Faida na Hasara za Tamko la JPM kwenye jamii.

ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
43,539
89,698
Nimeleta uzi huu MMU kwa sababu unaihusu jamii, hasa wanawake ambao kwa hili ni wahanga wakubwa.

Wiki iliyopita wote tulimsikia mheshimiwa kabisa akitoa tamko kuwa mtoto wa kike aliyeko shule akifanya kosa la kujibebesha mimba, hatorudishwa shuleni. Kwa maana kwamba mheshimiwa hataki kusomesha "wazazi".

Tamko hili limepokelewa kwa hisia tofauti, wapo wenye kumuunga mkono lakini pia wapo wanaopinga tamko la mheshimiwa, zikiwemo NGOs zinazotetea jinsia hii pendwa.

Kuna mambo ya kuangalia hapa, swala la utoaji mimba kwa dada/shangazi/wake/watoto wetu limeshamiri sana, hata kipindi ambacho hakukuwa na pingamizi la watoto kutorudi shuleni baada ya kujifungua. Kuna tafuti tofauti zimefanyika ndani na nje ya nchi, zikionyesha kuwa kati ya wanawake 10, watatu wamewahi kutoa mimba angalau mara moja. 30% sio kidogo ni idadi kubwa.

Katika hizi groups ambazo wengi wamekuwa hawapendi wake/dada zao wajihusishe nazo, kuna wanawake wanaofunguka kuwa wameshindwa kupata watoto kisa walijaribu kutoa mimba wakati fulani, wapo wanaokiri kutoa hadi mimba nne kabla ya kuolewa (staggering amount, four abortions?...God forgive us).

Sasa najiuliza, mheshimiwa kapiga pini kurudisha waliozaa mashuleni, manake uwezekano wa kuchoropoa mimba utaongezeka tu. Nini faida/hasara za hii pini/katazo? Tutegemee kuona kizazi cha namna gani baada ya miaka kumi-ishirini ijayo??
c630ac19effdf84564a4c73959a95fca.jpg
 
Acha utetezi wa mambo ya hovyo.hili lifanye kwako wewe na familia yako.wakusanye watoto wako uwaambie kwako mimba ni RUKSA !!mila zetu zibatuzuia.na dini zetu pia zinatuzuia wewe unatushawishi kw kigezo gn??!! Ni upumbavu mkubwa sn.vijana woote wako shule wapigane mimba.wakiume afungwe miaka 30 na shule marufuku.lkn wakike yeye asome.HII HAIWEZEKANI. Kwanza nashauri wafungwe woote kw kuliaibisha taifa na kuitia hasara nchi.
 
Mzee hajakataza wazaziwatoto hao wasisome. Mmemuelewa vibaya. Amesema kumsomesha mtoto huyo litakuwa ni jukumu la NGO tetezi, Mbakaji (endapo hatafungwa) na wazazi wa mzazimtoto huyo.
Rais hajakataza mtu kusoma.
Naungana naye kutokutumia kodi yangu vibaya.
 
Hujaelewa ninachokusudia hapa. Hakuna sehemu nimetetea watoto warudishwe mashuleni. Naongelea madhara/negative impact ya katazo la raisi hasa kwenye utoaji wa mimba.

Kabla hajakataza, tunashuhudia utoaji mkubwa wa mimba, je kwa katazo hili, tutegemee nini?
 
Ni aslimia ngapi ya watoto wa kitanzania wanasoma private mkuu? Tuangalie wale tuliopitia shule za serikali+kayumba kwanza. Hao wa private si tayari wanajiweza!!!
 
Mzee hajakataza wazaziwatoto hao wasisome. Mmemuelewa vibaya. Amesema kumsomesha mtoto huyo litakuwa ni jukumu la NGO tetezi, Mbakaji (endapo hatafungwa) na wazazi wa mzazimtoto huyo.
Rais hajakataza mtu kusoma.
Naungana naye kutokutumia kodi yangu vibaya.

Amesema hata VETA n.k wakasome huko
Ila sio shuke za bure
Hivyi waende private schools wakasome. Hao NGOs kawaongelea kwenye kupokea pesa za kusaidia kama wanajali kmhaswa basi wafungue shule itakayosomesha wazazi hao... ni ameeapa ukwelim wanapewa pesa kusaidia wao eapo busy nchini wanavizia mengi ya serikali kudandia na huku wakihamasisha mabaya kwa watoto wa nchini. Na mengine mengi mazuri aligaongea JPM...

Inashangaza watu wameamua tu kwa kukosa la kuongelea serikali, kutamka na kuongopeana kuwa kawakataza wasisome kabisa.

Kiki ambayo 2020 bado hawataiona Ikulu, ni wamebuma kabisa.
 
Tusimjadili JPM please, sio lengo la uzi. Tuangalie impact ya katazo lake kwa jamii yetu, hasa swala la utoaji/uchoropoaji wa mimba.

Three out of ten wamewahi kutoa mimba at least once, hudhani hiyo idadi ni kubwa? Huoni kama inaweza kuongezeka mara dufu?
 
Sawa ila ujumbe ndio kiini cha nini la kuongelea na huyo aliyeandika hayo imebidi nimweleze yaliyosemwa.

Hata wewe kabla ya hotuba ile usingeyaongelea haya leo labda kesho kutwa.
 
Kuna wakati hata nahisi wazazi watakuwa wakiwapeleka watoto wakatoe mimba (God forbid).
 
Acha utetezi wa mambo ya hovyo.hili lifanye kwako wewe na familia yako.wakusanye watoto wako uwaambie kwako mimba ni RUKSA !!mila zetu zibatuzuia.na dini zetu pia zinatuzuia wewe unatushawishi kw kigezo gn??!! Ni upumbavu mkubwa sn.vijana woote wako shule wapigane mimba.wakiume afungwe miaka 30 na shule marufuku.lkn wakike yeye asome.HII HAIWEZEKANI. Kwanza nashauri wafungwe woote kw kuliaibisha taifa na kuitia hasara nchi.
Unaonekana mtu wa hovyo hovyo wewe katetea nini?
 
Sawa ila ujumbe ndio kiini cha nini la kuongelea na huyo aliyeandika hayo imebidi nimweleze yaliyosemwa.

Hata wewe kabla ya hotuba ile usingeyaongelea haya leo labda kesho kutwa.
Exactly my point, ujumbe na sio personality. Baada ya yeye kulileta kwa wananchi, we out to digest the message, sio yeye.
 
Hujaelewa ninachokusudia hapa. Hakuna sehemu nimetetea watoto warudishwe mashuleni. Naongelea madhara/negative impact ya katazo la raisi hasa kwenye utoaji wa mimba.

Kabla hajakataza, tunashuhudia utoaji mkubwa wa mimba, je kwa katazo hili, tutegemee nini?
Huko ndiko kutetea mimba mashuleni.unajificha nyuma ya madhara.mr eli7 hakuna haki bira wajibu.hatuwezi kuruhusu mimba kw kisingizio cha madhara.hebu fikilia ndg angu Eli7 una watoto 7 nyumbani kwako wa kike woote.na woote wako shule.mkubwa yupo kdto cha 2 wengne wako msingi mkubwa anarudishwa shule na mimba.unaitisha kikao cha familia unamfariji mwanao na kumwambia HAKUNA SHIDA MWANGU.UKIJIFUNGUA UTARUDI SHULE.jee unajenga taswira gn kw hawa mabinti zako wengne.UNAFUNDISHA NINI?
 
Uhalisia ni kwamba katazo la kutokuwasomesha hawa watoto halitafanya mimba ziishe mashuleni. Mimba zitaendelea kuwepo tu kama kawaida labda idadi ipungue japo sijui.

Kikubwa tutegemee..
1. Utoaji wa mimba mwingi
2. Watoto wa kike kutokusoma maana akishapata mimba na akagoma kutoa wazazi hawana uwezo kilichobaki atabaki nyumbani tu.
3. Tutegemee watoto wasio na future. Mtoto atakayezaliwa na mama aliyenyimwa elimu usitegemee ataandaliwa maisha ya baadae.
 
Ni kz ngumu kw kipofu km wewe kuona alicho tetea.huwezi kuona km huna macho!!
Wewe unafikiri watoto wanaopata mimba wameombwa mchezo tu wakatoa kwa ridhaa yao tu?

Je wanaobakwa?
Je waliokatika dhiki watu wanatumia nafasi kuwarubuni kwa karo au sababu zingine?

Je taratibu za kimila? Halafu unaniita kipofu?
 
Back
Top Bottom