zootopia
Member
- May 29, 2016
- 74
- 76
Leo nimeamua kuja na uzi huu kutokana na tatizo kubwa lililomo katika jamii yetu ya Kitanzania hususani sehemu za Mijini hasa miji mikubwa mikubwa. Vijana wengi wadogo (18-25) wamejikuta katika mahusiano magumu sana ya kimapenzi, kwakutembea na wamama wa mjini kimapenzi kwa lengo la kujipatia maisha marahisi (watoto wa mjini wanasema mteremko / ganda la ndizi).
Sasa leo ningependa tujadiliane pamoja "Faida na hasara za shuga mama kwa vijana wadogo" ili tuweze kuwasaidia/kuwaokoa na maisha hayo. Mimi binafsi nimewashuhudia baadhi ya vijana wadogo wakilelewa kimapenzi na mimaza mikubwa umri sawa na mama zao.
Hizi ni baadhi ya faida na hasara nilizoziona kwao;
FAIDA:
1.) Upendo wa dhati: Siyo utani hawa wamama wakimpata kijana wampendaye, huwa wanaamishia mapenzi yote kwa vijana hao, huwajali wapenzi wao wadogo na kuwadekeza kimapenzi.
2.) Kupata fedha nyingi bila kuzifanyia kazi: Vijana wengi hupatiwa pesa nyingi hata bila ya kuziomba kutoka kwa hawa wamama,mfano unaweza kukuta kijana yupo katika mizunguko yake au darasani unexpectably anapata muhala kwa simu yake, mara nyingine hupewa pesa nyingi baada kuwaridhisha kimapenzi.
3.) Kutatuliwa matatizo yao kirahisi: Wamama hawa hawapendi kuwaona wapenzi wao vijana wakilia lia shida, mara wanapogundua wapenzi wao wanatatizo au hawapo katika hali ya kawaida huwauliza shida yao na kuitatua kwa muda mfupi sana.
4.) Kupata experience ya maisha ya ndoa/mapenzi: Vijana wengi wadogo hujifunza mambo mengi yanayohusu mahusiano ya kimapenzi na hata ndoa, hivyo basi hata wakiachana na wamama hao hujikuta wakimudu mikiki mikiki ya kimapenzi kwa wapenzi wao wapya.
5.) Kupata baadhi vitu vya thamani vya ndoto zao: Baadhi vijana hawa hupewa vitu vya thamani vya ndoto zao kama vile; simu za bei kubwa, kupangiwa nyumba nzuri, kupata viwalo vya nguvu kama vile vya kimamtoni na hata kukabidhiwa magari mazuri (luxury cars).
HASARA (MADHARA):
1.) Kutawaliwa kifikra na Kimwili: Kutokana na umri wa vijana hawa kuwa mdogo, vijana hawa hujikuta wakitawaliwa kifikra na hata kimwili. Iko hivi, kijana anaweza akawa na mawazo yake mazuri na makubwa lakini yakapingwa na mama kubwa kwa kuambiwa mimi nilitangulia kuliona jua kuliko wewe kwahiyo huwezi nifundisha chochote, kwahiyo anakuwa ametaliwa kifikra.
Kutwaliwa kimwili ni pale kijana anapolazimishwa kufanya mapenzi wakati hajisikii, au anafanyishwa mapenzi kupita kiasi.
2.) Kuwa tegemezi: Kijana yeyote anayetembea na shuga mama hawezi kujitegemea mwenyewe au kujitawala mwenyewe, Mara nyingi huwaza kusaidiwa kila kitu hata akipata shida ndogo sana anaomba msaada. Na hii ni tabia mbaya sana maana kijana ambaye ana nguvu, akili na umri mzuri wa kufanya kazi anashindwa kufanya kazi.
3.) Kupoteza kampani na marafiki wa karibu: Marafiki wengi au watu wa karibu humtenga/kumkwepa rafiki yao anayetembea na shuga mama, ni kwasababu hawapendi konekana kwamba nao wanatabia kama hizo. Pia kijana anayetembea na shuga mama huwa anatumia muda mwingi na lijimama lake kuliko marafaki zake.
4.) Chuki na Uadui mkubwa: Na hili ni tatizo kubwa sana kutokana na wamama hawa kutawaliwa na wivu na chuki kubwa. Unakuta kijana hatakiwi kushika hata simu yake maana anaogopa eti atachati na videmu vyake. Kutokana umri / stage walizopo vijana hawa hujikuta wakitamani kufanya mambo mengi ikiwemo kuwa na mademu tofauti tofauti, tatizo linakuja pale anapofanya akiwa na lijimama lake, lijimama linaweza kuvimba mpaka na kupandisha sumu mithili ya cobra tena King Cobra na kuanza kumtishia mpenzi wake mdogo a.k.a MARIOOO.
Chuki hii au wivu auishiagi hapo, hata ukiachana naye anaweza kukufuatilia kila step katika maisha yako anaweza hata akakudhuru kama siyo kukudhalilisha. Visa vingine vinasema anaweza hata kukukill.
5.) Kupoteza muda: Hasara kubwa zaidi ni hii ya kupoteza muda katika maisha yako. Kijana kumbuka "time is money", unapopoteza muda unapoteza pesa pia. Shuga mama anakupotezea muda kwa kudanganya na vipesa vyake vya anasa. Usiwe mjinga tafuta pesa zako kwakutumia muda wako na akili uliyopewa na Mwenyenzi Mungu, usikubali kudanganywa kwa kupewa vitu vidogo vidogo kwani mwisho wake ni mbaya sana, utakosa lijimama na utakosa kila kitu alichokupa maana hawezi kukubali akutunze bure au atunzie wanawake wengine mume.
Kwa kifupi kabisa huo ni mchanganuo wangu au mtazamo wangu kutokana na tatizo hilo linalowasibu vijana wetu ambayo ndiyo wanaotegemewa kuleta mawazo mapya na mbinu mbali mbali za kukuza uchumi wa nchi yetu hii ya "HAPA KAZI TU".
Ningependa kuwasilisha mada kwenu wana JF wenzangu ili nanyi muweze kuchangia au kutoa maoni na ushauri wenu kwa vijana wetu wanaokua katika jamii zetu za Kitanzania zenye mashuga mama wengi kwasasa kutokana na ndoa nyingi kuvunjika au wanawake kujifanya hawataki ndoa eti wanajiweza wenyewe.
ASANTE.