Nilipomaliza nikapata hofu maana sikuwa najua status yake.

Nikamwambia tukapime alikubali tukaenda hospital kupima. Nikaona ana hofu japo amekubali ikabidi nisisitize kwenda ,tukaenda dispensary kupima.

Tulipofika tukatoa damu tukaambiwa tusubiri, Baada ya dakika 10-15 akaitwa akatolewa damu tena. Nikaanza kupata hofu.

Muda wa majibu ulipofika tukaitwa, kufika ndani baada ya mazungumzo na yule mtoa Ushauri yaliyodumu kwa nusu saa akauliza mpo tayari kupokea majibu!? Tukasema ndio, akasema "kaka hongera sana majibu yako ni mazuri hauna maambukizi, Dada unaishi na maambukizi ya virus vya UKIMWI".

Nikajieleza juu ya mkasa wa kupasukiwa na condom, wakanipa dose ya pep for 28 days.

Hizo dawa ni kali vibaya mno, zinalevya hatari yaani Unachoka unajihisi kuumwa, mawenge na ndoto za ajabu ajabu kila siku. Asee asikuambie mtu ni dawa strong sana.

Yule binti alikataa kuanza clinic, akadai yeye Si Mgonjwa hana maambukizi
----
View attachment 688059

Kama View attachment 688061

Habari zenu wanaJF,

Mwezi mmoja uliopita nilileta uzi kuhusiana na kutembea na binti mwenye VVU,

Lengo kuu la kutembea na huyo binti ilikuwa ni tamaa ya kutaka kupata mtoto hata nje ya ndoa kwani mke wangu hana uwezo wa kupata ujauzito! Nimeishi nae toka 2010 lakini mpaka sasa hajawahi kupata ujauzito.

Tulienda hospital zifuatazo kutaka kupata tiba na suluhisho lakini imeshindikana. Saint Gasper Itigi, Upendo hospital (Dodoma), Agha Khan (Dodoma), General hospital (Dodoma), CF (Mwanza), Kamanga (Mwanza), Sekuture (Mwanza), Bugando (Mwanza) kwa Dkt Mwaka ( mtaalamu wa tiba mbadala- Ilala Bungoni)

Huko kote sio tu alikuwa anapatiwa peke ake matibabu, lah hasha hata mimi nilikuwa napimwa sperm analysis, nakuonekana niko poa.

Kisa cha mke wangu kutopata ujauzito ndio kilichonipelekea kutoka nje ya ndoa.

Mara baada ya kutembea na huyu mdada niliamua kwenda kumpima ili tuanze rasmi safari ya kutafuta mtoto tukiwa tunajiamini sote.

Tulipoenda maabara, huyu binti aligundulika kuwa +, sikuamini, nikamchukua kwenda maabara nyingine, majibu yalikuwa yale yale tu yaani she was HIV positive.

Immediately nikaamua kwenda Angaza, nikapewa hizo (PEP) nikaambiwa nizitumie mwezi mzima kisha nipime tena baada ya kumaliza hiyo dozi.

Kiukweli dawa hizi zinamaudhi sana mwanzoni, ndoto za ajabu, njaa kuumua kupita kiasi na kichefuchefu.

Doz hiyo nimemaliza juzi, so nilikuwa najishauri kwenda kupima huku moyo mwingine ukisita lakini nikaamua bora niende tu liwalo na liwe, maana hakuna kitachobadilika kama nitakuwa nimeathirika ni bora nijijue mapema tu! Basi bwana, nikaenda maabara, nimepimwa na kukutwa mzima (negative), hakika sikuamini ilibidi nimwelezee huyo aliyenipima situation ilivyokuwa, akasema hiyo inawezekana ukatembea na mwenye HIV kama kutakuwa na maandilizi ya kutosha na kusitokee mchubuko basi ni nadra zana kuambukizwa kwa mtu aliye negative.

Napenda kumshukuru mungu kwa kuniepusha na hili janga, na safari yangu ya kutafuta mtoto nje ya ndoa, nimeifuta rasmi.

Najua nawachosha lakini hiyo ndio hali halisi.

Hapa chini ni kopo la hizo dawa na majibu yangu, Mara baada ya kupima Leo.


Onyo! UKIMWI HAUJARIBIWI!KONDOM NI MUHIMU SANA!
----
UKIMWI upo tena sana asikudanganye mtu ,kuhusu PEP nafikiri aim ni wameweka kwa wafanyakazi wa afya sababu wanakuwa exposed sna yan mfano hapa m nimeanza dose week iliyopita baada ya kumwagikiwa na damu pia wanapewa wanawake waliobakwa.

Mind you PEP ni Arvs so tunapewa msaada la sivyo hatuwez kuafford na ARVs zimeletwa ili kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa kufatilia wingi wa virusi vyake(viral load counts) sasa ukisema wapewe kila mtu hizi gharama sisi hatuwez

Antiretroviral therapy cost an average of$9360 per year for each patient with a CD4 cell count below 50 cells/mm3. This compared to average annual costs of between$11,800 and $12,313 for those with higher CD4 cell counts. Antiretroviral therapy was most expensive for those with the highest CD4 cell counts.

Angalia gharama hyo alafu jifikirie marambili
Mwaka jana ilizinduliwa research baadhi ya mikoa ambazo zimelewa pep za unakunywa siku7 ndo unaenda kudinyana sijajua research kama imeisha
----
Kama huyu jamaa aliyejiprick na sindano alipimwa alikuwa negative, ndipo akaanza kutumia PEP kama kizuizi cha kusambaa na kuongezeka kwa kimelea wa UKIMWI basi yule aliyesex naye atakuwa safe au nafasi ndogo sana kupata maambukizi.

Wewe uliye kwenye PEP endelea dose yako mpaka siku 30 zitimie. Na baada ya hapo hakikisha unapima tena kuangalia kama PEP yako imefanikisha kufubaza kimelea cha HIV. Yule anayepaswa kuwa hofu sana ni yule uliyesex naye bila kinga,ikiwa tu wewe ulikuwa mgonjwa kabla ya kujichoma sindano.

Kama ile sindano ilikuwa na vimelea na ulianza PEP ndani ya masaa 72 na UKAWA UNATUMIA SAWA SAWA NA MASHARTI YAKE, viral load itakuwa chini sana kiasi kwamba uwezekano wa kumuabukiza mwingine ni mdogo mnooo. Ondoa shaka, hakikisha tu unatumia kinga unapofanya ngono na upime tena baada ya zile siku thelathini ili kujua kama dawa imefanya kazi au imeshindwa.

Pole na asubuhi njema kwako
 
Ni ngumu kumeza ..tunaloweka.....mmedinyana jana hujui ka mwenzio anao...unakimbilia kupewa dawa ndani ya saa 72?

1. Unapima siku ya kwanza. Hakuna viashiria.

2. Unarudi baada ya mwezi/miezi3 ...kuthibitisha

Nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika
 
Nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika.

Si kila mkidinyana..ndo mana nikasema baada ya kuwa exposed na HIV( mf:umefanya mapenzi na muathirika na ukagundua mapema kabla ya hizo siku tatu).
 
UKIMWI mnavyouchukulia sivyo ulivyo, huu ni mradi kama BRT tu, by the way huwezi jua km umeathirika within 72 hours unless otherwise uwe unafahamu kama uliyefanya nae mapenzi ni muathirka. is ol I knw

Huwezi kujua kama umeathirika ndani ya masaa 72 ndio..Na wala ukienda clinic hawakupimi kama umeathirika au hujaathirika.

Wanachofanya ni kukuuliza maswali, kwa nn umehamua kufanya PEP kabla hawajakuanzishia hiyo dozi
 
Lengo kubwa la PEP ni kukinga watoa huduma za afya dhidi ya maambukizi baada ya kupata majeraha wakati wa kutoa huduma. Majeraha haya yanahusisha kumwagikiwa damu, kujichoma sindando, ama kujikata na vitu vyenye ncha kali wakati wakitoa huduma.

Huduma hii pia hutolewa kwa watu waliobakwa kama kinga ya virusi.

WHO | Post-exposure prophylaxis (PEP)

Post-exposure prophylaxis (PEP) is short-term antiretroviral treatment to reduce the likelihood of HIV infection after potential exposure, either occupationally or through sexual intercourse. Within the health sector, PEP should be provided as part of a comprehensive universal precautions package that reduces staff exposure to infectious hazards at work.

Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection, Fact sheet - 1 December 2014

Key facts
WHO | Post-exposure prophylaxis to prevent HIV infection

Globally, there were an estimated 35 million people living with HIV, of whom 13 million were on antiretroviral treatment (ART) at the end of 2013.

People can be accidentally exposed to HIV though healthcare work or due to exposures outside healthcare setting, for example, through unprotected sex or sexual assault.

Antiretrovirals (ARVs) have been used to prevent infection in case of accidental exposures for many years. This intervention is called post-exposure prophylaxis (PEP) and involves taking a 28-day course of ARVs.

PEP should be offered, and initiated as early as possible, for all individuals with an exposure that has the potential for HIV transmission, and ideally within 72 hours.

If started soon after exposure, PEP can reduce the risk of HIV infection by over 80%. Adherence to a full 28-day course of ARVs is critical to the effectiveness of the intervention.

Recent evidence shows PEP uptake has been insufficient: only 57% of the people who initiated PEP have completed the full course and rates were even lower at 40% for victims of sexual assault.
 
Asante kwa kunielewesha mkuu ray lee

Huwezi kujua kama umeathirika ndani ya masaa 72 ndio..Na wala ukienda clinic hawakupimi kama umeathirika au hujaathirika..wanachofanya ni kukuuliza maswali, kwa nn umehamua kufanya PEP kabla hawajakuanzishia hiyo dozi
 
Last edited by a moderator:
rpg Sio lazima iwe kwa watoa huduma za afya tu, kama ni kinga basi kila mtu anaweza kupatiwa!
 
Mbona madaktari wana ngoma au haijui?

Hii inafanya kazi kama utawahi kuanza matibabu(ndani ya siku tatu toka virusi kuingia mwilini)..so sio watu wote wanajijua wamepata virusi ndani ya muda huo.

Watu wengi wanajijua wanavirusi baada ya kupimwa na kukutwa navyo ina maana hapo inakuwa ishapita siku,miezi au miaka kadhaa tangu virusi kuingia mwilimi..so haya matibabu yanakuwa hayana maana kwa kipindi hicho
 
Watu naona wanahisi wamebaniwa. Ni hizo ARV tu. Ila hata wahudumu wa afya huwa wanaogopa kutumia, sijui kwa nini.
 
Mtu mwenye akili timamu hata akisikia tu yule ana ukimwi hawezi kumgusa, halafu mtu adinyane tena pekupeku huku akijipa matumaini ya kutumia PEP!!

Kaka naona umekuja kiushindani na sio kwa lengo la kuelimishana.Ndo mana nikakujibu vile nikijua na ww utajiongeza..wapi nimesema mtu ukazini makusudi na mtu aliyeathirika kwa vile kuna PEP??..

What if unafanya mpnz na mtu zen baadae/kesho yake unaambiwa yule ni mwathirika?..vipi kama ndugu yako wa damu ni muathirika na home ndo mnamuuguza zen ikatokea contamination yeyote kwa bahati mbaya??..wat bout ma-nurse na wauguzi wengine wa afya wanaowahudumia waathirika, nao wako kwenye risk ya maambukizi..sababu ziko nyingi,zote hizo hujaziona??
 
nahisi mnanichanganya kwa kusema masaa 72, vinginevyo uwe unatambua wazi umefanya na mwathirika
Si kila mkidinyana..ndo mana nikasema baada ya kuwa exposed na HIV( mf:umefanya mapenzi na muathirika na ukagundua mapema kabla ya hizo siku tatu).[/QUOTE]

Mtu mwenye akili timamu hata akisikia tu yule ana ukimwi hawezi kumgusa, halafu mtu adinyane tena pekupeku huku akijipa matumaini ya kutumia PEP!!

Kaka naona umekuja kiushindani na sio kwa lengo la kuelimishana.Ndo mana nikakujibu vile nikijua na ww utajiongeza..wapi nimesema mtu ukazini makusudi na mtu aliyeathirika kwa vile kuna PEP??..Wat if unafanya mpnz na mtu zen baadae/kesho yake unaambiwa yule ni mwathirika?..vipi kama ndugu yako wa damu ni muathirika na home ndo mnamuuguza zen ikatokea contamination yeyote kwa bahati mbaya??..wat bout ma-nurse na wauguzi wengine wa afya wanaowahudumia waathirika,nao wako kwenye risk ya maambukizi..sababu ziko nyingi,zote hizo hujaziona??
Ukileta uzi humu halafu ukatae maswali kulingana na kile ulichosema nadhani hilo litakuwa tatizo lako.

Sidhani kama ningekuuliza maswali niliyokuuliza kama ungetoa ufafanuzi kama huu uliotoa kwenye rangi ya blue mwanzoni, lakini badala yake ukaanza kujibu kwa kejeli na kuniambia kwa dharau "another swali plz".

:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
 
Ukileta uzi humu halafu ukatae maswali kulingana na kile ulichosema nadhani hilo litakuwa tatizo lako.

Sidhani kama ningekuuliza maswali niliyokuuliza kama ungetoa ufafanuzi kama huu uliotoa kwenye rangi ya blue mwanzoni, lakini badala yake ukaanza kujibu kwa kejeli na kuniambia kwa dharau "another swali plz".

:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:

Don't act a victim..ulikuja kubishana hapa sema labda ulikuwa hujajipanga vizuri...

Maswali mangapi yameulizwa na nimejibu??..nwei nafurahi umejishusha..[/QUOTE]
Mimi nijipange kwa hoja zako dhaifu mtu usiyejua hata ku-quote uzi wa mtu wewe, umevurugwa nini!. Yani ulipoona nimeamua kukuacha na dharau zako uliona nakuogopa sana umeona uendelee kunifuata fuata siyo? Endelea unachokitafuta utakipata muda si mrefu.

Angalia hapo juu unavyoandika hovyohovyo ndiyo uwe na hadhi ya kushindanishwa na mimi, umekopi na kupaste sehemu unatuletea humu hata kuandika vizuri hujui hayo maswali utaweza kuyajibu? Mburula wahedi....
 
grafani11 Wewe unauejua ku-quote ndo umefanya nn sasa..una-edit lakini still unakosea..naona umeanza kupiga beat hahahha!!..hizo beat wenzako wanafanya biashara we unazitoa bure.Nani huyo anayeshindanisha watu humu?? Naomba na mi nimjue
 
Last edited by a moderator:
rpg sio lazima iwe kwa watoa huduma za afya tu..kama ni kinga basi kila mtu anaweza kupatiwa

Unachosema ni kweli, nimeeleza pia kuwa watu wanaobakwa hupatiwa huduma hii! Huwa natamani kuduma hii itolewe kwa watu wanaopata ajari mbay, lakini siyo common practice kwa Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
Unachosema ni kweli, nimeeleza pia kuwa watu wanaobakwa hupatiwa huduma hii! Huwa natamani kuduma hii itolewe kwa watu wanaopata ajari mbay, lakini siyo common practice kwa Tanzania!

Vipi Kwa hapa tz ,ma-nurse wanaopata virusi wakati wa kutoa huduma,wanapatiwa hii treatment???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom