JamiiTalks Faida na Hasara za Mitandao ya Kijamii kwa Vijana: Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo Hoteli ya New Africa

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Mdahalo huu ulifanyika Jijini Dar es Salaam Hoteli ya New Africa Tarehe 20 Oktoba na ulihusisha wanafunzi vijana na wahitimu wakisimamiwa na wabobezi na wadau wa Mtandao nchini.

Fuatilia hapa kilichojiri moja kwa moja katika ukumbi huo..

-----
20 October, 2018 JamiiFourms Debate & Discussion

Topic: Mitandao ya kijamii inawajenga au inawabomoa vijana wa Tanzania?

Venue: New Africa Hotel, Dar es Salaam.

KUJUA KUHUSU MDAHALO ULIOPITA, SOMA >"NAFASI ZA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI" - Yaliyojiri katika Mdahalo wa Wanachuo New Africa Hotel - JamiiForums

UTANGULIZI



Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media

Nichukue fursa kuwashukuru kwa ujio wenu.

Asili - Ni jumuiko la pili la midahalo, tunaita JamiiTalks. Tumeanza na wanavyuo ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutoa hoja nzito. Kwenye mdahalo huu ukiona kijana anatoa hoja kwa kupinga ujue sio mawazo yake ila anajaribu kujenga hoja na kujijenga(Capacity Building). Hatutaki kuwa na audience ambayo haihoji na isiyojiamini katika jamii.

Kwenye mdahalo huu wa leo tunaongelea 'Mitandao ya kijamii inawajenga vijana au inawabomoa?'.

Tuna majaji ambao watakuja kutoa majumuisho kwa jinsi hoja zilivyojadiliwa na washiriki tulionao.

UTAMBULISHO WA MAJAJI

Dr. Aikande Kwayu - Mhadhiri na Mtafiti

Anastazia Rugaba - TWAWEZA

Fausta Musokwa - Tanzania Media Foundation (TMF)

Agapiti Manday - COSTECH

Lusajo Mwaisaka - Mshauri masuala ya biashara

----------
UPANDE UNAOKUBALIANA NA HOJA


Mchangiaji namba 1 anasema;
Tanzania vijana wengi ndio wanaotumia Mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii inawasaidia vijana katika masuala ya elimu kupitia makundi ya kielimu

Mitandao ya kijamii pia inasaidia vijana/wanafunzi kupata ufadhili wa kielimu nchi mbalimbali

Mchangiaji namba 2 anasema;
Tokea kuibuka mitandao ya kijamii kuna watu walikuwa na mawazo hasi.Napingana na wanaosema mitandao inaharibu vijana. Hata runinga zilipokuja watu walisema zinaharibu vijana.

Mitandao ya kijamii Inasaidia kupata taarifa mbalimbali za masuala ya afya bila hata kumuona dakta (Fema,Femina, Afya Info)

Mchangiaji namba 3 anasema;
Inasaidia kujenga vijana hususani katika biashara. Zamani biashara ilikuwa lazima uwe na ofisi lakini sasa hivi mitandao inatumika kama soko na ofisi na inawafikia wateja kwa haraka zaidi.

Mchangiaji namba 4 anasema;
Kuunganisha watu kupitia mitandao ya kijamii. Mfano JamiiForums tumeona imeunganisha watu wa rika mbalimbali katika kujadili masuala mbalimbali. Watu wamekuwa huru kutoa maoni yao, hivyo mitandao ya kijamii ni muhimu kwa vijana kwa kuwasaidia kujadilia masuala ya maendeleo.

Mchangiaji namba 5 anasema;
Mitandao ya kijamii inawajengea uwezo vijana, inawasaidia kuibua vipawa na vipaji vyetu. Mfano Ebitoke, wachoraji mbalimbali. Vijana wanatengeneza vipaji na kuweza kujiingizia vipato.

Mchangiaji namba 6 anasema;
Mitandao ya kijamii inawasaidia vijana kupunguza msongo wa mawazo. Nilianza kutumia mitandao sio kwamba natafuta kazi bali nilitaka kuungana na watu ili niweze kujadili mambo mbalimbali. Sisi kama vijana tunatumia mitandao ili kuwasiliana na kujiburudisha, kupunguza mawazo. Ukiwa unaburudishwa haichagui dini, kabila wala unatokea wapi. Inasaidia akili ya kiafya nk

Mchangiaji namba 7 anasema;
Mitandao ya Kijamii inasaidia katika kufanya tafiti. Tafiti mbalimbali zinazofanywa na watu/wataalam na kupakiwa kwenye mitandao ya kijamii ili watafiti wapya waweze kusoma na kuangalia pale watangulizi waliposhindwa na kuendeleza wao. Tafiti hizi zinasaidia Jamii.

Mchangiaji namba 8 anasema;
Mitandao ya kijamii inakuza vijana wa Tanzania.Hapa inabidi tujiulize na tuelewe kwanini mitandao ya kijamii ilianzishwa? Watu gani watumiaji wa mitandao ya kijamii(Haina kizuizi lakini watumiaji wakubwa ni vijana).Kila mtandao wa kijamii umeanzishwa kwa malengo tofauti tofauti mfano (Instagram, Whatsapp,JamiiForums etc). Inasabisha vijana waweze kuwa wamoja kutokana na uwepo wa mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii ni chanzo cha kusababisha umoja kwa jamii. Mfano mdahalo wa leo umeratibiwa na mtandao mkubwa Tanzania na Afrika wa JamiiForums.

Mchangiaji namba 9 anasema;
Mitandao ya Kijamii inasaidia kurahisha upatikanaji wa habari kwa haraka.

Imerahisisha mawasiliano na imepunguza gharama ya mawasiliano nje ya nchi. Zamani ulikuwa unatuma barua ambayo ilikuwa inachukua muda.

Majumuisho
Mitandao ya kijamii imekuwa na manufaa makubwa kwa vijana na jamii kwa ujumla kwasababu imekuwa ni chanzo cha athari chanya kwa vijana wa Tanzania kijamii,kisiasa na kiuchumi.

UPANDE WANAOPINGANA NA HOJA

Mchangiaji namba 1 anasema;
Naangazia mitandao ya kijamii imeleta mshororo wa taarifa nyingi kwa vijana ambazo hazina tija wala umuhimu kwa vijana. Vijana wengi wamekuwa wakijikita katika kufuatilia mambo yasiyo na msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Mchangiaji namba 2 anasema;
Mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha kuvuruga vijana wengi wa Tanzania. Waziri wa Fedha na Mipango, mwaka 2016 aliwasilisha mpango wa pili wa maendeleo ya Tanzania ya Viwanda. Vijana tumeshindwa kujadili suala hili la mipango ya viwanda na kujadili mambo yasiyo na msingi.

Sasa hivi vijana wanajadili masuala ya 'UMAMA' kwenye mitandao ambayo yanashusha heshima ya mwanamke. Wengine wanajadili kuhusu 'Wanaume wa Dar' na kuacha kujadili masuala yenye tija.

Sheria ya mitandao ya Kijamii imekuwa ikiwasweka vijana wengi ndani kwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, vijana wengi tumekuwa wahanga wa sheria hii. Wengi tunajadili vitu visivyo vya msingi vya Kitaifa.

Mchangiaji namba 3 anasema;
Mitandao ya kijamii inapoteza pesa katika kuendesha. Unakuta kijana ana mtandao zaidi ya mmoja na yote anahudumia na kujadili vitu visivyo vya msingi. Kijana anatumia Tzs 2000 kujiunga na mitandao ya kijamii kila siku, pesa hiyo ni nyingi kwa mwezi.

Kupoteza maisha na kuleta athari kubwa- Vijana wa kike wamekuwa wakitegeka kwa tamaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kujihusisha na mambo haramu kama madawa ya kulevya nk.

Mchangiaji namba 4 anasema;
Mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwenye jamii ya Tanzania. Sisi kwa jamii yetu hatukujiandaa kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kama wenzetu. Watu wanaposti faragha zao na za kifamilia jambo ambalo sio salama. Vijana wanaposti mambo ya udaku kuliko ya kujenga. Watu wanaingia mkenge kwenye pages za udaku, wanapo-click wanasambaza taarifa zao kwa watu baki na zinaweza kutumika vibaya kuwabomoa.

Muda - Viajna wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kwa muda mrefu bila kupata muda wa kupumzika hivyo kupelekea kukosa muda wa kulala na kupelekea matatizo ya kiafya.

Tamaa - Kijana anatamani mambo makubwa ili aweze kushow off kwenye mitandao ya kijamii.

Mchangiaji namba 5 anasema;
Addictive, Depression

Mchangiaji namba 6 anasema;
Vijana kuamini kupata mafanikio kwa njia rahisi. Vijana badala ya kuwaza atumie njia gani apatae mafanikio ila yeye anawaza njia za mkato kupata mafanikio hivyo kujikuta anajiingiza katika mtego wa kufanya kazi haramu ili apate mafanikio ya haraka.

Upotoshaji wa taarifa - Mfano MO alivyotekwa kila mmoja alitamani awe wa kwanza kutoa taarifa wakati kuna Vyombo vinavyohusika.

Badala ya mtu kukaaa na kufikiri vitu vya muhimu kuhusu nchi ila kijana huyo anafikiria vitu visivyo na tija kwa jamii.

Mchangiaji namba 7 anasema;
Vijana wanatumia mitandao ya kijamii kuwashambulia na kuwaumiza wenzao kwa maneno bila kujali(Cyberbullying)

Sasa hivi baina ya vijana kumeibuka suala la UMAMA na WANAUME WA DAR jambo ambalo linadharaulisha na kushusha heshima na utu wa wanawake na wanaume.

Mchangiaji namba 8 anasema;
Mitandao ya kijamii imeongeza kiwango cha uhalifu(Criminality rate) kwa vijana. Vijana wengi wamekuwa wahanga wa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii inapumbaza. Watu wanatumia majina ya watu wengine(Fake accounts), mitandao ya kijamii inafanya watu waingilie mitandaoni(Hacking) ya watu wengine na faragha(Privacy).

***********************************************************

KUKABILIANA NA HOJA

WANAOKUBALI

- Mitandao ya kijamii iwe nyenzo ya kuwasiliana kwa urahisi.
- Economic development - Vijana wameweza kujiajiri kuliko kutegemea kuajiriwa.
- Tumekuja hapa JamiiForums kupitia mitandao ya kijamii, bila hivyo tusingejua kwamba kuna tukio kama hili.
- Tatizo sio la mitandao ya kijamii bali tatizo ni la watumiaji wa mitandao ya kijamii.
- Mitandao ya kijamii itumike kama ulinzi - Mfano Gwajima alisema watu wakija hapa siwaelewi elewi napiga nao selfie natuma kwenye mitandao ya kijamii ili likitokea baya waweze kujulikana

WANAOPINGA
- Mitandao ya kijamii inapelekea mmomonyoko wa maadili kwa vijna
- Sheria makosa mitandao
- Mifumo ya elimu iboreswhe ili vizazi vijavyo viweze kujua matumizi ya mitandao ya kijamii.
- Taasisi kama JF inaandaa mijadala hivyo vijana wajitokeze, kupitia midahalo tunajifunza mengi
- Ni wakati kama vijana kutumia mitandao ya kijamii kujadili vitu vya kitaifa na kimsingi vitakavyotupelekea kwenye Tanzania tuitakayo.
- Tuje na takwimu za kweli zisizopotosha


MAJAJI
Dr. Aikande Kwayu -

Utamaduni wa kujifunza na kusoma - Ukiwa na vitu hivi hata ukitengeneza hoja itakuwa na mashiko sana kwasababu utakuwa na uelewa mpana zaidi.

Kujiandaa (Kuwa serious na unachokifanya) - Hii inapelekea mchangiaji kujiamini

Kufanya kazi kwa pamoja(Team Work) - Hii nasaidia timu kuwa na mawazo sawa na kuepusha marudio kwa baina ya wachangiaji

Kuwa sensitive (Kutaja majina ya watu kwenye mitandao ya kijamii) - Tusipende kuwa mahakimu kwenye tabia za watu. Tusipende kuwazungumzia watu maana inaweza kuleta mtafaruku.


Anastazia Rugaba -

Nawapongeza sana, nawaona miaka mitano ijayo. JamiiForums iendelee na hii mijadala.

Kujiamini - Kukwepesha macho, kuzungusha mikono. Katika principles za uzungumzaji hayo mambo inabidi kutoyafanya. Kila gesture unayofanya ina maana katika uzungumzaji.

Muda - Zingatieni muda mnaopewa, wengi mlikuwa hammalizi muda wenu mliopewa. Tumia muda wako uliopewa mpaka uishe.

Vijana Taifa la kesho - Aliyesema vijana ni taifa la kesho, hiyo kauli aitoe kabisa. Anayesema kijana taifa la kesho anadidimiza vijana. Vijana ni Taifala leo

Maneno ya kutumia - Kuwa makini na maneno unayotumia na uyaelewe vizuri. Maneno kama 'uelewa wangu mdogo' sio maneno ya kutumia kwenye mijadala.

Utambulisho - Suala la utambulisho ni la muhimu na kuzingatia sana. Mtu kujitambulisha 'mdau' sio utambulisho rasmi

Kukosa takwimu, kufikiri na kukosa hoja si suala zuri.Lazima kuongea jambo unalolijua.

Matumizi ya Kiswahili - Ni muhimu sana kutumia Kiswahili fasaha. Kuna mtu mmoja ametumia kiswahili vizuri na misamiati mizuri.

Kurudia hoja - Mkiwa kwenye jopo msirudie hoja moja labda kama ulikuwa unataka kuiboresha.


Fausta Musokwa -

Lugha - Chagua lugha moja unayoweza kuitumia kwa ufasaha

Usikivu - Kusikiliza key points kutoka upande mwingine walivyosema ili uweze kujibu kwa ufasaha

Kujiamini - Ukijiamini unasema kile unachokiamini na kukielewa

Mifano - Tumia mifano na Takwimu sahihi

Agapit Manday -

Tafiti - Fanya Tafiti za uhakika kwa mnachotaka kuzungumza

Msimamo - Vizuri kuwa na msimamo na kupigania unachokiamini.

Kuzungumza points kwa mapana yake zaidi.

Mawakili - Wajumbe ambao ni Mawakili tunategemea sana kubeba makundi na kuja na facts, mkishindwa hapa huko mahakamani hamtaaminiwa.

Lusajo Mwaisaka -

Kufanya utafiti
Kujenga hoja yako kwa mapana

---
Paschal Mayalla - Moderator
Social media kuna uzuri na ubaya, tutafute usawa na kuchukua mazuri ya social media na yale mabaya tuyapigie kelele ili mitandao ya kijamii ilete maendeleo furaha nk.

Kwenye mitandao ya kijamii kuna watu wanaishi maisha ya kuiga. Haya sio matumizi mazuri. Ili uweze kufaidi matumizi ya mitandao ya kijamii ishi uhalisia. Kama unakaa Mbagala sema, usipige picha kwenye magari ya watu. Unajipandisha juu ili watu waone. Maskini wa roho itakuuma kuonesha watu upo juu kumbe upo chini.


Wahudhuriaji nao walipata wasaa wa kuchangia kama ifuatavyo...


Mjumbe namba 1
Vijana wanaweza kupashana habari mbalimbali za kisiasa. Mfano habari ya sheria ya kimtandao. Hata mimi nina blog naelimisha watu sheria ya makosa ya kimtandao.

Kiuchumi -Nina kitabu kinaelezea jinsi gani unaweza kujiongezea kipato kwa kutumia mitandao ya kijamii kama FB, YouTube nk.

Mjumbe namba 2
Mazuri ni mengi sana kwenye mitandao ya kijamii. Kila jema halikosi baya. Sasa hivi kuna utitiri wa TV za online. Unakuta mtu anaandika kitu kwenye kichwa cha habari kinatofautiana na kile kilichomo ndani. Hatujui tutawadhibiti Vipi. Kama wadau naomba tuangalie namna ya kushirikiana ili tuweze kuwadhibiti wote wanaopotosha.

Mjumbe namba 3
Huwezi kwenda kwa jirani bila kutokea kwako. Jirani ni mtandao wa kijamii. Je, kwangu(mimi) kupoje?

Waanzilishi wa mitandao ya kijamii hawakuwa na malengo mabaya. Sisi tunaotumia ndio tuna matatizo. Sisi tuwe na mabadiliko ya kifikra.

Mjumbe namba 4
Nitaelezea mazuri. Kuna habari hatutazipata kwenye vyombo rasmi lakini kwenye mitandao ya kijamii tunapata habari.

Mitandao imesaidia kuwajibisha viongozi. Wananchi wanauliza maswali kwa waheshimiwa kwenye makundi ya whatsapp na waheshimiwa wanajibu hivyo inaonesha uwajibikaji kwa viongozi wetu.

Mjumbe namba 5
Mitandao ya kijamii ina faida na hasara.

Hatujui kujifunza mazingira ya mitandao tunayoitumia. Mitandao sio mibaya ila sisi tunaoitumia ndio wabaya. Watu wengi tunatumia mitandao ta kijamii kuwaangamiza wale wanaofanya vizuri.

Mitandao ya kijamii wengi wanatumia kuchafua. Mitandao ya kijamii inatusaidia kuwa karibu. Nmenunua saa online na nimeletewa hii hapa.

Mjumbe namba 6
Kupitia mitandao ya kijamii imepelekea kukua kwa teknolojia. Inasaidia watu kusoma/kutoa elimu. Inaungamisha watu.

Sisi kama vijana tunatakiwa tujikite kwa lengo la kuingia kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii inasaidia sana kukuza teknolojia na hatujui kesho tutakuwa wapi.

Mjumbe namba 7
Nimepata kazi za kujitolea kupitia mitandao ya kijamii. Wanafunzi wengi tunaowatembelea wanasema wanatumia mitandao ya kijamii kuchat na marafiki zao.

Vijana inatakiwa watumie mitandao ya kijamii kutafuta fursa na kitu chenye faida.

Kwenye mitandao ya kijamii tuwe mabalozi kwa ndugu zetu na watoto wetu.

Mjumbe namba 8

Wizi, kuzushiwa na watu kubakwa yalikuwepo kabla ya social media.

Wakati naingia kwenye mitandao nilikuwa nawafuatilia watu maarufu. Baadae nikaamua kufuatilia vitu vya maana. Ni wewe mwenyewe kuamua. Niliacha kufuatilia watu maarufu na kurasa za umbea na kuanza kufuatilia kurasa zenye tija kama JamiiForums na sasa niko hapa.

Mjumbe namba 9
Mwanadamu ili akili yake na fikra yake ifanye kazi lazima ajiongezee maarifa. Ili kujua kitu hadi ukisome.. Mitandao ya kijamii inasaidia kuongeza maarifa na kupunguza Dhuruma.

Mitandao ya kijamii inaharibu ukaribu uliokuwepo. Licha ya kuandika andika tutembelee ndugu pia ili uweze kujua hali zao. Unaweza muuliza mtu kwenye mtandao wa kijamii hali yake akakuambia nzuri lakini sio kweli kwamba ni nzuri.

