ERoni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 43,602
- 89,928
Nimeleta uzi huu MMU kwa sababu unaihusu jamii, hasa wanawake ambao kwa hili ni wahanga wakubwa.
Wiki iliyopita wote tulimsikia mheshimiwa kabisa akitoa tamko kuwa mtoto wa kike aliyeko shule akifanya kosa la kujibebesha mimba, hatorudishwa shuleni. Kwa maana kwamba mheshimiwa hataki kusomesha "wazazi".
Tamko hili limepokelewa kwa hisia tofauti, wapo wenye kumuunga mkono lakini pia wapo wanaopinga tamko la mheshimiwa, zikiwemo NGOs zinazotetea jinsia hii pendwa.
Kuna mambo ya kuangalia hapa, swala la utoaji mimba kwa dada/shangazi/wake/watoto wetu limeshamiri sana, hata kipindi ambacho hakukuwa na pingamizi la watoto kutorudi shuleni baada ya kujifungua. Kuna tafuti tofauti zimefanyika ndani na nje ya nchi, zikionyesha kuwa kati ya wanawake 10, watatu wamewahi kutoa mimba angalau mara moja. 30% sio kidogo ni idadi kubwa.
Katika hizi groups ambazo wengi wamekuwa hawapendi wake/dada zao wajihusishe nazo, kuna wanawake wanaofunguka kuwa wameshindwa kupata watoto kisa walijaribu kutoa mimba wakati fulani, wapo wanaokiri kutoa hadi mimba nne kabla ya kuolewa (staggering amount, four abortions?...God forgive us).
Sasa najiuliza, mheshimiwa kapiga pini kurudisha waliozaa mashuleni, manake uwezekano wa kuchoropoa mimba utaongezeka tu. Nini faida/hasara za hii pini/katazo? Tutegemee kuona kizazi cha namna gani baada ya miaka kumi-ishirini ijayo??