Mjumbe namba 10

Mitandao ya kijamii ni nini? Ni pale kunapokuwa na kubadilishana mawazo. Social media ni kama platform, inategemea sana unachezaje wewe. Unavyocheza ndo inategemea wewe unachezaje.

Anastazia Rugaba(Jaji)
Ukija kwenye usahili nakutafuta kwenye google. Nikiona hupatikani popote zaidi ya NECTA sikuchukui maana utakuwa mvivu na sio maarufu huwezi kazi. Naangalia unacho-post pia kwenye Mitandao ya kijamii. Tumieni online platform kuwa brand.

Mjumbe namba 11
Mitandao ya kijamii inatusaidia kupata kipato. Unaweza ukapata mkopo kwa account yako ya facebook kutokana na idadi ya wanaokufuata na unaowafuata. Mitandao ya kijamii inaongeza kujiamini.

Mjumbe namba 12
Mitandao ya kijamii inatusaidia kuwa na muda wa kufanya shughuli nyingine. Yaani unaweza kufuatilia kitu baada ya kumaliza kazi zako.

Mjumbe namba 13
Mitandao ya kijamii ni biashara.

Mjumbe namba 14
Faida za mitandao ya kijamii faida ni nyingi kuliko hasara. Challenges zinaweza kutatuliwa.

Ni vizuri tuwe na agenda ya kitaifa ya uwajibikaji wa pamoja kuanzia ngazi ya familia hadi ngazi ya kitaifa.


Paschal Mayalla(Moderator)
Social media ni ajira za watu. Watu waliokuwa wanatembea barabarani, ila sasa wanaoneka kwenye mitandao. Anakuwa kwake na list ya namba za wateja anafanya kuwapigia tu kwenda kupata huduma.

Nashukuru JamiiForums kwa kunikaribisha. Mimi pia ni member.


KUFUNGA
Maxence Melo - Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media


Shukrani kwa washiriki wote na hadhira.

Tutashirikiana na mentors ili kuwajengea uwezo wa kujenga hoja.

Kuna mambo ambayo hatuwezi kuyakwepa. Tusipotumia vya kwetu, tutatumia vya wenzetu.

Tutawakaribisha tena kwenye mdahalo mwingine utakaofanyika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.


PICHA ZA MATUKIO

0N4A1297.JPG

Kutoka kulia ni Dr. Aikande Kwayu, Lusajo Mwaisaka, Maxence Melo, Anastazia Rugaba, Fausta Musokwa na Agapiti Manday
(Jopo la Majaji)

DSC_0035.JPG

Kundi lilikokuwa likiwakilisha Wasiokubaliana na hoja

DSC_0037.JPG

Kundi lililokuwa likiwakilisha Wanaokubaliana hoja
 
Mitandao ya kijamii kwa sasa imekuwa ikipanua wigo wake wa mawasiliano kutoka kuwa mitandao ya kijumla na kuwa bayana zaidi. Kwa mfano watu wamekuwa wakitengeneza makundi ya fani fulani fulani ambapo inawasaidia wataalamu wa fani hiyo kukutana pamoja mtandaoni na hata kuongeza wigo wa kukutana uso kwa uso. Na hii imesaidia watu ambao wamekuwa wanataka kuingiza kwenye makundi ya fani hizo waweze kujumuika nao pamoja
Pia watu wanapata wachumba na michepuko
 
Hii mijadala ni mizuri na inasaidia haswa kujenga vijana....Tunamshukuru mpiganaji Maxence Melo na uongozi na wafanyakazi wa JamiiForums kwa ujumla.

Ila tunaomba siku nyingine mijadala kama hii wawepo watu kutoka kwenye mamlaka itasaidia sana....tunasikia maoni ya wananchi na pengine Wadau na wanaharakati mbalimbali bila uwepo wa mamlaka
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom